Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanangu ana kigugumizi

Discussion in 'JF Doctor' started by Kiresua, Mar 21, 2011.

 1. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Halow Jf Dr,
  jamani madactari na wote wenye fani ya utabibu, nina binti wa miaka 4, alianza kudevelop kigugumizi tangu akiwa na miaka 3 mpaka sasa, kuna wakati kinakuwa juu sana wakat mwingine kinashuka. Sasa ndugu zangu naomba msaada wenu niweze kumnusuru binti yangu na mateso ya kuongea. Lingine pia mimi nina kigugumizi, na nina wadogo zangu 2 pia wanacho, bab pia anacho lkn kwa mbali. Najua kinaweza kuwa cha urithi ila ningependa kujua kama kuna njia ya kumpunguzia bint yangu shida ya kuongea. Nawasilisha kwa msaada wa maoni na ushauri. Asanteni
   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,670
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole sana.
  Wakati ukingojea msaada wa wataalam hapa JF. Jaribu kupitia hii link:

  Have a problem stutter or stammer. The How to stop stuttering stammering centre can help

  Jamaa anaeleza kuwa amewasaidia watu kadhaa kuachana na kigugumizi.
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Pole sana mtoa mada mwanao anakuwa na kigugumizi wakati gani?? mfano mimi nikiwa na hasira huwa kinanitokea yani nashindwa kuongea kabisaa naweza hata kuua mtu akiwa karibu yangu.
  Je mwanao anacho wakati wote au??
   
 4. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,587
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Sorry to bother you, mimi huwa ni mpenzi wa kuangalia TV Emmanuel, jamaa alikuja ana kigugumizi mpaka kuongea kanisani ilikuwa ni shida. Alivyopewa annointing water kikaisha na akaeleza shida yake pale pale na kupona. Huwa kuna aina nyingi upepo mbaya unapita katika njia nyingi.
   
 5. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
 6. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #6
  Mar 22, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Maria Rosa, asante, Mwanangu anacho wakati wote, kuna wakati kinashuka lakn hakiishi, ila anakuwa nacho wakati wote
   
 7. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Caro, nashukuru kwa ushuhuda, nahisi hvyo, wakati tukiendelea na maombi tunaangalia sayansi inasemaje, usijekuta ni kukosa kula karoti tu, naishia kukemea. Al in al, I should not underestimate the power of The Great God of Might!
   
 8. n

  niwaellyester1 Senior Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mie pia ninacho, na mama yangu pia anacho, na mdogo wetu pia anacho, me nadhani ni cha kurithi coz hata ww inaonekana mwanao pia karithi, kwa me nishakizoea, ni cha kawaida cio rahic mtu kunigundua
   
 9. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,564
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Usikute ni agano baya la kipepo walifanya wazazi mababu na mababu, kataa hilo agano huku ukiomba na kusema navunja agano na shetani likome kizazi na kizazi chako kijacho katika jina la YESU
   
 10. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Amen ön high Gaga. Wil definately do it. Thanks
   
 11. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,984
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  aaaaaamen!
   
 12. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uko BONGO au ULAYA ,.?mtafute SPEECH THERAPIST,.huyo ana elimu ya kuwasaidia watu kama hao,.hata mabubu,wenye vithemi,waliozaliwa na midomo ya sungura[cleft palate] na watu waliopatatwa na stroke pia,.kwa bahati mbaya kwa Tazania to the best of my knowladge hayupo,.aliyekuwepo aliondoka,..mdogo wangu aliyepo marekani alihudhuria mafunzo yake na sasa hivi anaongea vizuri
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,823
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Ushauri ninaoweza kukupa ambao utapunguza taratibu kigugumizi cha mtoto wako ni huu:
  1. Wakati anapozungumza na kukwama, asitokee mtu kutaka kumkwamua kwa kumalizia neno aliloanza. Mwacheni ajitahidi mwenyewe hata kama itapita dakika nzima. Kumsaidia/kumkwamua kunamfanya ajihisi vibaya na kisaikolojia hii inamuathiri kwa kuhisi kuwa "hana anachokijuwa). Hapa itawabidi uwaeleze wanafamilia wote na watu wanaomzunguka wasimsahihishe, wasimsaidie, wasimkwamue. Ikiwa yuko nursery zungumza na walimu wake tatizo lake na wao wachangie therapy hii.

  2. Muda wote muonesho upendo, muwache kumkemea hasa akiwa yumo katika juhudi za kutaka kutamka neno. Kisaikolojia nayo hii inamfanya awe moga, aone haya kusema na inapunguza kujiamini kwake.

  3. Anapokwama muda mrefu na baadaye kujikwamua mwenyewe, apongezwe badala ya kukemewa au kupuuzwa.

  4. Kama utakuwa umechunguza, mtu mwenye kigugumizi hupungua au hutoweka kabisa wakati anaimba. Mnunulie/mtafutie nyimbo za kitoto na watu wa familia wawe wanaimba naye mara kwa mara. Hata michezo ya kitoto iliyo na nyimbo ndani yake inasaidia sana.

  5. Njia nyengine ambayo nimeona kwenye filamu ya karibuni inayoitwa Hotuba ya Mfalme "The King's Speach" inayohusu mfalme mwenye kigugumizi ni kusoma kipande cha habari wakati mtu akiwa anasikiliza mziki kwa sauti ya juu kidogo. (Tahadhari isiwe sauti kubwa sana kiasi cha kuumiza masikio). Hii ni kwa sababu mtu mwenye kigugumizi huwa anajisikiliza sauti yake wakati anapozungumza, kwa hiyo akiwa anasikiliza mziki huku anasema huwa hasikii sauti yake na hufanya juhudi ya kushindana mziki ili ajisikie. Njia hii ni nzuri zaidi kwa watu wazima, sijui kama kwa watoto wadogo wasiojua hata kusoma inaweza kufaa.
   
 14. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,227
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Hakina dawa
   
 15. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,823
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Kuna tafauti baina ya dawa na tiba.
  Dawa kwa maana ya vidonge zipo: benzodiazepines, anti-convulsanta, anti-pressants, antipsychotic na antihypetensive (Nimeziona hizi kutoka Wikipedia, lakini mti akiamua kutumia dawa SIKU ZOTE IWE NI KWA USHAURI WA DAKTARI.
  Tiba za kigugumizi ni pamoja na baadhi nilizozieleza ambazo ni pamoja na mazoezi ya kuzungumza, mbinu za kudhibiti kigugumizi, ukaribu, upole na mapenzi.
  Kwa kawaida watoto wote wanaanza kuongea kwa kigugumizi, na kawaida kinaondoka wenyewe mtoto anapofikia miaka 5 ikiwa sio cha kurithi au sababu nyengine. Ukipita muda huu ndipo mzazi unapaswa kuhangaika kutafuta ufumbuzi.
  Cha kufanya si kukata tamaa. Tunaweza kupata mengi kwa kutumia wavuti husika, ushauri na kubadilishana maoni na wazazi wenye matatizo kama haya pamoja na kuwaona wataalamu wa mogonjwa ya sauti (Speach pathologists)
   
 16. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Bawa, thanks, niko bongo, nilipanga kununua dvd za hi therapy. Nasikia huwa ni user friendly. Kasheshe ni kwenye hapa kilugha cha ughaibuni
   
 17. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mamamia, asante mno, what a piece of advice! I should keep reading ur post for my own good. Asante sana
   
 18. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mamamia, again i say thank you! Asante kwa huduma yako
   
 19. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mamamia thx for ur advice, na raia fulani don't just generalize kwa kusema hakina dawa,

  Pia mwanangu alipoanza kuongea alikuwa nacho bahati nzuri watoto wadogo walikuwa wengi mtaani kwetu na walipenda sana kuimba, basi tulishahama ila kiliisha kabisa, sijui ni zile nyimbo ama ni nini?
  Namshukuru Mungu
   
 20. Kiresua

  Kiresua JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2011
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Nsiande, namshukuru Mungu kwa ajili ya upönyaji wa mtoto wako.
   
Loading...