Mwananzila: Tulikurupuka sekondari za kata

Augustoons

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
409
30
Mwananzila: Tulikurupuka sekondari za kata
na Mwandishi WetuSERIKALI ya Awamu ya Nne, imekiri kukurupuka katika ujenzi wa sekondari za kata ambazo kwa asilimia kubwa zimekosa sifa za kupokea wanafunzi, upungufu wa walimu na vitabu.
Akizungumza wakati wa mahafali ya tatu ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya St Matthews, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ludovic Mwananzila, alisema uamuzi huo unaigharimu serikali.

Pamoja na hayo, Mwananzila aliweka wazi kwamba kufutwa kwa michepuo ni sababu nyingine inayoendelea kuathiri sekta ya elimu Tanzania.

Alisema, katika kuhakikisha kwamba shule za kata zilizohimizwa kujengwa nchi nzima, zinakuwa na michepuo ya maabara, karakana na kuajiri walimu wa kutosha wenye sifa, serikali pia itatoa mafunzo ya kiwango cha juu kwa walimu wa sekondari hizo.

“Haiingii akilini kuona shule ina mwalimu mmoja…hili ni jambo lisilowezekana hata kama shule hiyo ingekuwa ina darasa la kwanza tu,” alisema naibu waziri huyo.

Katika kuhakikisha kwamba serikali kupitia wizara yake inaboresha kiwango cha elimu nchini, Mwananzila alibainisha kuwa lengo la serikali ya Awamu ya Nne, kwa sasa ni kuangalia jinsi itakavyotoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu.

Naibu waziri huyo aliwataka wanafunzi wanaokopa kurejesha mikopo hiyo mara wanapoanza kazi, ili kuwasadia wengine wanaojiunga na vyuo hivyo.

Awali akimkaraibisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa shule hiyo, Thadeus Mtembei, aliitaka serikali kuziboresha shule za kata ili zikidhi sifa sambamba na vyuo vya ufundi kwa lengo la kuajiri wanafunzi wanaomaliza mafunzo mbalimbali.

Naye Mkuu wa Shule hiyo, Charles Mtenga, alimpongeza mkurugenzi huyo, kwa kutenge sh milioni 20 kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki na fedha taslimu kama motisha kwa walimu wanaofaulisha vizuri hali inayochangia ukuaji wa taaluma na ufaulu wa wanafunzi wao.

Jumla ya wanafunzi 219 wa shule hiyo walihitimu na kutunukiwa vyeti huku baadhi yao wakijizolea zawadi mbalimbali na nyingi kati ya hizo zilikwenda kwa wasichana walioongoza kitaaluma.
chanzo:Tanzania daima 14/1/2008
KWAKWELI HII NAYO KALI.
Hawa jamaa sijui wanapopanga mipango yao sijui huwa wanafanya utafiti? au sijui huwa wanaota ndoto tu na kuanza kutekeleza? wana JF hii serikali sometimes nashindwa kuielewa. Wizara ya elimu imekuwa wizara ya majaribio ya sera,kila waziri akija anakuja na msimamo wake matokeao yake ni kuwa na mawaziri karibu kumi na misimamo kumi tofauti.Halafu cha kushangaza mara wanapoanza kutekeleza mikakati hiyo ukiwapinga wanakuwa wakali kama pilipili na wa kwanza kukanusha. Ona sasa aibu inavyowapata hadi wanafikia kukiri hadharani.Hii unatufundisha nini?
 
Yaani mimi nimeshateremsha matarajio mapema kabisa kuondoa "disappointment"

Kwa kweli nilishateremsha matarajio pale tu Kikwete alipotajwa kuwa mgombea wa CCM.

Siku hizi kuharibu ndiyo kawaida, tena hawaoni hata aibu kusema tulikurupuka.Utarajie kukurupuka katika kila kitu.Cha kushangaza si kukurupuka tena, kama kuna kitu kinafanyika vizuri, hicho ndicho kitanishangaza.
 
Ni wapumbavu wote hao waliodhani kujenga shule nyingi kama uyoga kutasaidia kupunguza matatizo ya elimu Tanzania. Nyingi ya shule hizi walimu wake (kama shule ina walimu) ni wale waliopata division 0 O'level. Hawajui lolote ni sawa na kichwa cha mwendawazimu tu.
 
Eti ule ndio ulikuwa utekelezaji wa mkakati wa MGD's (millenium development goals) hahaha kwa kweli tumerudi kulekule kwenye Ualimu Pasipo Elimu(UPE)kwani tunachofanya sasa ni kutaka quantity kuliko quantity, saa nyingine mtu unafikiri hadi unajiuliza hivi siku moja tuwapige mawee nini?Pundit bora wee ulishajikatia tamaa,manaake taifa la wajinga linaloundwa sasa mi nashindwa hata kuelewa unamaliza form four hujui testtube ikoje na anyekufundisha mwenyewe hana uhakika,bado Rais anataka nchi inayokua kisayansi. mmmmh
 
Lakini nasikia by 2015 tutakuwa ontrack with MDG.

Na kwenye afya hiyoooo inakuja, kila kijiji kuwe na dispensary!

kazi ipo!
 
Maeneo mengine kama huko umasaini madarasa yaliyojengwa kwa mbinde na wananchi kulazimishwa kutoa michango hayana hata wanafunzi licha hata ya walimu. Muda si muda tutaanza kuona manyasi yanaota ndani.
 
Kwa hakika hii ni aibu kubwa, inaonesha kukosa umakini katika maamuzi ya serikali. Lakini cha kushangaza ndugu zangu ni kwamba maofisa wanaohusika kuishauri serikali katika masuala haya ya elimu na mengine wana elimu nzuri tu. Tatizo ni kuwa na wataalamu ambao ni watumwa wa wanasiasa, ukimshauri mwanasiasa jambo tofauti na analofikiri yeye ankuona wewe ndio hufai, kwa hiyo anatoa amri toka jukwaani na wewe unalazimishwa kutekeleza. Usipotekeleza anakuondoa kwenye madaraka hayo ama anakunyanyasa na kuku-frustrate. Nimewaona wenzangu wengi tu ambao wako pale wizara ya elimu makao makuu ambao hawakubaliani na mambo mengi ambayo serikali inashinikiza katika suala la maendeleo ya elimu, lakini wanalazimika kuyakubali tu hivyohivyo. Mfano wa wazi ni hizi shule za sekondari ambazo mimi naziita za "msaragambo". Ni aibu tupu, watoto wanakwenda kucheza mchana kutwa wanarudi nyumbani jioni! Wanadanganywa wako sekondari! Dhambi kabisa hii. Bora tu wangekaa nyumbani wakajifunza kuchoma tofali!
 
Nafikiri, wenzetu hawa wako bize kujifikiria wao wenyewe, jinsi watakavyoweza kubaki madarakani, milele na milele, badala ya kuifikiria nchi na wananchi kwa jumla.

Nakumbuka jinsi Rais Mstaafu Mkapa, alivyokuwa anapenda kujisifu nini alichofanya na kuyatolea takwimu, hayo aliyoyafanya. Kuna siku alikuwa akitoa takwimu za shule za msingi zilizojengwa wakati yeye akiwa madarakani kama Rais.

Shule zanyewe hizo ni zile zizokandikwa kwa udongo, kuezekwa kwa nyasi au makuti, hazina milango wala madirisha na sakafu ambazo hazikusakafiwa kwa udongo ulaya. Ndani yake, wanafunzi wamekaa chini mavumbini, hawana vitabu wala kalamu. Mwalimu, hana chaki wala ubao ukutani wa kuandikia na yeye mwenyewe hajalipwa mshahara kwa miezi kadhaa. Isitoshe mwalimu mwenyewe alimalizia darasa la saba na hana taaluma ya kufundisha.

Kukurupuka kwa hiyo, kunasababishwa na hamu ya kutaka kufanya mambo kadhaa kwa haraka na kwa muda mfupi unaowezekana, ili mtu apate kujinadi, wakati muafaka ufikapo, kwa shabaha ya kubaki madarakani kwa sifa zisizomnufaisha mtu mwingine katika jamii.

Unaweza kuamini kuwa baada ya kukiri makosa ya kujenga shule za sekondari, ambazo maendeleo yake hayakupangwa kisayansi, watu hao hao wanazungumzia kujenga dispensari katika kata zote hizo hizo. Ikifika 2010 wasimame majukwaani/ulingoni wadai wamefanya hiki na kile, ili wapate kuchaguliwa tena (kama wanachaguliwa kweli), kuendelea kuwa madarakani.

Uchu wa madaraka ndio unaoleta ukurupukaji huu. Tanzania kila Rais, kuanzia Nyerere mpaka hapa tulipo, anataka kila kitu kifanyike na kikamilike katika uhai wa madaraka yake. Hatuna mpango wa miaka hamsini, licha ule wa miaka mia moja na hamsini au mia mbili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom