Mwanasheria anaposhindwa kuzungumyia katiba mpya

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
1,250
Wana jf nimesikitishwa na kitendo cha mwanasheria tena wakili mpya kabisa aliyeapishwa jana tarehe 17/12/2010 na jaji mkuu anashindwa kutoa maoni yake kuhusu uhitaji wa katiba mpya!!! Alipoulizwa nini maoni yake kuhusu kuwepo kwa hitaji la katiba mpya wakili huyo ambaye ni mwanamke alisema yeye hawezi kuzungumzia masuala ya "kisiasa"....Nilipigwa na butwaa niliposikia mwanasheria anasema suala la katiba ni suala la kisiasa.....!!!!!
 

Babkey

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
4,832
2,000
No name, no source...what the hell!!?!

But damn...tehtehteh....

Ni kweli na ilikuwa Mlimani Tv taarifa ya habari usiku.
Kushindwa kuzungumzia katiba kwa wao ni kawaida. Kumbuka wanaingia kwenye serikali inayopenda kulindwa hata kwa maovu wanayofanya na wao waliapishwa kuwa Mawakili wa serikali. Kwa muonekano wanahitaji katiba mpya, ila ni waoga na hawako huru kulizungumzia hilo hadharani.
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,983
2,000
Ni kweli na ilikuwa Mlimani Tv taarifa ya habari usiku.
Kushindwa kuzungumzia katiba kwa wao ni kawaida. Kumbuka wanaingia kwenye serikali inayopenda kulindwa hata kwa maovu wanayofanya na wao waliapishwa kuwa Mawakili wa serikali. Kwa muonekano wanahitaji katiba mpya, ila ni waoga na hawako huru kulizungumzia hilo hadharani.

Ndo tatizo la bongo hilo. Kila kitu ni bush-league..si ma lawyer wala madaktari au so called wataalam wengine. Wote ni bogus tu.

Sasa huyo anadaiwa kusema kuzungumzia katiba ni kuzungumzia masuala ya "kisiasa"....mweeee

Katiba ni suala la sheria. Ni sheria zinazoiongoza nchi...sasa huyu mwanasheria hata ku spin hajui (hiyo kama ni kweli alisema hivyo)

Bogus kabisa....
 

Ntambaswala

JF-Expert Member
Dec 7, 2008
255
195
Ndo maana watu wanasema kuna tofauti ndogo sana kimtazamo, kiakili na uwezo wa kupambanua issues kati ya mhitimu wa kidato cha sita anayefuatilia issues na mhitimu wa shahada ya kwanza, kadhalika mwenye shahada ya kwanza na ya uzamili ( kutoka kwenye vyuo vingi vya hapa bongo). Fuatilia hasa kwa wanafunzi toka vyuo hivi: Saut, tumaini, tia, mzumbe, ifm, cbe na hata udsm.

Tatizo la hawa watoto wetu ni kuwa wakishamaliza shule, basi ndo mwisho wa kusoma, wao ni kuangaalia Chnnl O, EATV, Clouds, Facebook na kusoma magazeti ya udaku. Maarifa mengi ya namna ulimwengu unavyokwenda hayapo kwenye lecturer rooms ni lazima uwe unafuatilia current news ndo unaweza kusimama mahali hata ukihojiwa utazungumza la maana.

Shame kwa huyo mwanasheria, wish tungejua jina lake..............................................
 

KIBE

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
943
0
ndo maana watu wanasema kuna tofauti ndogo sana kimtazamo, kiakili na uwezo wa kupambanua issues kati ya mhitimu wa kidato cha sita anayefuatilia issues na mhitimu wa shahada ya kwanza, kadhalika mwenye shahada ya kwanza na ya uzamili ( kutoka kwenye vyuo vingi vya hapa bongo). Fuatilia hasa kwa wanafunzi toka vyuo hivi: Saut, tumaini, tia, mzumbe, ifm, cbe na hata udsm.

Tatizo la hawa watoto wetu ni kuwa wakishamaliza shule, basi ndo mwisho wa kusoma, wao ni kuangaalia chnnl o, eatv, clouds, facebook na kusoma magazeti ya udaku. Maarifa mengi ya namna ulimwengu unavyokwenda hayapo kwenye lecturer rooms ni lazima uwe unafuatilia current news ndo unaweza kusimama mahali hata ukihojiwa utazungumza la maana.

Shame kwa huyo mwanasheria, wish tungejua jina lake........

......................................


binafsi mi naona tatizo sio vyuo tatizo ni wanafunzi wenyewe. Hivi kweli mwalimu ndo akauambie uangalie bbc,cnn? Usome magazeti ,uangalie taarifa za habari ,ufatilie mambo mbalimbali yanayoendelea duniani? Hapani si kazi ya mwalimu ni wewe mwenyewe mwanafunzi.
Walimu wanawafundisha vizuri sana tena sana lakini wanafunzi wa siku hizi sio wafatiliaji wa mambo kazi kwenda club,matamasha wkend mishikaki basi na wakiwa nyumbani wao ni filamu za kina kanumba . Sasa hapo utaongeza nini katika taaluma yako? Wengi hawasomi.
Binafsi nimeshuhudi mwanasheria hajui hata kuanda charge cheet!!!!!.
Na hata ukifatilia upatikanaji wa uwakili wa sikuhizi ni wa kujuana tu. Na ninavyujua mimi ni jopu la majaji na wtalamu wengine wanakaa na wanawafanyia usaili only one day na kwa dakiki kazaa ukipita hapo uwakili unao.
 

quimby_joey

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
383
250
Lazima tuelewe kuwa wahitimu wengi siku hizi wanapata degree zao kwa njia nyingi hasa dada zetu. nina mifano ya watu walioapishwa jana kuwa mawakili ambao nilikuwa nao chuoni wakati huo alikuwa hawezi kufanya mtihani peke yake bila msaada wa 'kibomu' au washkaji. lakini walimaliza na kwenda law school huko ndo ilikuwa balaa kabisa. tuliwashuhudia kwa macho kwenye oral examination wakitoka wanalia kwa kushindwa kujibu kabisa maswali lakini matokeo yalipotoka 'ubao' ulisomeka safi na jana wameapishwa.

Rai yangu kwa wananchi ni kuwa tuwe makini pindi tutakapohitaji wataalimu kutatua matatizo yetu. Tumeshaona daktari mmoja Muhimbili aliyemfanya mtu operesheni ya kichwa wakati ana matatizo ya miguu, mgonjwa anapewa dozi ya malaria wakati anaumwa tumbo, sasa tusishangae siku zijazo mtu akahukumiwa kunyongwa kwa kosa la wizi, wakili anachukua pesa ya mteja halafu haonekani mahakamani....kuna siku nilishuhudia mwenyewe kituko hiki ambacho naweza kusema ni aibu ya mwaka pale Land Tribunal ya Ilala, wakili mmoja kutoka law firm ambayo mmoja wa partners wake ni aliyekuwa waziri wa wizara nyeti ambaye kapigwa chini huku nyanda za kaskazini na kung'oa viti vyote vya iliyokuwa ofisi yake, wakili huyu alishiriki kwa asilimia mia kumweka rais wetu wa sasa madarakani , pia alihudhuria kuapishwa kwa girlfriend wake jana...jamaa alipoulizwa na mwenyekiti wa baraza shauri lake lilipotajwa akasema yeye amamtetea "ACCUSED PERSON" ikabidi mwenyekiti amuulize mara ya pili nae akarudia kujibu vilevile tena kwa msisitizo, ikabidi mwenyekiti apotezee kiaina pasipo kumrekebisha kwa kuogopa kumchafulia JINA. katika mabaraza ya nyumba hakuna ACCUSED PERSON, pale kuna walalamikaji na walalamikiwa, hakuna kesi ya criminal inayoendeshwa pale....huo ni mfano tu mmoja waungwana...NACHANGIA!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom