Mwanao anaongoza darasani au alikua anaongoza, nini ulifanya kufanikisha hilo?

Muvi za kitoto ni zipi? Zile katuni zs wazungu? Zs ku fanya watoto kuwa wajinga?

Juzi Ijumaa palikuwa na mkutano wa kitaifa wa wadau wa elimu kujadili mitaala na mustakabal wa elimu Tanzania. Mtoa mada mmoja alitukumbusha umuhimu wa kuzingatia ukuaji wa ubongo wa mtoto katika miaka michache ya kwanza. Alisema, watoto wa kizazi hiki cha simu za kupangusa na senema za katuni, zina stimuli nyingi zinazokuza miunganiko ya nyuroni kipindi cha ubongo kukua. Hoja yake ni kwamba watoto hao wana bongo zilizo na miunganiko mingi, hivyo zenye uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo.

Hivyo Ubongo Kids, muvi za kitoto za katuni za wazungu haziko kufanya watoto wawe wajinga. Hata hivyo, kuwa makini na muvi zipi. Reviews for what your kids are into (before they get into it) | Common Sense Media wanazo review nzuri za kujua muvi ipi inafaa, ipi haifai.

Pana kitabu cha Maria Montessori -- The Absorbent Mind

Montessori anasema miaka 0 - 3 , na miaka 3-6 ni muhimu sana kwenye makuzi ya akili ya mtoto. Ukikosea hapo unakuwa na kazi kubwa baadaye.


 
Nimemtoa kijijini akiwa la PILI nimemleta mjini mwaka jana akawa wa 54 kati ya watoto 218, kipindi hiki kawa wa 3 kati ya hao hao 218 sijampeleka tuition, nimemnunulia vitabu na anapata muda mwingi wa kujipangia ratiba ya kusoma simpangii mimi. Mahakikisha tangu aje mjini hatembei hovyo! Vipindi vya TV ni vile vinaendana na elimu.

Kiukweli hata sijui ni njia gani zinampa uwezo mkubwa hata akiwa kijijini alikuwa anashika 1 & 2 tu.

Sijui niseme karithi kwangu !!!? Yawezekana.
 
Japo umeiweka kama utani, ni kwamba huyu mwamba nafasi yake ni ya 72 kati ya watoto 100…just in case..
Mtoa hoja anatutaka sisi wenye watoto wanaocheza kwenye top ten tumpe mbinu... Sasa hiyo 72 inatoka wapi?
 
, mdogo wangu alikua anashika nafas ya kwanza kwanzia darasa la 1 had la 3 kati ya wanafunzi 80 darasani ila alivyo hamishwa shule akaanza kuwa wa 13+ kat ya watoto 40 hajawahi kuwa ndan ya top 10
Lakn uwezo huo huo alio nao akirudishw kule alipotoka atawaburuza tena inategemeana anaoshindana nao wana uwezo kiasi gani
Hilo ndio swala la muhimu
 
Mie pia nilikua napata nafasi ya tatu hadi ya tano lakin aikumbuki kama ni kwa mapenzi yangu au ni zile fimbo za baba maana baada ya hapo sipendi kusoma kabisa hadi leo

bhasi hukuwa na hiyo passion ila mwanao anayo lakini pia inawezekana anapenda competition ama kukubalika kama mwamba. Hivyo hata akishuka kwa nafasi moja inaweza kumuumiza kuliko unavyofikiria kwa sababu hizo namba kwake ni zaidi ya ufaulu tu mkuu

Nakumbuka pia O'level nilikuwa na friend ambaye kwake namba mbili ilikuwa sio namba na alikuwa anahustle kweli kweli, Mwisho wa siku mtihani wa mock form 4 akapitwa na mshindani wake mkubwa. Alilia siku ya tokeo na cheti cha Academic alipokikosa pia ilimliza

so, jitahidi kumuelewa na umpe emotional assistance pale inapohitajika maana umezaa kichwa
 
Kwa uzoefu wangu mazingira yanaweza kuathiri sana lakini kwa ushauri wa bure jitahidi kumnunulia vitabu. Maana tuition zingine hamna kitu mi n mwalimu wa tuition mbalimbali kuna mengi hua nayaona. Pili mbane mtoto mfano hakikisha anafanya homework zake. Lakini pia akifanya vizuri mpe zawadi hii itamuongezea kujituma sana. Over
 
Back
Top Bottom