Mwanangu anapenda sana simu nifanyeje aache tabia hii mbaya na ya ovyo

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
25,558
45,828
Wakuu mwanangu Ana mwaka na nusu Sasa.

Namshukuru Mungu anaendelea vizuri ila shida ni moja.

Anapenda kuchezea simu tu.nimejitahidi kumnyima ila anapiga yowe Dar nzima


Yaani ukifika nyumbani anapokea pochi anaulizia tu simu simu. Usiku halali vizuri anaota tu simu.

Najilaumu hili tatizo nimesababisha Mimi maana nilikuwa namuonesha humo vikatuni.

Nataka mwanangu akue na maadili mema sitaki kumlea kipuuzi.

Nifanyeje mwanangu aachane na mambo ya simu bila kuumia maana analia hadi anatia huruma
 
Dopamine imezidi

Ni kemikali inayotoka ubongoni tunaposex,angalia TV,angalia Facebook,Instagram,etc

Hapo sasa mama kinafuata addiction...

Baada ya addiction ikafika plateau,kinafata kifo!

Scary indeed!

Chapa raia!
 
Pole sana kwa hilo tatizo. Ila nikujuze jambo moja tu kua hilo tatizo ni lako ww mwenyewe kwa kushinda kutwa kuchezea simu hivo na mtoto kukurithi hio tabia kwani watoto wadogo ni rahisi sana kufata mambo wanaoyaona kutoka kwa walezi wao hivo usitafute mchawi hapo ni ww kujirekebisha tu.
Wabillah Taufiq.
 
Pole sana kwa hilo tatizo. Ila nikujuze jambo moja tu kua hilo tatizo ni lako ww mwenyewe kwa kushinda kutwa kuchezea simu hivo na mtoto kukurithi hio tabia kwani watoto wadogo ni rahisi sana kufata mambo wanaoyaona kutoka kwa walezi wao hivo usitafute mchawi hapo ni ww kujirekebisha tu.
Wabillah Taufiq.
Ahaaa mkuu Mimi naondoka home saa kumi na mbili narudi saa tatu usiku.labda dada anaekaa nae home
 
Just take it away.

Muache alie atanyamaza.

I did it with my son. He was starting to become an addict. Simu ikiisha charge basi nyumba nzima haikaliki.

Nikajisemea geraurahiyaaaa nikaifichilia mbali.
Nimefikiria kufanya hivo na nilianza Jana ila hakujalalika ndani mtaa mzima dogo kapiga yowe.nimeumia sana . Ila nitajikaza leo simpi hata alie uchi
 
Nimefikiria kufanya hivo na nilianza Jana ila hakujalalika ndani mtaa mzima dogo kapiga yowe.nimeumia sana . Ila nitajikaza leo simpi hata alie uchi

Jikaze. You are going to spoil that little baby if every time she/he cries you give in to her/ his whims.
 
Wazazi wengi wa siku hizi hawajui kuwa mtoto hajui kipi bora kwake ila anachoangalia ni kufurahishwa na kuridhishwa full stop. Utakuta mtoto anataka chips, bhasi wazazi wanahangaika nazo kisa mtoto kapenda bila ya kujua kuwa sio healthy food kwa mtoto.

Miss huyo mtoto unamdekeza na kashajua unamdekeza. Wewe iweke mbali na umfundishe mipaka yake mapema lakini na wewe usiwe unashinda nayo kila time maana ndio anachokiiga kutoka kwako. Unaweza kuwa mama ukakaa na kucheza nae au kumnunulia vitu vya michezo kwa ajili ya kumueka busy. Simu sio nzuri kiafya na usihuzunike akili yaani jua unafanya maamuzi magumu kwa ajili yake maana yeye hajui kilicho bora kama unavyojua wewe. Be wise and patient miss
 
Wanawake wengi mnaharibu watoto kwa kuwapa simu, mm wanangu huwa hawagusi simu zangu hata nikiacha hapo siku nzima, tena wanaambiana simu ya baba. Ila za mama yao wanacheza magemu, kusikiliza vidio miziki nk na yeye huwa anawaona tu hawakanyi.
 
Mpe kwa ratiba, ni mdogo sana huyo kukushinda. Miaka hiyo ndo mizuri kumfundisha mipaka na kwamba si lazima apate anachotaka. Lazima ajifunze NO na akubaliane nayo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom