mwananchi..;Wataka nchi kuingizwa Guinness kufaulisha wasiojua kusoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mwananchi..;Wataka nchi kuingizwa Guinness kufaulisha wasiojua kusoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 14, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Monday, 13 August 2012 21:26

  Daniel Mjema, Dodoma
  KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema Tanzania inastahili kuingia katika kitabu cha kumbukumbu cha Maajabu ya Dunia cha The Guinness Book of Records kwa kufaulisha wanafunzi 5,200 wasiojua kusoma wala kuandika.

  Akiwasilisha maoni ya upinzani bungeni, Msemaji mkuu kuhusu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo alisema hiyo ni kashfa kubwa kwa Serikali ya CCM. “Hii ni kashfa kubwa na kama kweli Serikali hii ingekuwa inafuata misingi ya utawala bora na uwajibikaji, basi leo viongozi wakuu wa elimu wangeshaachia ngazi, lakini tumeendelea na utamaduni wa kufanya mambo kwa mazoea,” alisema.

  Kambi hiyo ilidai inashangaa mpaka sasa Waziri na Naibu wake wapo madarakani wakishangilia ushindi wa kuongoza taifa kushika nafasi ya kwanza duniani kwa kufaulisha wanafunzi wasiojua kusoma na
  kuandika.

  “Kambi rasmi ya upinzani inahoji hivi ni mpaka Waziri Mkuu atishiwekupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye, ndiyo Waziri wa Elimu na Naibu wake wajiuzulu?... kwanini wasiwajibike kwa uzembe na makosa ya
  waziwazi?” ilihoji.

  Lyimo alisema tatizo la wanafunzi kuhitimu elimu ya msingi bila kujua kusoma wala kuandika, ni ufisadi wa aina yake katika sekta ya elimu, watendaji hawatimizi wajibu wao ipasavyo na wanajihusisha na vitendo vya rushwa. Vitendo hivyo vya rushwa vinadaiwa kusababisha kuvuja kwa mitihani, hivyo kuwalemaza wanafunzi kifikra kwa kuwaaminisha kwamba kufaulu
  kunawezekana bila bidii katika masomo. Mwaka jana wanafunzi 9,736
  walifutiwa matokeo.

  “Huu ni ushahidi tosha kuwa sekta ya elimu kuna mafisadi wenye uchu wa utajiri wa harakahara kwa gharama yoyote ikiwamo kuiua elimu yetu kwa kuuza mitihani,” alisisitiza Lyimo katika hotuba
  yake hiyo.

  Lyimo aliwaangukia walimu nchini akiwaomba wasaidie kuwaelimisha Watanzania juu ya umuhimu wa kufanya mabadiliko ya uongozi kwa maslahi ya nchi na mustakabali mzima wa maendeleo ya elimu.

  Halikadhalika kambi hiyo imeionya Serikali isifikiri kutokuwapo kwa mgomo halisi (Active Strike) ndiyo imemaliza tatizo la madai ya walimu, kwani kuna migomo baridi inayoendelea kwa baadhi ya walimu.

  “Athari za migomo baridi huwa ni mbaya zaidi ya mgomo halisi kama walimu wataamua kulipiza kisasi kwa kuwafundisha watoto vitu visivyo halisi, basi kuna hatari kubwa ya kupata kizazi kisicho na elimu
  kabisa”alisisitiza Lyimo.

  Kauli hiyo ya kuporomoka kwa elimu nchini, iliungwa mkono pia na Mbunge wa Viti Maalumu, Maulida Komu (Chadema) wakati akichangia
  bajeti hiyo.

  HAPO VIIP,, WHAT IS YOUR TAKE?
   
Loading...