Mwanandoa, yale mambo unayopuuza ati ni ya kitoto ndio mwiba mchomo kwa ndoa yako

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,216
2,000
Wakubwa wanafaidi!

Ni nadra sana kukuta wanandoa wakichat kwa meseji muda mwingi, kwa kile wanachokiita ndoa yenye heshima basi hutumiana jumbe nyeti tu au maelekezo ya majukumu yao.

Wakati huo akiwa na mchepuko atajiunga kifurushi cha meseji 3000 na zitaisha kwa wiki. Hii ni kwa wake kwa waume.

Roho ya kila mmoja wao inatamani kufanya huo wanaouita utoto (kuchat), lakini anaona si busara kuchat na mkewe. Anafurahia zaidi kuchat na mchepuko kwa stori nyingi hizo za kitoto.

Ni nadra kama sio hakuna kabisa kukuta mke na mume wanatazama 'pilau' kwa pamoja.

Wakati huo kila mmoja (wengi wao) hutafuta muda wa kutazama pekee yake au na watu anaodhani wanastahili huo 'utoto'.

Huyu akienda kwa mchepuko anakutana na GBs storage za pilau na anafurahia, ila akirudi nyumbani anazificha sio heshima.

Nilitaka kuandika kitu kuhusu chumvini, najua wanawake wengi kama sio wote wanapenda. Ila nami nimeona sio heshima.

Ndugu zangu, itoshe tu kusema kuwa hivyo vitu unavyojilazimisha kujiepusha mbele ya watu unaodhani unawaheshimu lakini bado unavifanya huko gizani, vivyo hivyo mwenzako naye anatamani vile vile.

Wengi huchepuka ili wakafurahie hayo mambo ya kitoto, kisha hurejea nyumbani kwenye maisha yenye kanuni serious ili kutumiza wajibu.

Hata mandiko yalituasa, bila kujifanya mtoto ni ngumu kuupokea wokovu.

Siku nikiwa mkubwa, nitarudi utoto..!!

Ncha Kali.
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
9,216
2,000
utafanya hayo lakini bado kutakuwa na sababu zingine za mkeo kuchepuka

sababu hazijawahi kwisha na hakuna anayeweza kuzicontrol zote

Sahihi kabisa, kuchepuka ni suala mtambuka... ila kuziba mianya panapowezekena ni muhimu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom