Mwanao anaongoza darasani au alikua anaongoza, nini ulifanya kufanikisha hilo?

inaonekana hiyo tabia ya kufaulu kwa kiasi hicho hajairithi kwako kabisaaa kwa hiyo jitahidi tu kumuelewa
Mie pia nilikua napata nafasi ya tatu hadi ya tano lakin aikumbuki kama ni kwa mapenzi yangu au ni zile fimbo za baba maana baada ya hapo sipendi kusoma kabisa hadi leo
 
Kama huna akili hata usome cambridge hufiki kokote ,mzazi kutambua umuhimu wa elimu hakumsaidii mtoto kilaza,akili ni vipaji vya kurithi genetically inherited
Unaongeleaje shule zilizofaulisha wawili katika mia na wengine wakapata fursa ya kurudia katika shule bora na wakatusua mpaka juu huko

Pia unaongeleaje ambao hawakupata fursa kama hizo za kurudia katika shule bora
Hawa wote wewe unawaweka katika kundi la wasio na akili?
Private school nyingi zinapokea rejected
Lakini mbona zinaongoza

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru hata mimi mwanangu yupo kwenye topu teni, alikuwa wa 8 kati wa wanafunzi 11. Ninachofanya ili asitoke kwenye topu teni ni kumsisitiza asome. Asandi sana
Top 10 then? Je huyo mtoto Maisha halisi anaweza pambana? Ukiacha huo u top 10?
We tulia tu, najua mwanao anabeba darasa.. tuachie ss wa topu 10
 
Mtengenezee mwanao motisha ya kusoma.

Sio kumjazia TU mavitabu Kama ndugai
IMG_20210218_174706.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru hata mimi mwanangu yupo kwenye topu teni, alikuwa wa 8 kati wa wanafunzi 11. Ninachofanya ili asitoke kwenye topu teni ni kumsisitiza asome. Asandi sana
Japo umeiweka kama utani, ni kwamba huyu mwamba nafasi yake ni ya 72 kati ya watoto 100…just in case..
 
Unaongeleaje shule zilizofaulisha wawili katika mia na wengine wakapata fursa ya kurudia katika shule bora na wakatusua mpaka juu huko

Pia unaongeleaje ambao hawakupata fursa kama hizo za kurudia katika shule bora
Hawa wote wewe unawaweka katika kundi la wasio na akili?
Private school nyingi zinapokea rejected
Lakini mbona zinaongoza

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kuwa rejected haimaanishi huna akili.we kubali tu kuna watoto hawana akili wako wengi tu vichwa vigumu hata ufanyeje utapiga itaua,utabadilisha shule zote
 
Yani hii elimu sijui ikoje,huko nyuma Yani olevel na advance nilikuwa na uwezo wa kuwaelekeza wenzangu kuhusu masomo na maswali yake kwa ufundi mkubwa ila Cha ajabu nikiandika Mimi majibu kwenye mtihani sifaulu kiwango Cha juu naishia kupata alama za wastani tu ,ila kufika chuo kikuu nikajikuta nikisoma tu kidogo imoo, pepa ikija naionea kweli mpaka Sasa najiuliza kilichonifanya nisifaulu kwa daraja la juu kabisa huko olevel na advance ni kitu gani,kumbe nikaja kupata majibu kuwa nilihitajika kukariri vitu vingi huko nyumaa...kwa hiyo Cha msingi ni kuhakikisha mwanao anaelewa tu Mambo Mana Mambo ya kushika namba moja ndo yanayowaharibu watoto kisaikolojia,we mtengenze kisaikolojia tu ilmradi yy aelewe Mambo vizuri tu kama vile sayansi na hisabati pia apate muda wa ziada wa kufanya kazi ndogondogo kwani akizidi kukua utaona anabadilika tu utashangaa...
 
Saa nyingine ni bahati tu na Mungu kuwasaiadia . Nina watoto wanne na wote wamekuwa wakiongoza na wawili wameshamaliza chuo kikuu wanaendelea na Masters degree na mwigine yuko mwaka wa mwisho kumaliza degree yake. Wa mwisho yuko form five na alipata A+ masomo yote kidatu cha nne. Katika hayo sina sana msaada mkubwa wa kusema mimi ndiye nimewawezesha na niseme tu Mwenyenzi Mungu ndiye amewasaidia.
 
Mwanangu nataka awe wa kawaida tu wana simpi presh.

Kwenye familia yetu mimi ndio nlikuwa na akili sana za darasani lakini nliishia kusota mtaani na nikapata ajira kwa connection za bro wangu.

Bro na sista wangu walikuwa na uwezo mdogo darasani, tia maji tia maji, lakini walihitimu vyuo hivyo hivyo, Bro na sista kwa sasa wana mpunga wameniacha mbali sana,

Mdogo wangu saizi yupo anamsaidia bro kwa lengo nae aje ajiajiri baadae kwenye biashara,

Mshahara wangu si haba, unacheza kwenye 1.8 hivi baada ya makato lakini hii pesa bro na sista kwao ni ya kawaida tu, nao walianza chini mpaka wapo mbali kwa sasa, sista alibebwa sana na bro, saizi ana restaurant zake na anafanya deleivery maofisini, pesa kaipata kwakweli, kuhusu bro yupo biashara za usafiri na makazi.

Huyu dogi nae sio muda anaweza nichapa gepu, na mimi saizi nna biashara ila chamoto nakipata maana muda mwingo sipo dukani.
 
Pole sana..

Kabla ya kumlaumu mtoto hafanyi vizuri, jiangalie nyie kwanza wazazi, je mlishwahi kufanya vizuri...
Mtoto wa nyoka ni nyoka...
 
Wapo wa aina hiyo ndugu. Ninaye mmoja hapa nilijitahidi naye sana. Nikampeleka hadi private nzuri. Amerudia madarasa wee... Mwishoe alileta mjukuu nyumbani... Sasa hivi nimempeleka village akajaribu jembe.
Hello bosses,

Kama mwanao anaongoza darazani angalau nafasi 10 za juu.

Je, nini ulikifanya kufanikisha hilo?,

Mtoto anapata shule nzuri, tuition za kutosha, muda wa kupumzika, homework n.k lakini bado maendeleo yake ya shule sio ya kuridhisha.
 
Kula cartoon na mwanao mzee..
Baadhi ya ambazo sisi tumeshakula;
1. Chicken run
2. Madagascar...
3. Puss in boots
4. Coco
5. Shrek
6. Ice age
7. Khumba
8. Frozen/Elsa
9. Ralph breaks the internet
10. Zootropia
11. Hotel translvania
12. Ballerina (Ballery dance...)
13. Barbie
14. Etc.

Sisi tunasubiri tufike P5 tuanze shule rasmi.. Kwasasa tunaelezana concept ndogo ndogo tu..
Tatizo muda
 
Hello bosses,

Kama mwanao anaongoza darazani angalau nafasi 10 za juu.

Je, nini ulikifanya kufanikisha hilo?,

Mtoto anapata shule nzuri, tuition za kutosha, muda wa kupumzika, homework n.k lakini bado maendeleo yake ya shule sio ya kuridhisha.
Sina mtoto ila nitakupa mbinu alizotumia mzee wangu ili mimi binafsi niweze kufanya vizur katika masomo yangu
1. Constant follow-up jitahidi sana uwe unafatilia maendeleo ya mwanao kwanzia homeworks, test na mitiani
2. Hakikisha unatengeneza urafiki na walimu wake ilihali iwe virahisi wao kumfatilia unapokua mbali naye
3. Jitahidi kumpa rewards na kumtia moyo pale anapoanguka.
4. Epuka kumfananisha na watoto wa fulani bali jitahid kumwambia story zako za ushindi ulipokua shule
5. Wajue marafiki zake na uwe unawatia moyo na kuwakazania juu ya kusoma wakiwa pamoja
 
Mimi wa kwangu mara ya kwanza alitupwa 34 kati ya 78 alivyorudi nikamwambia aniambie nini tatizo akasema vitabu na nimpeleke tuition mimi huwa ni mbishi lakini kwa hilo nikamtimizia juzi kaniletea no.3 katu ya 78 nikasema hapo sawa.
 
Back
Top Bottom