Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 3,896
- 12,686
Nililazwa na binti yangu wa kwanza kwa takribani siku 6 baada kuugua homa (akiharisha na kutapika ) lakini tukaruhusiwa juzi baada ya afya yake kutengemaa(japo amethoofika).
Majibu ya ugonjwa aliokuwa anaumwa yametoka kuwa ni HIV +, tulipatwa na mstuko kwa majibu hayo ilibidi mimi na mke wangu tupime lakini majibu yametoka hatuna maambukizi.
Hatukutosheka na majibu hayo tulienda Consolota na The dream kupima tena wote watatu lakini majibu yale yale sisi wazima ila mtoto ndio Positive.
Tulikaa kujiuliza kavitoa wapi? Ilibidi nisombe nyumba nzima maana nipo mimi, mke wangu, wanangu watatu, msichana wa kazi na bibi yangu nikawapeleka kupima lakini majibu ni yale yale.
Ikabidi tukampime kama aliwahi kubakwa ila alituficha lakini vipimo havioneshi hivyo.
Mpaka dakika hii tunajiuliza amevitoa wapi?
Niko na huzuni sana ndugu zangu.