Mwanangu sijui atafaulu Hesabu!!

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,100
6,022
Baada ya mazoezi mengi na mifano mingi, akakutana nayo hii hesabu jana kwenye pepa ya form 4, dah nikachanganyikiwa sijui kama atafaulu...kweli "Mathematics ni janga la kitaifa"

ztyu79.jpg
 
inawezekana tatizo ni mwalimu na si mwanao. Niligombana na ml mkuu wa shule ya binti yangu wakati fulani baada ya kuona kituko hiki

1x2=02 nilipomuuliza kwa nini ameandika 02 akajibu mwalimu alitufundisha hivyo, kwamba sifuri haina thamani, bila kuwafafanulia kuwa inategemeana na ilipo hiyo sifuri.

nikamuuliza kwa maneno sita mara saba ni ngapi akanijibu arobaini na mbili. lakini swali hilohilo alikuwa amelikosa kwenye mtihani maana aliandika hivi;

6x7=402 akili na tumbo langu vilichafuka sana. Baada ya kuonana na mwl mkuu kuhusu hili mwalimu alikiri makosa na akajirekebisha.

Wazazi tufuatilie watoto hata writing style pia. Kuna waalimu wengine hupenda kuandika kwa mfano 8 kuanzia kushoto kwenda kulia. inapofika mtoto anatakiwa aandike S au 5 inakuwa shughuli pevu.
 
Back
Top Bottom