benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Moja katika habari kubwa kwenye medani ya siasa za Kimataifa inayomhusisha Mtanzania ni habari ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson kuteuliwa kuwania Urais wa Umoja wa Mabunge ya Dunia (IPU) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2023.
Taarifa za kuteuliwa zilitangazwa Mei 11, 2023 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax baada ya kikao na mabalozi wa nchi mbalimbali kuhusu Tanzania kuwania nafasi hiyo.
Kama inavyofahamika kwa kuwania nafasi kubwa kama hii ni lazima apate baraka za Mheshimiwa Rais wa nchi na bila shaka kama ambavyo Rais Samia aliridhia Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Liberata Mulamula kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ni wazi pia aliridhia ("endorsement") Spika Tulia kugombea nafasi ya hiyo ya Urais wa Mabunge ya Dunia (IPU).
Serikali imesimama na Dkt Tulia na kwa kupitia Wizara wa Mambo ya Nje, Waziri Dkt Tax amekutana na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini ili kuomba kuunga mkono jitihada za Dkt Tulia ambaye sasa anawakilisha Tanzania. Vyombo vya habari vimeandika habari hii yenye maslahi mapana kwa Taifa lakini Mwananchi Communications Ltd kupitia gazeti la The Citizen (nadhani wameandika kwa lugha ya Kiingereza kwa makusudi kabisa) wameamua kupingana na juhudi zote hizi na kupingana na maslahi ya Taifa.
Tunafahamu maamuzi ya juu kabisa ya Gazeti hili yanatoka makao makuu yaliyoko nchi jirani ambayo ni mpinzani mkubwa na mshindani wa nchi yetu katika kila suala hivyo pengine hiyo ndio sababu ya kuandika makala yenye kichwa "WHY I THINK TULIA IS UNSUITABLE TO LEAD IPU". Yaani The Citizen wanaamua kwa makusudi kuchafua taswira ya Mtanzania anayewania nafasi kimataifa tena wakichapisha katika lugha ambayo ni rahisi kueleweka na wapinzania wa DKt Tulia, HII SIO SAWA NA NI JAMBO LA KUKEMEWA NA WOTE WANAOWEKA MASLAHI YA TAIFA MBELE
Tunapaswa kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari lakini pia tunapaswa kusema na kukemea pale ambapo vyombo hivi vinashindwa kusimamia maslahi ya nchi na pengine vinatumika kubeba agenda za nchi nyingine bila kujua au kwa kujua.
Lakini hapa ndipo tulipo The Citizen wamewaomba wajumbe kutomuunga mkono Dkt Tulia na wameshauri wajumbe wamuunge mkono Spika wa Bunge la Afrika Kusini.