Mwanamuziki Rihanna aingia orodha ya matajiri wa Uingereza

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
1589381747600.png

Mwanamuziki Robyn Rihanna Fenty (32) maarufu Rihanna kwa mara ya kwanza ameingia kwenye orodha ya Wanamuziki tajiri wanaoishi Uingereza na kushika nafasi ya 3. Amehamia London mwaka 2019

Rihanna ambaye pia ndiye Mwanamke wa kwanza kwa utajiri kwenye orodha hiyo ana utajiri wa takriban Tsh. Trilioni 1.325 (Paundi Milioni 468). Katika orodha hiyo amewapita pia wanamuziki kama Sir Elton John na Mick Jagger

Utajiri wake umekua kutokana na kufanikiwa kwa biashara yake ya vipodozi vya Fenty Beuty na kuingia ubia katika biashara nyingine kama 'Lingerie line' inayohusika na nguo za ndani na uuzwaji wa albamu zake 8 za muziki

Katika orodha hiyo, nafasi ya kwanza inashikiliwa na Sir Paul McCartney pamoja na Andrew Lloyd Webber ambao wote wana utajiri wa Paundi Milioni 800. Nafasi ya nne yupo Sir Elton John (£360m) na nafasi ya tano yupo Mick Jagger (£285m)
 
Huyo dada mi nampenda!
Sijui nimwambie vipi ili ajue kuwa nampenda..
Nimetumia njia zote kumtongoza mpaka na hirizi zinazopumua lakini holaa!

Hivi nakosea wapi..?
Au ndo kusema mungu na waungwana shetani na wahuni 😅
 
Mkuu kwanini usihamie hukohuko Uingereza na wewe? Yaani umekaa Mbagala tu, Rihanna akija huko wahuni si watapora mpaka chupi.
 
Huyo dada mi nampenda!
Sijui nimwambie vipi ili ajue kuwa nampenda..
Nimetumia njia zote kumtongoza mpaka na hirizi zinazopumua lakini holaa!

Hivi nakosea wapi..?
Au ndo kusema mungu na waungwana shetani na wahuni
mpe mimba,hakusumbui ten.
 
Back
Top Bottom