Huenda Tanzania ikazuwiwa kupeleka Mahujaji Soudi Arabia kuhiji kutokana na deni linalodaiwa la Dola 69300 sawa na shilingi 155,232,000 za Tanzania za mwaka jana. fedha hizo ni malipo ya Mhema, Chakula na Nyumba. Kwa upande wa Zanzibar taasisi zote hukamilisha malipo yao mapema lakini upande wa Tanzania Bara ndio wenye matatizo hayo. miongoni mwa Taasisi zinazodaiwa kutomaliza deni ni nane ambapo mbili zimeanza kulipa kidogo kidogo na tano zilizobaki hazijamaliza nazo ni (1) Baraza kuu la waislamu (BAKWATA) (2) Tanzania Muslim Hajj Trust (3) (4) Zamzam Center,
4.Jamarat Hajj (5) Al Husna Hajj Taibah.
Sheikh Khamis Yussuf ni mmoja wa taasisi za kusafirisha Mahujaji aliye katika umoja wa taasisi hizo anasema wamesikitishwa sana na kitendo cha Tanzania kutaka kuzuwiwa kwenda Hijja kutokana na deni ambalo lilipaswa kulipwa muda mrefu.
Hata hivyo amesema wao hawapo tayari kuona kadhia hiyo inaendelea hadi kufikia kuzuwiwa kwenda Hijja.
Naye Katibu Mtendaji wa Wakfu na Mali ya amana Sheikh Abdallah Talib amekiri kuwepo kwa jambo hilo na amesema taratibu za kidiplomasia zinaendelea.
Febuari 25 kwa mujibu wa hiyo barua iliyoandikwa kwa kiarabu ndio siku ya mwisho wa kupokea malipo iwapo Tanzania itashindwa kuwasilisha fedha zinazodaiwa watanzania hawataruhusiwa kwenda Hijja mara hii ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuzuwiwa.