TANZIA Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi, Mafumu Bilal Bombenga afariki dunia

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
MAFUMU BILAL HATUNAYE TENA

Gwiji wa Saxophone na mwimbaji mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini, Mafumu Bilal Bombenga amefariki dunia usiku huu.

Mafumu aliyetamba na bendi kadhaa zikiwemo Maquis, MK Group, Bicco Stars, Bima Lee, African Stars na African Beats, amefariki baada ya kuzidiwa ghafla jioni ya leo.

Mke wa Mafumu amethibitishia kifo chake na kusema kuwa mumewe amefariki na kwamba hali yake ilibadilika ghafla jioni ya leo na kuaga dunia muda mfupi baadae.

Mafumu alikuwa akisumbuliwa na sukari kwa muda mrefu hali iliyopelekea kukatwa kwa mguu wake wa kushoto.

Mafumu amewahi kueleza kuwa alijifunza Saxophone 1972 JKT Makutupora kwenye Brass Band yao

1589225418964.png


Moja ya nyimbo ambazo zilikuwa na ufundi wa Mafumu

 
Mwenyezi Mungu amrehemu. Jamii forum Ebu fungueni jukwaa la misiba maana naona mmegeuza jamvi kuwa notes board ya obituary ya misiba, kwanza mnaongeza hofu kwa wananchi na pili vifo vipo kwa kila mmoja kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu tusifanye kama tunafurahia.
 
Kama kifo kipo tu, mbona una-panick?
Mwenyezi Mungu amrehemu
Jamii forum Ebu fungueni jukwaa la misiba maana naona mmegeuza jamvi kuwa notes board ya obituary ya misiba, kwanza mnaongeza hofu kwa wananchi na pili vifo vipo kwa kila mmoja kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu tusifanye kama tunafurahia
 
Back
Top Bottom