Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Kingine HIV ni mdudu, je walimuona, uliza swali hili kwa hao walimpima, na sio kufanya kukisia maana mpaka sasa hakuna vipimo vya kumuonesha huyo mdudu kama ilivyo typhoid au malaria.
 
Pole sana mkuu ila nina wasi wasi kwenye majibu kama aliwai kufanya mapenzi au lah...
Watoto wa siku hizi wana ingia kwenye ngono mapema sana.....
Huyo ni wazi aliupata kwa ngono.....
Mpeleke aka anzishiwe dawa mapema japo kama alichelewa....

Tulimpima vipimo kama aliwahi kuingiliwa lakini havioneshi hivyo mkuu.
 
Nililazwa na binti yangu wa kwanza kwa takribani siku 6 baada kuugua homa (akiharisha na kutapika ) lakini tukaruhusiwa juzi baada ya afya yake kutengemaa(japo amethoofika).

Majibu ya ugonjwa aliokuwa anaumwa yametoka kuwa ni HIV +, tulipatwa na mstuko kwa majibu hayo ilibidi mimi na mke wangu tupime lakini majibu yametoka hatuna maambukizi.

Hatukutosheka na majibu hayo tulienda Consolota na The dream kupima tena wote watatu lakini majibu yale yale sisi wazima ila mtoto ndio Positive.

Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.

Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.

Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?

Niko na huzuni sana ndugu zangu.
Kwanza nikupe pole lakini pia usiumie Mungu ndiyo mwamzi.
Yawezekana huyo mwanao ulibadilishiwa hospital bila kujua pima na DNA.

But pia angalia na mazingira yanayokuzunguka wewe.
 
Watoto wetu wanapitia mengi sana huko kwenye mashule na wawapo michezoni... nakumbuka siku za nyuma nilimkuta mtoto akichezea Condom tena imetumika walidhani puto maskini anapuliza, nikamnyang'anya...Dah! Pole sana mkuu
Umenikumbusha jambo baya sana, Siku ka binti kangu nilikakuta kanachezea surgical/examination gloves! Nilijisikia vibaya sana tena alikuwa anapuliza kama puto!
 
Nililazwa na binti yangu wa kwanza kwa takribani siku 6 baada kuugua homa (akiharisha na kutapika ) lakini tukaruhusiwa juzi baada ya afya yake kutengemaa(japo amethoofika).

Majibu ya ugonjwa aliokuwa anaumwa yametoka kuwa ni HIV +, tulipatwa na mstuko kwa majibu hayo ilibidi mimi na mke wangu tupime lakini majibu yametoka hatuna maambukizi.

Hatukutosheka na majibu hayo tulienda Consolota na The dream kupima tena wote watatu lakini majibu yale yale sisi wazima ila mtoto ndio Positive.

Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.

Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.

Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?

Niko na huzuni sana ndugu zangu.
Pole sana mkuu.

Jee unajua jinsi virusi vya Ukimwi vinavyosambazwa kutoka mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine?

Hizi ni njia za Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

1. Mama kwa Mtoto pindi Mama anapozaa akiwa ameathirika wakati wa kutenganisha mama na mtoto halafu damu ya mama ikachanganyika na ya mtoto.

2. Kujamiana na aliyeathirika bila kutumia kinga.

3. Wakati wa kuongezewa damu ambayo VVU.

4. Kushirikiana vitu vyenye ncha kali(sindano, kiwembe n.k) na aliyeathirika.

Tafakari mwenyewe jinsi mwanao alivyoathiriwa.
 
Yuko day au boarding? Umewahi kuishi na ndugu zako wa kiume hapo home?
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom