Rocky City
JF-Expert Member
- Nov 22, 2017
- 869
- 652
Shukran mkuu.usistuke mkuu, asilimia kubwa ya hizi saloon zetu hazina usalama wa kiafya, mtu akimaliza kunyolewa vifaa havisafishwi ipasavyo akinyolewa mtu ni rahisi kuwaambukiza watakaonyolewa baada yake endapo mashine ilimkwangua wakati wa kutinda (hapa huwa vinyozi wanasogeza viwembe mbele ili watengeneze ile patern ya nywele vizuri, hivo akifanya alignment mbaya ya kiwembe ni rahisi kumchuna mteja na kusababisha damu ambayo inarahisisha kumuambukiza mtu mwingine)
Watu tunatilia maanani unsafe sex tunasahau hili. Ni muhimu elimu itolewe kwa wamiliki wa saloon ili kupunguza/kutokomeza kabisa maambukizi yanayosababishwa na uzembe.
Soma hii article hapa Potential risk of HIV transmission in barbering practice among professional barbers in Ibadan, Nigeria