Elections 2010 Mwananchi: Masha, Mramba, Batilda, Mkuchika hoi!

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,445
2,268
TBC1 imenukuu gazeti la Mwananchi likitangaza kifo cha ubunge wa mawaziri MASHA, MRAMBA, BATILDA, MKUCHIKA

Kaa chonjo
 
He he he sijui sasa watalifanyaje Mwananchi si walitishia kulifuta naona habari hizo zitakuwa shubiri kwa watu.
 
He he he sijui sasa watalifanyaje Mwananchi si walitishia kulifuta naona habari hizo zitakuwa shubiri kwa watu.
huyo Mkuchika ndo huyo yuko chali, na hakuna wa kuendeleza policies zake pale Utamaduni, Bendera alishakuwa dead on arrival hata kabla hajamaliza term yake. Mkwere aliwaambia anaetaka basi kuna job vacancies za Ukuu wa Wilaya...AIBU!
 
Masha, Batilda, Mramba, Mkuchika maji ya shingo Send to a friend Monday, 01 November 2010 00:49 0diggsdigg

batildaburian.jpg
Batilda Burian akiwa katika kampeni

Waandishi Wetu
MWENENDO wa matokeo ya awali yaliyokuwa yakikusanywa hadi jana usiku yameonyesha kuwa vigogo takribani wagombea 10 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wana hali ngumu.Taarifa zilizokusanywa na Mwananchi katika majimbo mbalimbali zinaonyesha kuwa Philip Marmo (Mbulu), Lawrance Masha (Nyamagana), Dk Batilda Buriani (Arusha Mjini), Kapteni George Mkuchika (Newala) na Basil Mramba(Rombo)hali zao ni ngumu katika uchaguzi huu.

Matokeo yalikusanywa katika kata za majimbo ya wagombea hao yanaonyesha kwamba kuna mchuano mkali sana baina yao na wale wa vyama vingine na baadhi yao wamezidiwa hadi zaidi ya nusu ya kura, huku kata zilizobaki katika majimbo hayo zikiwa ni za kunyang'anyana.

Washindani wakubwa wa wagombea hao wanatoka Chadema na CUF ambavyo vimeweza kuongeza ushawishi katika maeneo mbalimbali nchini, kubwa ikiwa ahadi yao ya kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita.

Hadi jana jioni mvutano ulikuwa mkali katika majimbo hayo huku askari wa jeshi na wale wa polisi wakijaribu kutuliza hali ya mvutano uliokuwa umeanza kujikita kwenye majimbo hayo.

Taarifa zaidi zilieleza ukiukwaji wa taratibu wakati wa kura za maoni, tuhuma za rushwa na wanachama kupinga maamuzi ya baadhi ya kamati za siasa za mikoa kugeuza matokeo, ni mambo ambayo yanaendelea kuisumbua CCM.

Matokeo mengine ya awali ya urais, ubunge na udiwani yalionyesha jimbo la Simanjiro Kata ya Ngorika kura za urais CCM imepata kura 853, Chadema 282, CUF 5, APPT, 3 na NCCR 1. Udiwani katika Kata hiyo CCM imepata kura 941 na Chadema 200.

Katika Kata ya Kibaya jimbo la Kiteto, kura za urais CCM imepata 83, Chadema 102 na CUF kura 4. Katika ubunge Chadema imepata kura 132, CCM 60 na CUF 2. Kwa upande wa udiwani Chadema imepata kura 125 na CCM 67.

Katika Kata ya Sanya Juu jimbo la Siha CCM imepata 1,269 na Chadema 949.

Kata ya Ngamiani Kusini, urais APPT 3, CCM 1,145, Chadema 104, CUF 1,254 na NCCR 4 udiwani CCM 11,180, Chadema 52, CUF 1,479 na UDP 5. Ubunge jimbo la Lupa, CCM 1,039, TLP 589, Chadema 37 na CUF 5
 
Musoma == Chadema hii ni kwa mujibu wa ITV...Nyerere kapata zaidi ya 56%
 
mama mbenga jimbo la iringa mjini kachiinjiwa kwenye mto ruaha
chadema roho kwatu .
 
Kwa Masha was obvious!!! Maana alikuwa hana amani Mwanza!! Ilifikia hatua akawa hafanyi kampeni tena. Kila anakopita anazomewa hadi basi...

Wananchi wameamu... Marmo...... nimefurahi sana, maana huyu mzee alikuwa anaona uongozi ni haki yake...:doh:
 
TBC1 imenukuu gazeti la Mwananchi likitangaza kifo cha ubunge wa mawaziri MASHA, MRAMBA, BATILDA, MKUCHIKA

Kaa chonjo

Mungu yule yule aliyemwambia Musa "inua kijiti juu" na moto ukakiteteza kule jangwani
Ndo huyu huyu anatenda miujiza leo. Utawala wa udini; watoto, urafiki; ufisadi, uzinzi, kuabudu majini nk unathani unadumu??
Hapo ni mwanzo tu. bado. Mungu si kwamba haoni mpaka aachie taifa zima lenye wateule wake liangamie.
Onyesha ukuu wako.
In allah we believe and belong
 
Huyo Batilda si alishafanyiwa sendoff part? Kilichobaki ni msimamizi wa uchaguzi kumkabidhi kwa mshenga afungishwe ndoa ya mkeka (viti vya dezo vya rais)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom