Mwananchi: Dhahabu ya bei mbaya yaibwa, vigogo matatani

Samahani wakuu hapa watakaonielewa ni watu wa hii fani:
Enzi za JPM hadi mchimbaji mdogo alikuwa na uwezo wa kwenda kuchenjua dhahabu yake mwenyewe kwenye "plant" na kuuza mwenyewe sokoni. Maskini leo hii ninapoandika hapa kila mchimbaji anayejaribu kupeleka "rudio" lake plant anaambulia kupigwa, wamekata tamaa mitaji imekata kwa muda mfupi tangu Mzee afariki. Wachimbaji tunajiuliza JPM aliwezaje kuleta neema kwetu na sasa neema hiyo inatoweka ghafla? Ngoja tuone hadi mwisho wa sinema hizi nini kitatokea. Sitaki kuzungumzia magendo ya madini yetu maana nami nimeshawishika kuingia humo, hakuna anayejali!
 
Sasa huko plants wanapigwa na nani?
 
Kuibiwa ni hali ya mtu kuchukua Mali ya mwingine bila idhini yake lakini kuibwa ni mtu moja kumchukua mwingine kwa nia ya kumteka.
Kutoweka ni hali ya kitu au mtu kutokuonekana bila taarifa yoyote.
Huwa tunafanya makosa makubwa kwa kusema kwa mfano dhahabu imeibiwa; ukisema imeibiwa una maana dhahabu ilikuwa na kitu ambacho kimeibwa! Usahihi ni kusema dhahabu imeibwa. Mtu akiwa na dhahabu na ikachukuliwa bila ridhaa yake na bila kufahamu akagundua baadaye kwa dhahabu yake haipo basi tutasema mtu ameibiwa dhahabu na siyo dhahabu imeibiwa!
 
Back
Top Bottom