Mwananchi: Mbowe na Lissu sasa ni vita rasmi

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Gazeti la Mwananchi la leo limekuja na habari nzito inayoelezea kuwa sasa hivi Lisu na Mbowe wako kwenye vita rasmi kwani kila mmoja ana amini ya kwake tofauti na msimamo wa Chadema.

Freeman Mbowe ana imani katika kulamba asali na amesikika mara kwa mara akimsifia Rais Samia kuwa pamoja na kwamba ametokana na legacy ya Magufuli lakini ni kiongozi mzuri na yuko tayari kuwaomba Chadema wamtetee 2025 ili aendelee kuwa Rais mpaka mwaka 2030.

Tundu Lisu yeye amesikika akiponda maridhiano yaliyofanywa na Mbowe na Rais Samia akiiyaita ni nusu mkate na ni utapeli mkubwa kwa wana Chadema.

Lisu anatamani Rais Samia aondolewe madarakani kwenye uchaguzi mkuu wa 2025
20230525_073610.jpg
 
Mbowe ni mwanasiasa mzuri mno kama alivyo mfanyabiashara mzuri pia.
Mwisho wa siku mfanyabiashara alie ndani yake ndie hushinda daima.

Kuna ukomo wa kujitoa kwa binadamu hasa pale panapokuwa hakuna shukran. Acha Mbowe ale asali.

Lissu ni mwanasheria na mjenga hoja mzuri mno ila si mzuri katika kusimamia hoja zake na anaendeshwa mno na mihemko.

Pia Lissu ana itikadi ya kuamini yeye ndie yupo sahihi zaidi. Hili linamgharimu kwa sasa kupelekea hata fanbase yake kupuputika.
Amekuwa kama CD iliyochunika, inajirudia hapo hapo bila way forward.

Mwisho wa siku katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Sitostaajabu kesho Lissu akiwa kavaa kijani akikata mauno stejini kumsifia Samia.
 
Lissu ndio mgombea uraisi wa CHADEMA 2025, hivyo huu ni mkakati kuhakikisha Lissu anaendelea kukubalika kwa kuendelea kukosoa serikali huku Mbowe akimjengea Lissu mazingira ya kufanya siasa(wanajua wanachofanya).

Mbowe anaonekana kumkuballi Mama lengo ni kuhakikisha CHADEMA inafanya siasa, huku Lissu ndio anafanya siasa ya kukosoa serikali(akili kubwa).

Mtawajua dhamira yao 2025 wataposimama pamoja jukwaani huku Mbowe akimuombea Lissu kura.
 
Lissu ndio mgombea uraisi wa CHADEMA 2025, hivyo huu ni mkakati kuhakikisha Lissu anaendelea kukubalika kwa kuendelea kukosoa serikali huku Mbowe akimjengea Lissu mazingira ya kufanya siasa(wanajua wanachofanya).

Mbowe anaonekana kumkabali Mama lengo ni kuhakikisha CHADEMA inafanya siasa, huku Lissu ndio anafanya siasa ya kukosoa serikali(akili kubwa).

Alafu Mbowe atamuombea kura Lisu huku akimsifia Rais Samia?
 
Lissu ndio mgombea uraisi wa CHADEMA 2025, hivyo huu ni mkakati kuhakikisha Lissu anaendelea kukubalika kwa kuendelea kukosoa serikali huku Mbowe akimjengea Lissu mazingira ya kufanya siasa(wanajua wanachofanya).

Mbowe anaonekana kumkabali Mama lengo ni kuhakikisha CHADEMA inafanya siasa, huku Lissu ndio anafanya siasa ya kukosoa serikali(akili kubwa).

Mtawajua dhamira yao 2025 wataposimama pamoja jukwaani huku Mbowe akimuombea Lissu kura.
Kadri mnavyozidi kulificha hili suala kwa kulipa majina tofauti, kama akili kubwa na mengine, ndivyo linavyozidi kuibuliwa kwenye vyanzo tofauti vya habari na kuzidi kukuzwa, niwashauri tu msifiche maradhi kifo kitawaumbua. Chadema wakae chini wamalize hii vurugu, na wala sio "akili kubwa" kama mnavyoita.

Hiki ulichoandika hapa naweza kukiita ni side A, lakini pia hapa tukubaliane ipo pia side B, hao jamaa kuonekana kupingana hadharani sasa hivi mpaka kufikia hatua mmoja kuyapinga maridhiano, na kuwapinga wenzake walioanza kuutolea macho ubunge, mpaka kufikia hatua ya kuuliza kama wapo sawa vichwani!, kwangu sioni kabisa kama huo ni mpango wao kuelekea 2025, au ndio "akili kubwa" kama mnavyotaka kutuaminisha.

Kwangu nachokiona hapo, ni mmoja kuamua kutema nyongo tena baada ya kukaa nayo ndani kwa muda mrefu, kwasababu madai/shutuma anazotoa anaonekana moja kwa moja kuwalenga wenzake chamani, wala sio kumlenga Samia kuelekea 2025 kama unavyotaka kutuaminisha kwa kivuli chenu cha "akili kubwa".
 
Iko wazi kwamba Lissu anapigania maslahi mapana ya nchi, Mbowe anapigania maslahi yake binafsi.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kukubaliana na majadiliano ama maridhiano aliyoingia Mbowe ama anayoyapigia kelele Mbowe. Mbowe ni fisadi aliejificha chama cha upinzani lakini ukweli haujifichi kwamba ni mtu mwenye very very corrupt mind

Huhitaji kua na elimu ya darasa la 4 kung'amua hilo.
 
Mbowe ni mwanasiasa mzuri mno kama alivyo mfanyabiashara mzuri pia.
Mwisho wa siku mfanyabiashara alie ndani yake ndie hushinda.
Kuna ukomo wa kujitoa kwa binadamu hasa pale panapokuwa hakuna shukran. Acha Mbowe ale asali.

Lissu ni mwanasheria na mjenga hoja mzuri mno ila si mzuri katika kusimamia hoja zake na anaendeshwa mno na mihemko.

Pia Lissu ana itikadi ya kuamini yeye ndie yupo sahihi zaidi. Hili linamgharimu kwa sasa kupelekea hata fanbase yake kupuputika.
Amekuwa kama CD iliyochunika, inajirudia hapo hapo bila way forward.

Mwisho wa siku katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu. Sitostaajabu kesho Lissu akiwa kavaa kijani akikata mauno stejini kumsifia Samia.
Falsafa ya siasa za upinzani hazina mizizi ya kutosha katika jamii za kiafrika. Toka enzi na enzi uchifu ulitamalaki, kabla ya ukoloni na hata baada ya ukoloni. Kulazimishiwa kitu ambacho siyo historia yako na wala hakipo kwenye DNA yenu ya maongozi mtajikuta mnalalamika mwanzo mwisho. Sioni nchi yoyote ya kiafrika ambayo siasa za upinzani yaani demokrasia ya vyama vingi vya siasa vinavyoshindana kuchukua uongozi wa nchi umesaidia nchi kupiga hatua za kimaendeleo. At best ushindani umesababisha nchi kutumia pesa kubwa sana za walipa kodi kuendesha siasa, at worst ushindani umesababisha coup detats kibao kama Sudan, Mali, Ivory Coast na malalamiko yasiyo na suluhu.
 
Lissu ni mtu amekua tayari kumwaga damu yake kwa maslahi ya chama na nchi. Mbowe hawezi. Walifunga akaunti yake moja tu akakubali kuingia kwenye maridhiano ya kizezeta ili tu arudishiwe pesa zake.

Hakuna kiongozi yeyote kutoka kanda ile anaeza kua na uchungu na maslahi ya nchi bila kujali anatoka chama gani, hakuna.
 
Falsafa ya siasa za upinzani hazina mizizi ya kutosha katika jamii za kiafrika. Toka enzi na enzi uchifu ulitamalaki, kabla ya ukoloni na hata baada ya ukoloni. Kulazimishiwa kitu ambacho siyo historia yako na wala hakipo kwenye DNA yenu ya maongozi mtajikuta mnalalamika mwanzo mwisho. Sioni nchi yoyote ya kiafrika ambayo siasa za upinzani yaani demokrasia ya vyama vingi vya siasa vinavyoshindana kuchukua uongozi wa nchi umesaidia nchi kupiga hatua za kimaendeleo. At best ushindani umesababisha nchi kutumia pesa kubwa sana za walipa kodi kuendesha siasa, at worst ushindani umesababisha coup detats kibao kama Sudan, Mali, Ivory Coast na malalamiko yasiyo na suluhu.
Una akili sana
 
Gazeti la Mwananchi la leo limekuja na habari nzito inayoelezea kuwa sasa hivi Lisu na Mbowe wako kwenye vita rasmi kwani kila mmoja ana amini ya kwake tofauti na msimamo wa Chadema.

Freeman Mbowe ana imani katika kulamba asali na amesikika mara kwa mara akimsifia Rais Samia kuwa pamoja na kwamba ametokana na legacy ya Magufuli lakini ni kiongozi mzuri na yuko tayari kuwaomba Chadema wamtetee 2025 ili aendelee kuwa Rais mpaka mwaka 2030.

Tundu Lisu yeye amesikika akiponda maridhiano yaliyofanywa na Mbowe na Rais Samia akiiyaita ni nusu mkate na ni utapeli mkubwa kwa wana Chadema.

Lisu anatamani Rais Samia aondolewe madarakani kwenye uchaguzi mkuu wa 2025 View attachment 2633991
Mnahangaika sana
 
Wenye akili timamu tayari tumeshaonganisha dot toka mwanzo.

Katika hili Sagala mimi niko upande wa Mbowe ambae anasimama na taifa kwanza (ndio maana chama kina msapoti.

Huku Lisu akiwa anasimama na mabeberu (belgium) kina Amsterdam nk (ndio maana chama kimempuuza na kumtelekeza)

Inashangaza wapasha habari wa chama mashuhuri wameshindwa kuliweka hili wazi, ili watu wenye akili walitafutie ufumbuzi.

Erythrocyte where are you mkuu??
 
Attachments

  • IMG-20230520-WA0008.jpg
    IMG-20230520-WA0008.jpg
    110.2 KB · Views: 3
  • images (12).jpeg
    images (12).jpeg
    11.5 KB · Views: 3
  • images (10).jpeg
    images (10).jpeg
    12.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom