Mwananchi: Hamza alikuwa na msongo wa mawazo kwa kupoteza milioni 400

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
751
1,000
Naona gazeti la Mwananchi wanasema Hamza alipata msongo wa mawazo baada ya kuwekeza milioni 400 Mbeya na kutofika malengo aliyokusudia, jana pia imesambaa video ikionyesha Hamza lengo lilikuwa ugaidi.

Polisi wangejitokeza basi kutupa muelekeo wa tukio, naamini sababu ya Hamza kufanya alichofanya wameshajua.

Pia watu wa media mmeshindwa kabisa kupata watu waliokuwa ndani ya ile daladala na kuwahoji alichozungumza Hamza? Mambo yashakuwa tafrani.

Hamza.PNG
 

Rwehumbizadarlin

JF-Expert Member
Dec 5, 2015
283
1,000
Naona gazeti la Mwananchi wanasema Hamza alipata msongo wa mawazo baada ya kuwekeza milioni 400 Mbeya na kutofika malengo aliyokusudia, jana pia imesambaa video ikionyesha Hamza lengo lilikuwa ugaidi.

Polisi wangejitokeza basi kutupa muelekeo wa tukio, naamini hizo ABC wameshapata.

View attachment 1912045
walimbebea hela zake bana, wewe uwe na msongo huko uje uue askari bila chochote ...haiwezekani kuna jambo hapa
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
8,329
2,000
Milioni 400 ndio chanzo halafu hasira zake akawaelekezea polisi?

Inahitajika Tume Huru iundwe kuchunguza hili tukio, vyombo vya habari na wengine wote wanaogopa kutumia akili zao vizuri kwa hofu ya kufungiwa, tumebaki na speculation za mitandaoni pekee.

Waandishi wa habari za kiuchunguzi wanaoheshimika na walio na uhuru wakufanya kazi zao pia wangesaidia kupata majibu, tatizo ndio hofu ya kufungiwa vyombo vyao imewakumba.
 

MAMESHO

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
1,170
2,000
Madaktari wa akili watatujuza jinsi kutofikia malengo kunavyoweza kuua wengine.

Inawezekana lakini? Ndio maana Manka aliona haolewi akaamua kumchoma jamaa.

Mmh, haya, kuna mdada nampenda humu jf nioombeeni nifikie malengo mkiskia Paaaaa mjue malengo hayakufikiwa.

Kuna mdau pia alinipa hesabu za kilimo cha watermelon nishaweka mzigo mrefu sasa nangojea matokeo yake. Hahahhaha

Nawaombea wote humu mfikie malengo yenu kiwe na amani na utulivu.
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,718
2,000
Naona gazeti la Mwananchi wanasema Hamza alipata msongo wa mawazo baada ya kuwekeza milioni 400 Mbeya na kutofika malengo aliyokusudia, jana pia imesambaa video ikionyesha Hamza lengo lilikuwa ugaidi.

Polisi wangejitokeza basi kutupa muelekeo wa tukio, naamini hizo ABC wameshapata.

View attachment 1912045
Unapoteza hela Mbeya kisha unakuja Dar kuua askari wakati Mbeya askari wapo! Askari wa Dar wanahusika nini na matukio ya Mbeya? Hamza kuwa msomali si kigezo cha kutaka kutuaminisha kuwa alikuwa na malengo ya ugaidi, kitendo cha polisi kuikamata familia yake kilikuwa ni cha kibaguzi kikabila na kidini.
 

Kijana wa jana

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
11,837
2,000
Na ile sauti kwenye video ambapo alisikika Hamza akimtuhumu afande siro nayo vipi?

Kwanini awaue polisi tu? Tukumbuke mwenye msongo wa mawazo akiamua kufanya hivyo hachagui wa kumuua.

Pia angekuwa na msongo wa mawazo angeanzia nyumbani asingepanda usafiri akafanye tukio sehemu maalumu kama ile
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,026
2,000
Milioni 400 ndio chanzo halafu hasira zake akawaelekezea polisi?

Inahitajika Tume Huru iundwe kuchunguza hili tukio, vyombo vya habari na wengine wote wanaogopa kutumia akili zao vizuri kwa hofu ya kufungiwa, tumebaki na speculation za mitandaoni pekee...
Nikisikiliza ile clip ya sauti ya Hamza sion dhuruma wala Madini na ushenzi tu aliojiamulia kuufanya
 

Hammaz

JF-Expert Member
May 16, 2018
3,698
2,000
Bwana mkubwa, mjadala usihamishwe!

Hamza aliporwa madini yake na waliyopewa dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zake. Ndiyo akachukua hayo maamuzi ya ajabu kwa hao jezi khaki.

Alichokifanya si kizuri ila hakiondoi uhalali walichokifanya jezi khaki ndiyo chanzo. Wasitanue magoli.

Hili lilishawahi kutokea hata kipindi cha Zombe yule askari na wenzake. Waliwaua wafanyabiashara ya madini wa Mahenge kwa kuwapora madini yao na kuwapachika jina walikuwa majambazi.

Askari bado wana utovu wa nidhamu mkubwa sana! Video tofauti mwaka jana kilichotokea Znz baada ya kuwagonga kwa term waliyotumia wao "wahalifu" ajabu wakawa wanawawasachi kwenye mifuko yao na kuchukua fedha zao.

Wengine wanafungua waleti za wahalifu na kuchukua chenye thamani kilichomo humo! Walibeba mpaka nyama za vingunguti na kwenda kugawana vituoni na raia wakishuhudia baada ya mamlaka kudai hizo nyama si salama mamlaka ambayo ilipishana na wauzaji/wachinjaji wa nyama hapo!

Hayo yote waliyakataa ijapokuwa ushahidi ulikuwa wazi mithili ya mwezi mpevu. Na wakuu wao wanatetea huu uhalifu wao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom