Mwanamuziki Chakachaka alizwa na kifo cha malaria Mtwara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamuziki Chakachaka alizwa na kifo cha malaria Mtwara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 26, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,547
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  Date::4/25/2009
  Mwanamuziki Chakachaka alizwa na kifo cha malaria Mtwara

  Na Mpoki Bukuku, Mtwara

  Mwananchi


  [​IMG]
  Mwanamuziki maarufu wa Afrika Kusini Yvonne Chakachaka, akibubujikwa na machozi baada mtoto kufariki kwa malaria na mama yake kuondoka na maiti yake akiwa ameibeba mgongoni.​


  MWANAMUZIKI wa Afrika Kusini, Yvonne Chakachaka jana alibubujikwa na mchozi baada ya kusikia kuwa mtoto aliyekuwa amelazwa kwa malaria amefariki dunia na mama yake kuondoka na maiti mgongoni.

  Yvonne ambaye pia ni Balozi wa Malaria duniani alikuwa akigawa vyandarua vyenye dawa katika wodi namba tano ya hospitali ya Mkoa wa Mtwara, Lugula alipokuwa amelazwa mtoto huyo.

  Alipofika wodini hapo, aliambiwa kuwa alikuwapo mgonjwa huyo, lakini alifariki dunia jana na mama yake akalazimika kuubeba mwili wa marehemu mgongoni kutokana na kukosa usafiri, ndipo mwanamuziki huyo alishindwa kuzuia machozi.

  "Najua wengi mmeshangaa nilivyolia, lakini kama mzazi imeniuma, kwa kuwa siamini kama kunaweza kuwa na tukio kama hilo katika bara letu la Afrika," alisema.

  Alisema hiyo ilikuwa siku mbaya maishani kwake na hawezi kuondokana na kumbukumbu ya tukio hilo.

  "Nimeamua kununua gari moja ambalo litakuwa linatumika maalum kwa ajili ya kina mama na watoto wanaosumbuliwa na ugonjwa huu sugu hapa nchini."


  Alisema kuwa kwa sasa anaangalia uwezekano wa kuja kuishi nchini na kama ikiwezekana iwe Mtwara, ili aweze kusaidiana na akinamama ambao wanapata matatizo ya watoto na uzazi.

  "Sioni sababu ya sehemu kama hii nzuri kuwa na matatizo, mimi nimeipenda Mtwara, nimetembelea baadhi ya mikoa Tanzania, lakini naona nchi hii ni ya kuwa makazi yangu ya baadaye," alisema.

  Chakachaka ambaye aliwasiri juzi kwa ajili ya kushuhudia maadhimisho ya siku ya Malaria duniani alitembelea Hospitali ya Ligula na baadaye kufanya onyesho katika viwanja vya mashujaa na kuhutubia wananchi.

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyekuwa mgeni rasmi, alisema kuwa mikoa ya kanda ya ziwa ndio imekuwa ikiongoza nchini kwa kuwa na asilimia 34 ya maambukizo ya malaria ikifuatiwa na mikoa ya kusini asilimia 30 na mikoa ya magharibi asilimia 21 wakati mikoa mingine ni asilimia 14.

  Alisema kuwa wengi wa wanaoathirika zaidi na ugonjwa huo ni kina mama na watoto wenye umri usiozidi miaka mitano. Takwimu za watoto waliofikishwa kwenye vituo vya afya zinaonyesha kuwa mwaka 2003 watoto 7,907 walikufa wakati mwaka 2004 watoto waliokufa walikuwa 8,853 na mwaka 2006 watoto 8,297 wakati mwaka 2007 walikufa 6,676.

  Pinda alisema kuwa wananchi wanatakiwa kusema malaria haikubaliki na hivyo kusafisha mazingira yao ili kuondoa mazalia ya mbu, kutoa kipaumbele katika kupuliza dawa katika nyumba zao na kutumia vyandarua vyenye dawa.

  Takwimu zilizotolewa na Waziri wa Afya, Profesa David Mwakyusa zinaonyesha kuwa zaidi ya watu 20,000 nchini hufa kwa malaria kila mwaka.

  "Utafiti wa wizara yangu unaonyesha idadi kubwa ya wananchi hawajikingi na mbu waenezao malaria wakati wa kulala na hivyo kutoa sadaka miili yao ili ing'atwe na mbu ambao huambukiza vimelea vya malaria na kuleta maradhi," alisema Mwakyusa.
   
 2. O

  Ogah JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuendelea kufa kwa ugonjwa wa Malaria ni UNYAMA UNOAFANYWA NA SERIKALI dhidi ya wananchi
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Apr 26, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Jambo la kusikitisha sana. Kuivunja vicious circle ya umaskini ni kazi ngumu, amabyo kwa bahati mbaya tumewapa jukumu hilo viongozi mafisi na majambazi.
   
 4. Killuminati

  Killuminati JF-Expert Member

  #4
  Apr 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2007
  Messages: 321
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hiyo hospital nina experience nayo ya maumivu, ilikuwa rubbish back then and it looks like it is still trash todate. Mungu amrehemu mtoto huyo, apumzike kwa Amani.

  Wizara ya Afya my as*, it should be called Wizara ya Misala.
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Apr 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Inaskitisha kweli yaani mijitu inaiba tu uko serikalini wakati huku kuna wananchi wanyonge masikini wanakufa kwa maradhi yanayotibika?! Watanzania amkeni, shida hizi za kujitakia jamani...!!!
   
 6. moza

  moza Member

  #6
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Roho imeniuma sn kwani sijategemea km hayo yangewez akutokea. Mungu amrehemu mtoto huyo na mungu ampe subra huyo mama!
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Apr 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Yaani habari inasikitisha sana: sasa mbona Mawizarani haya magari yapo mengi sana kwani yanafanya nini??

  Kwa nini haya magari yasipewekwe huko mahospitalini vijijini kusaidia wagonjwa?
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Apr 26, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...naam, bora amejionea ukweli, Rushwa iliyokithiri inatufanya roho za kibinadamu kututoka, tunageuka wanyama! Kinachouma zaidi ni kwamba;

  Katika msafara huo lazima kulikuwa na msururu wa magari ya Viongozi akiwemo Waziri Mkuu Pinda, tena wenyewe wamejifungia vioo wasipatwe na vumbi na huku wakijipulizia viyoyozi!

  ...huenda gari hilo la msaada likatumiwa na mkuu mmoja wapo wa kitengo 'kutanulia' mpaka saa nane za usiku na vibaa-medi!

  Bora Yvonne ahamie huko Mtwara, maana hata MKAPA mwenyewe amepakimbia, kaenda jenga Lushoto milimani huko!
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Apr 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,547
  Likes Received: 81,981
  Trophy Points: 280
  Wako busy kununua mashangingi yenye kugharimu kati ya shilingi millioni 100 hadi milioni 150 ambapo kwa bei hiyo unaweza kabisa kupata ambulance 2 hadi 3.
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Apr 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  watu wako busy focus yao sasa hivi ni 2010........
   
Loading...