Mwanangu wa miaka 9 amekutwa na Virusi vya UKIMWI, sijui amevitoa wapi?

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
3,894
12,680
Nililazwa na binti yangu wa kwanza kwa takribani siku 6 baada kuugua homa (akiharisha na kutapika ) lakini tukaruhusiwa juzi baada ya afya yake kutengemaa(japo amethoofika).

Majibu ya ugonjwa aliokuwa anaumwa yametoka kuwa ni HIV +, tulipatwa na mstuko kwa majibu hayo ilibidi mimi na mke wangu tupime lakini majibu yametoka hatuna maambukizi.

Hatukutosheka na majibu hayo tulienda Consolota na The dream kupima tena wote watatu lakini majibu yale yale sisi wazima ila mtoto ndio Positive.

Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.

Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.

Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?

Niko na huzuni sana ndugu zangu.
 
Imenitouch sana hii asee! Hadi amefikia hatua ya kuharisha na kutapika viral load itakuwa heavy sana na stage yake itakuwa sio ya kuridhisha.

Muwaishe akapate medication mapema, but habari nzuri zipo kwamba kuna uwezekano mkubwa HIV ndani ya miaka 10 ikapatiwa cure kwani research za Dawa ya kutibu kabisa zimefikia karibu sana kugundua Dawa ya HIV akiwemo Dr Khalil mmarekani huyu amefanikiwa kutibu panya na sokwe kibao kwa tiba yake ya cell editing waliowapandikiza HIV na wote wàlipona kabisa.

Israeli wana Dawa yao inaitwa Gamorah iko katika hatua ya mwisho kabisa kukamilika.

USA tu ndio wanachelewesha maana HIV kwao ni fimbo ya kuchapia mataifa ya ulimwengu wa tatu kwa misaada via USAID.. Sasa ikipatikana tiba tutakuwa na kiburi so he is controlling us kwa kupitia HIV maana soon Dawa ikigunduliwa atapoteza ushawishi wake Duniani.

But its around the corner maana mataifa kibao yanavumbua Dawa na kupata nguvu kijeshi punde Dunia itashindwa kuvumilia na kuzindua tiba kamili.

Relax! We will survive!

Usife moyo mkuu..mwanao probably akapona kabisa kama atasurvive for the next 10 years to come which is possible akipata medication early.

Don't lose hope.

Though, I'm so sorry to hear this? Sometimes the world is cruel and heartless.
 
pole sana....nenda jukwaa la jf doctor "" katafute Uzi unaoitwa "" je unaweza kutembea na mtu aliyeathirika lakini usipate maambukizi.....utapata majibu yote huko """tena nivizuri zaidi kama mods wakiuhamishia huu Uzi wako huko
 
Nililazwa na bint yangu wa kwanza kwa takriban siku 6 baada kuugua homa (akiharisha na kutapika ) lakini tukaruhusiwa juzi baada ya afya yake kutengemaa(japo amethoofika). Majibu ya ugonjwa aliokuwa anaumwa yametoka kuwa ni HIV + , tulipatwa na mstuko kwa majibu hayo ilibidi mimi na mke wangu tupime lakini majibu yametoka hatuna maambukizi. Hatukutosheka na majibu hayo tulienda Consolota na The dream kupima tena wote watatu lakini majibu yale yale sisi Wazima ila mtoto ndio Positive.
Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, Msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.
Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.

Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?

Niko na huzuni sana ndugu zangu.
Pole sana muhimu kila mzazi afahamu rafiki za mtoto wake mtaani na shuleni......majira yamebadilika sana uwazi utawaokoa watoto wetu tukiendelea kujificha kwa mwamvuli wa maadili ya Mtanzania ktk vizazi hivi tunajiumiza
 
Pole sana mkuu ila nina wasi wasi kwenye majibu kama aliwai kufanya mapenzi au lah...
Watoto wa siku hizi wana ingia kwenye ngono mapema sana.....
Huyo ni wazi aliupata kwa ngono.....
Mpeleke aka anzishiwe dawa mapema japo kama alichelewa....
 
Aisee, mbali na njia ya kujamiiana, UKIMWI unapatikana kwa blood contact na damu yenye virus.
Pengine saluni au huko shuleni ama mtaani ktk michezo na watoto wenzake aliumia ndio ikawa chanzo cha kuambukizwa na mwenzie ambaye ni +.

Inasikitisha
 
Nililazwa na binti yangu wa kwanza kwa takribani siku 6 baada kuugua homa (akiharisha na kutapika ) lakini tukaruhusiwa juzi baada ya afya yake kutengemaa(japo amethoofika).

Majibu ya ugonjwa aliokuwa anaumwa yametoka kuwa ni HIV +, tulipatwa na mstuko kwa majibu hayo ilibidi mimi na mke wangu tupime lakini majibu yametoka hatuna maambukizi.

Hatukutosheka na majibu hayo tulienda Consolota na The dream kupima tena wote watatu lakini majibu yale yale sisi wazima ila mtoto ndio Positive.

Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.

Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.

Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?

Niko na huzuni sana ndugu zangu.
Mkuu pitia uzi huu wote
Inawezekana mtu akalala na mwenye UKIMWI tena peku na asipate UKIMWI?
 
Back
Top Bottom