Mwananchi, Nipashe, Guardian, Mtanzania wazima habari ya Wikileaks! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwananchi, Nipashe, Guardian, Mtanzania wazima habari ya Wikileaks!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Dark es Salaam, Sep 6, 2011.

 1. D

  Dark es Salaam Member

  #1
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magazeti "huru" ya kila siku, ikiwemo Mwananchi, Nipashe, Guardian, Mtanzania leo yamepuuzia habari ya Wikileaks kuhusu tuhuma za Rais Kikwete kupewa rushwa na mfanyabiashara wa Dubai anayemiliki hoteli za Kilimanjaro.

  Je, huu ni uzalendo? Self sensorship, kutishwa wasiendike au kujipendekeza kwa Rais kulikofanywa na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari hivi? Tutafakari...


  1. MWANANCHI

  Mhariri Mkuu: Theophil Makunga, Mmiliki: Aga Khan (Nation Media Group)

  2. NIPASHE/GUARDIAN

  Mhariri Mkuu: Jesse Kwayu/Wallace Mauggo, Mmiliki: Reginald Mengi (IPP)

  3. MTANZANIA

  Mhariri Mkuu: Deodatus Balile, Mmiliki: Rostam Aziz (Caspian)

  * Siku ambayo tuhuma za Wikileaks zimeibuka, Rais akatoa hotuba kukemea RUSHWA kwenye sekta ya ujenzi. Sura yake ilionesha kumsuta.
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  umeanza vizuri lakini mstari wa mwisho umetibua hoja nzima..
  sijui kuhusu mwananchi lakini mtanzania na nipashe wamiliki wake wote wana kadi hai za ccm
  kipindi cha dakika 45 cha itv ni kama jukwaa la propaganda la ccm
  subiri kesho mwanahalisi watakavyomchana prezidaa na maushahidi kibao
   
 3. M

  Mojo Senior Member

  #3
  Sep 6, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanajipendekeza tu kwa Kikwete hao. Si sahihi kuminya (suppress) habari hata kama wameombwa wafanye hivyo. Wananchi wanastahili wapate habari waamue wenyewe ukweli uko wapi, si kwa magazeti kuamua kuwaficha. Kwa karne ya leo ya SMS na dot.com huwezi kuficha habari yoyote hata kwa wanakijiji
   
 4. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Guardian wameandika "state house rubbishes Wikileaks allegations" na Mtanzania "ikulu yakanusha taarifa za Wikileaks", na ni ndio majibu yaliyotolewa na Ikulu, sijaelewa ulitaka waandikaje... wapuuze kauli ya ikulu na kushikilia kwamba Wikileaks wamemtuhumu Rais bila kutoa current status au? na ofcourse ukisoma hizo habari ndani lazima ukutane na tuhuma zilizoelekezwa kwa Rais
   
 5. u

  utantambua JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />

  Kweli tuna magazeti "huru" na si magazeti huru. Yote hayo yamejishushia hadhi yao kwa kiwango kikubwa. Yaani hata mwanachi?
   
 6. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,519
  Likes Received: 1,689
  Trophy Points: 280
  hivi kila tunachokitaka wana jf lazima kiandikwe kwenye magazeti? Mimi niwe wazi kwenye hili, wikileaks sio ya kuientertain. Binafsi siishobokei kabisa
   
 7. T

  Testimony Senior Member

  #7
  Sep 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  magazeti yalipaswa kwanza kuandika habari ya weakleaks kisha kufuatilia majibu ya ikulu. kuanza na kutoa majibu kabla ya kutoa kilichojibiwa si uhadishi bora wa habari. inaonesha wazi mmesha-take sides. ni aibu kwa magazeti yetu hususan katika zama hizi ambazo watu wengi wanaweza kupata habari kwa njia nyingi tofauti. kama haikuwa habari yenye uzito, ikulu isingelazimika kuijibu! aibu kwenu wahariri na wamiliki! huu woga sijui utatufikisha wapi. na kama ni kumbeba asiyebebeka, mtazama nae!
   
 8. Gracious

  Gracious JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,750
  Likes Received: 343
  Trophy Points: 180
  Yuu are right mkubwa,Magazeti wameelezea jinsi ikulu ilivyokanusha.Na hiyo ndo role ya vyombo vya habari.
   
 9. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Inatakiwa tupiganie katiba mpya vyombo vya habari havipo huru , freedom is comming
   
 10. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Pale ambapo vyombo vyetu vya habari nchini watakuwa wanakosesha wananchi nafasi ya KUFAHAMU juu ya sakata fulani, Jamii Forum bila shaka itafanya kaziyo hiyo mara moja tena kwa unyenyekevu mkubwa kama ambavyo walivyofanya tangu juzi.

   
 11. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  Opinion yako kuhusu wikileaks naiheshimu.
  However, ninachojua kuhusu huu mtandao ni kuwa haujagi na vitu hivi hivi tu. Inawezekana story isiwe 100% accurate lakini lazima kuna transaction ilikuwa imefanyika inayomhusu JK.....there must (repeat must) be something definitely!
   
 12. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu nakubaliana na wewe kidogo mwishoni mwa mchango wako ila sikubaliani mwanzoni mwake. Kaa ukijua wengine tuna uzoefu mkubwa wa kusome body language ambayo kwa kifupi huchukua miaka mitatu kuielewa vizuri. Nitakupa kipande kimoja tu na ukiwa mfuatiliaji sana wa mambo utagundua ni nani pia aliwahi kurudia somo hili. Ona kaka; mtu unapomuuliza swali huku umemkazia macho na akakujibu huku kaangalia juu kushoto kidogo huku kichwa chake kikinyenyuka kidogo kidogo, juwa huyo anakudanganya kwa sababu anakuwa anafanya kitu tunaita 'rapid creativity kwa kutimia ubongo wa mbele sehemu ya creation ambayo kimsingi iko kushoto. Huyohuyo akikujibu hali amekukazia macho na sauti yake ikaendana na yako na mikono yake ikiwa kwenye original state tangu umuulize swali huyo anasema kweli, na yule pia anayekukazia macho na kutimia miguu ama mikono kuificha slight shaking huyo anakuficha jambo na jua kabisa anasoma reference centre kwenye ubongo wake na anahusisha pia creativity kubadili ukweli. Sasa kwa hayo kidogo tu kaka napenda kuhitimisha kwa kukuambia hili pia, mtu anapotabasamu wakati akieleza suala zito, huyo hana uwezo wa kulisema hilo na mara nyingi huwa analazimisha kukumbuka alichoambiwa kusema sasa kucheka mara nyingi hu refresh reference centre kwa sababu si zaidi ya misuli saba inayokuwa inafanya kazi kichwani hii ni zaidi na kuwa siliazi ambapo mtu hutumia zaidi ya misuli 32 kichwani hii ikikanisha hutumia karibu 50% ya capacity ya cerebllum yaani ubongo wa mbele hasa sehemu ya speech, wisdom, positive imagination (kama ya Martin Luther King Jr), na kadhalika. JK ni kweli akitoa hotuba hiyo alikuwa anafikiria sana kushushuliwa.
  Mheshimiwa napenda kutoa hoja.
   
 13. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Mmoja wa wabaya wa nchi hii katika kusafisha uchafu wa viongozi wetu ni wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari. Tabia yao ya kujipendekeza kwa watawala kwa ajili ya manufaa yao imewanyima uelewa wananchi wengi wa kawaida na kuwafanya wawe hawaelewi kinachoendelea.
  Kupuuza kabisa habari hii ya mteule wa wakati ule kununuliwa suti na kulipiwa "event in guestroom usd 1000", mchango wa usd kadhaa kwa chama chake na mengineyo na wamiliki wa Hotel yenye utata unaoendelea hadi sasa ni ujinga uliokomaa. Tunatafuta uadilifu uko wapi na si vinginevyo. Waziri Mkuu wa Italy Berlusconi anaanikwa yote aliyofanya na afanyayo ili kulinda hadhi ya ofisi kuu na anajitokeza kujibu yeye mwenyewe sio kupitia wasemaji wa ofisi wanaolipwa na walipa kodi. Hatujasikia wahariri wa huko wakifichaficha habari hiyo kwa nini?
  La kusemwa lisemwe ili ukweli uwe wazi na kama ni kweli HESHIMA NA USAFI WA OFISI KUU UZINGATIWE. Hii itatusaidia sana baadae kama taifa kuwa si kila mtu anaweza kuwa Rais, kabla ya kuipigania nafasi hiyo mtu atajipima na kuona anastahili? sio kama sasa kila mtu anakimbilia kuchukua fomu ya kugombe Urais kwa vile Watanzania wanaweza kuongozwa na yeyote yule mradi kampeni na mbinu ziwe za uhakika.
  Hata Salva hakupaswa kutetea jambo hili kwa vile ni la kibinafsi zaidi ndio maana ktk taarifa yake kashindwa kutaja hilo la Event in guestroom kama ilivyoonyeshwa kwenye hiyo cable.
   
 14. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #14
  Sep 6, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mkuu,
  Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100.
  Jambo la pili, Salva anapaswa ajue kuwa yeye si msemaji wa Kikwete bali yeye ni msemaji wa Rais Kikwete. Vitu viwili tofauti. Na ajue halipwi mshahara na Kikwete analipwa Mshahara na watanzania kwa kazi hiyo.Hahusiki na matatizo binafsi ya Rais. Kama anataka kujiingiza aandike kitabu cha maisha ya kikwete kwa muda wake na pesa zake. Si kodi yetu.
   
 15. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Between line.
  Good observation.
  Some issues can go unnoticed unajua ukiweka kujumlaujumla.
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu hutaki habari motomoto? unataka zile zilizochujwa na ccm? Huoni habari za wikileaks zilivyowaumbua hata wabwana wakubwa USA? We ni mtu waaina gani ambaye huwezi kwendana hata na mazingira?
   
 17. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Kamanda huyu Salvatory hana jipya sisi ukweli tunao Rushwa imepelekwa sana Ikulu.Kauli ya Mwl.Nyerere kuwa Ikulu mi Mahali Patakatifu haipo tena.Ikulu imekuwa Mnada wa Tanzania yetu.
   
 18. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,977
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  Mwananchi huwa halilalii chama tawala,labda tayari limeshatulizwa.
   
 19. olele

  olele JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 814
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 80
  Hivi lile la Edward Hosea wa TAKUKURU kuhusu kunyimwa na JK kuwashughulikia ma papa wa rushwa liliishia wapi?? tunakawaida ya kusahau vitu mapema sana.
   
 20. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mwanahalisi iliyokuwa inafanya mambo hayo ilikufa zamani hii iliyobaki ya Mwanamrithi-Malaria Sugu haiwezi kuleta habari za kina, zisizo za umbeya na nongwa kwa anaowahisi kuwa wako juu zaidi yake au wanatofautiana kimtazamo na wanaomsaidia.
   
Loading...