Mwananchi kulipishwa garama ya nguzo ni uonevu-muhongo

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,597
1,005
Waziri wa nishati na madini profesa Sospiter muhongo amesema Kitendo cha tanesko kuwalipisha wananchi garama za nguzo ni uonevu.
Profesa amesema
garama za nguzo zinapaswa kubebwa na tanesko,

mimi kama raia nimefurahishwa sana na muhongo kama watatekeleza mpango huo, kwa kweli watu wengi wa vijijini wanakosa nishati ya umeme kutokana na sharti la kulipia nguzo ambayo ni tsh milioni moja,
Tunaitaka serikali kubeba suala la nguzo wananchi hawawezi kulipia nguzo.

Nampongeza sana mh waziri kama ulivyotangaza bungeni kwamba januari utaratibu wa kutolipia nguzo utaanza rasmi.

Sisi walala hoi wa huku vijijini tunakutakia maisha marefu, kama utatusaidia.

Source,ITV HABARI
 
Tatizo la viongozi wetu wanalalamika tuu bila kuchukua hatua.
apige marufuku basi ili wananchi wasiwe wanalipishwa.
Kulalama tu haitoshi.
 
Ni lazima kuwepo na utaratibu unaoeleweka. Isije ikawa kuunganisha umeme inachukua miaka 3 kwa kisingizio cha kukosa nguzo!
 
Inapaswa mtu akilipia umeme hata kama anatumia nguzo ni miezi 2 tu!
 
wizi ni pale, unapotakiwa kulipia nguzo halafu wanasema nguzo ni mali ya tanesco ilhali umeilipia.
Kama nguzo inamilikiwa na mimi niliyeilipia ni sawa, lakini kama nikilipia kitu nisicho miliki TRA, TAKUKURU mko wapi?
 
Mimi ni mmoja wa wahanga wa kulipa nguzo za umeme.

Nilijiuliza sana hili swali na kuwauliza Tanasco wakasema ndio utaratibu wao.
 
Angepiga marufuku kulipia nguzo kuanzia leo hakuna haja ya kumwacha mwizi TANESCO aendelee kuiba huku umemkamata.
 
Tatizo lingine hapa lipo katika idara ya ardhi katika kupima viwanja ambapo inapelekea watu kujenga katika maeneo yasiyopimwa ambapo ili uletewe nguzo zikufikie unahitaji nguzo kadhaa, kama viwanja vingi vingekuwa vimepimwa inakuwa rahisi kusambaza kwa kuwa ni jukumu lao kupeleka nguzo huko kulingana na ramani za eneo husika.

Hofu yangu ni kwamba hili tatizo litakuwepo tu kwa kisingizio cha mjikusanye muwe watu wengi ndi tuje tuwaunganishie umeme especially kwenye maeneo ambayo huduma haijafika kwa kiwango kikubwa
 
Back
Top Bottom