Mwanasheria azungumzia uzushi wa kifo cha Gwajima

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Peter Kibatala ambaye ni mwanasheria wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameeleza kusikitikishwa na taarifa zilizosambazwa kuhusu kifo cha mteja wake wikendi iliyopita.

Taarifa za uzushi zilizosambaa hususan kwenye mitandao ya kijamii zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia wakati akipewa matibau katika hospitali ya TMJ iliyoko Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Uzushi huo uliutaja ugojwa wa saratani ya damu kuwa chanzo cha kifo cha askofu huyo.

“Nimesikitishwa na taarifa hizi na nimepigiwa simu nyingi sana leo kuniuliza juu ya kifo cha Askofu Gwajima na nimebaki nashangaa kwani ni mzima wa afya,” alisema wakili Kibatala.

Kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao, ni kosa kuandika au kusambaza habari zisizo za kweli. Hivyo, mkono wa sheria unaweza kuwashukia walioeneza habairi hizo.
 
Ni wakati sasa umefika tuone wale wote wanaoeneza taarifa za uzushi tuone wakishughulikiwa hadharani, this is too much.

Where is Cyber crime law!
 
UNAJUA NINI:
MTU AKIZUSHIWA KIFO NI KWAMBA JAMII HAIMPENDI NA LISEMWALO MIDOMONI MWA WASWAHILI...LIPO AU LITATOKEA KWA 89.80%
 
Hebu ngoja nione sheria zitakazochukuliwa juu ya waliosambaza taarifa hizo za uongo.
 
Back
Top Bottom