samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Wana jf nimesikitishwa na kitendo cha mwanasheria tena wakili mpya kabisa aliyeapishwa jana tarehe 17/12/2010 na jaji mkuu anashindwa kutoa maoni yake kuhusu uhitaji wa katiba mpya!!! Alipoulizwa nini maoni yake kuhusu kuwepo kwa hitaji la katiba mpya wakili huyo ambaye ni mwanamke alisema yeye hawezi kuzungumzia masuala ya "kisiasa"....Nilipigwa na butwaa niliposikia mwanasheria anasema suala la katiba ni suala la kisiasa.....!!!!!