Mwanasheria Kuu wa Smz Zanzibar: asema Muungano unaweza kuvunjwa Pindipo Wananchi wa Z'bar wakitaka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanasheria Kuu wa Smz Zanzibar: asema Muungano unaweza kuvunjwa Pindipo Wananchi wa Z'bar wakitaka.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jul 21, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][​IMG][/h] Mwanasheria Mkuu wa Serekali ya Mapinduzi ya zanzibar Mh othman Masoud Othman


  Na Mwinyi Sadallah

  20th July 2012

  Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaweza kuvunjika kama wananchi hawataridhishwa na misingi ya muungano wenyewe.
  Alisema hayo wakati akifafanua hoja za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) mjini Zanzibar, baada ya kuchangia bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria katika kikao kinachoendelea huko Chukwani.
  Alisema si kweli kwamba muungano wa Tanganyika na Zanzibar hauwezi kuvunjika kama wanavyoamini baadhi ya watu.
  “Sio kweli kwamba muungano hauwezi kuvunjia…unaweza kuvunjika kama wananchi watakuwa hawakuridhishwa na misingi ya muungano wenyewe” alisema.
  Alisema kwamba, kasoro za kikatiba katika mungano wa Tanzania zilianza kuonekana tangu kuasisiwa kwa kwake mwaka 1964 na kusababisha malalamiko kutoka pande zote mbili za muungano huo.
  Othman alitoa mfano kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuchaguliwa kuwa Rais bila kupata kura hata moja Zanzibar au jimbo la uchaguzi kwa chama chake.
  Aidha, alisema katika Katiba ya Tanzania kuna vifungu vingi vya sheria vimekaa kimya kuhusu nafasi ya Zanzibar katika muundo wa muungano kutokana na kusema Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano bila ya kuweka wazi kama nchi mkoa au wilaya.
  Mwansheria huyo alisema tatizo kubwa la muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kwamba haujajengwa na misingi mathubuti wakati wa kuanzishwa kwake.
  “Muungano huu hauna tofauti na watu waliojificha katika boksi na kushindwa kufahamu kinachoendelea nje na kujikuta wakipoteza hewa” alisema.
  Alitoa wito kwa wananchi kutumia nafasi ya kutoa maoni katika Katiba mpya yatakayosadia kuimarisha muungano huo.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa Zanzibar wenye kulinda Muungano kwanza Wajiulize Jee huyo mshirika wa Muungano Tanganyika Ipo? na Kama ipo ipo wapi? na nivikao vingapi vya Tanganyika vilivyo kaa kujadili mambo ya Tanganyika tu yasio ya Muungano?.

  Mimi nasema hii Tanzania ni Sawa na ile Zaire kuita Kongo ndio Tanganyika hii ya leo Tanzania na ukitaka mfono mfupi kujuwa ni kuona nafasi zote za juu ni wao na hata mambo ya sio ya Muungano wao husema ni ya Muungano mfano mawaziri wote wa Tanganyika wale wasiwa wa Muungano ni Wa Tanzania.
   
Loading...