Mwanamziki wa Marekani Shaggy, awa chifu wa Wasukuma?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamziki wa Marekani Shaggy, awa chifu wa Wasukuma?.

Discussion in 'Entertainment' started by Ng'wamapalala, Aug 27, 2012.

 1. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145
  Shaggy chifu wa Wasukuma!!!, ama kweli Wasukuma tumeishiwa.
  Jamii yetu imejengwa katika matabaka mbalimbali ambayo nguzo zake kuu ni mila na desturi. Tatizo kubwa ambalo linaikabili jamii yetu kwa sasa ni uhaba wa watu wenye fikra na hekima katika kupambanua mambo mbalimbali yanayo athiri na yatakayoendelea kuiadhiri jamii yetu katika kizazi kijacho.
  Inanishangaza na kunisikitika sana ninapoona wazee wetu tunaowategemea kuzilinda na kuziendeleza hizi nguzo zetu kuu katika jamii wanapoanza kuzibomoa hasa pale pesa inapokuwa ndio mzizi wa utoaji wa maamuzi. Pomoja na kwamba Mwalimu Nyerere aliamua kufutilia mbali uongozi wa machifu katika jamii ya kitanzania.
  Nikiwa mmoja wa wajukuu wa aliyekuwa Chifu wa Itilima, inaniumiza sana ninapoona kuna watu kwa sasa wanajifanya ndio vinara katika maamuzi ya mila na desturi kwenye jamii yetu. waswahili wanasema, ashakumu si matusi na nisamehewe kama nimekosea, Jamani, ni lini na wapi Mark Bomani amepewa haya madaraka ya kutuamualia maswala mazito kama haya. Kwanza, yuko pale kwa ajiri ya masilahi yake kama mmoja wa wajumbe wa bodi ya serengeti breweries. Huyu Shaggy, Ninaamini kwanza hajui chochote juu ya historia, mila na desturi ya wasukuma. kama serengeti breweries na bodi yao ambayo Mark Bomani ni mjumbe wanataka wajulikane katika bidhaa zao(market exposure), inanisikitisha sana kuona wanafanya hivi kwa kupitia kwa wazee wetu ambao hata hawajui nini maana ya 'market economy' katika dunia ya sasa iliyojaa ulaghai katika masoko ya bidhaa. Ama kweli, elimu bila fikira na hekima ni kazi bure.
   
Loading...