Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Mkuu, pole sana kwa taarifa hizi za kushtusha,i cant imagine what you are going through,i have been there,nimeshawahi kutumia PEP, niliteseka sana so najua ninachomaanisha,cha muhimu hapi ni kuhakikisha anaanza kuhudhuria ART mapema ili aanze kupatiwa ARV, kupunguza viral load na kupandisha CD4, all in all its very pain full situation. sema kwa wenzake waliobakia,uwe makini,wapatiwe elimu ya vvu na ukimwi, makundi rika wanayocheza nayo pia uwe nayo makini
Pole sana mkuu
Kuwa na imani
 
Nililazwa na binti yangu wa kwanza kwa takribani siku 6 baada kuugua homa (akiharisha na kutapika ) lakini tukaruhusiwa juzi baada ya afya yake kutengemaa(japo amethoofika).

Majibu ya ugonjwa aliokuwa anaumwa yametoka kuwa ni HIV +, tulipatwa na mstuko kwa majibu hayo ilibidi mimi na mke wangu tupime lakini majibu yametoka hatuna maambukizi.

Hatukutosheka na majibu hayo tulienda Consolota na The dream kupima tena wote watatu lakini majibu yale yale sisi wazima ila mtoto ndio Positive.

Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.

Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.

Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?

Niko na huzuni sana ndugu zangu.
duuuuh kiatu kimenibana hiki pole sana mkuuu
 
mmmh nimekos hata la kusema muhimu ni apime DNA kwanza
DNA inaweza kuibua mengi na ndio ikawa mwisho wa familia, nafikiri jambo muhimu ni kumwanzishia mtoto dawa na pia kuwaambia yeye na wadogo zake hali halisi. Kutafuta mchawi kunaweza kuisambaratisha familia fasta.
 
Bonge la dawa habbat soda Mimi kwa sasa hua naenda Hosp kufata vipimo najitibu kwa miti shamba tu!

Watu wanapona ukifata proper dose though some people will argue!
Wakubwa tupeane formula basi ya kutumia hiyo Habbat soda. Kwanza ikoje hiyo soda??
 
Very sad,pole sana ndg kumbuka vyanzo vya maambukizi ya ukimwi siyo ngono peke yake,
Kuna
1.kuongezwa damu yenye maambukizi kwa uzembe wa tabibu
2.ajari zinazotokea kila siku huenda aliwahi kugusana na damu yenye HIV + kwenye sehemu ya jeraha
3.kitu chenye ncha kali kilichotumiwa na mwenye HIV na damu ikabaki nacho
Kwa kifupi sababu zipo nyingi sana ila kwa sababu mmeshagundua ana maambukizi mna jukumu la kuhakikisha hanyanyapaliwi kwa namna yeyote ile,aanze kuhudhuria kiliniki na kupata ushauri kadri iwezekanavyo,hakikisheni haelewi kama lile n ttz,bali ni hali tu ya kawaida katika maisha mkizingatia ushauri wa taalamu ataishi umri mrefu mpk mtasahau kama alishawahi kuambukizwa HIV.
 
Hivi vitu vyenye ncha kali vikitumika Na mtu ambae ni + alafu kikakaa labda hata masaa mawili je mtu ambae sio + akitumia anaweza pata maambukizi?

Napata mashaka sana na hizi vifaa vya masaloon jamani tutapona kweli?
hili swali huwa najiulizaga hata mm kwakwwli mwenye majibu atupatie
 
ARV = Death Trap!
I would therefore strongly recommend the following hereunder:
1) Strictly switch to 'dietary meals' kwa huyo little angel, by maximizing on veges & matunda! Epuka kabsa kumpa junk foods/drinks. Mlo wake uwe ni healthy foods tu.
2) Maji safi & salama is part of the package. Anywe maji ya kutosha kwa siku. Better aianze siku na maji ya uvuguvugu yalokamuliwa limao kiasi, anywe asubuh anapoamka on empty stomach.
3) Apate uji-lishe on daily basis asubuh na usku. Better wekamo kijiko kimoja cha unga wa mlonge. Atumie asali tu (mbichi original) kwenye uji, achana kabsa na sukari za viwandani.
4) Mkingeni na infections mbali mbali, mfano Malaria, typhoid, n.k ili kumuepusha kunywa mavidonge (antibiotics) mara kwa mara.
5) Hakikisha ana furaha muda wote, acheke na kufurah.
Then baada ya miezi mitatu hivi au zaid, kwa kuyazingatia hayo mambo 1 to 5, mpelekeni akapimwe tena hicho kipimo cha h.i.v... YOU WILL BE SURPRISED!
-Kaveli-
nashukur sana.
Sasa mmi nina ndugu yangu nimempa elim amenielewa sasa ila nikwamba ameishaanza kutumia ARVs kwahiyo nifanyeje ili aziache maana madhara yake ni makubwa yatakayo mpata.
ushaur wako tafadhar..
 
pole mkuu, aanze clinic tu.
Miaka 9 kwa sasa ni mkubwa huyo, wanajifunza mengi mitaani, kwa marafiki na shuleni, na njia za kupata ni nyingi sana, ukiachilia mbali ngono pekee.
Kama hauwezi kumpeleleza mpeleke wa wataalamu wa afya washauri, wakae naye kuongea ma kumshauri.
 
Back
Top Bottom