Mwanamsafara: CCM hatuna chetu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mmoja wa wanamsafara wa Sekretarieti mpya ya CCM iliyo ziarani mikoani,amefunguka. Mwanamsafara huyo ambaye anatokea upande wa Zanzibar kuingia kwenye Sekretarieti,amesema kuwa sera ya kuzunguka imeshindwa mapema. ' Hakuna mafanikio. Hali ni ngumu. Ndio kwanza tumeacha ugomvi nyuma yetu. Wanachama wanahoji iweje shughuli za chama zimilikiwe na viongozi wa Serikali?' alisema . ' Nadhani mikutano ya hadhara si aina yetu ya mapambano ya kisiasa. Hatutafanikiwa. Aibu tupu' aliongea kwa kwikwi mjumbe huyo. Afadhali yetu sisi tuliobaki dar
 
Si mlisema Kinana mwanamapinduzi,mwanauchumi na kiboko wa chadema.? Sasa tena imekuaje.?
 
Watashindana ila hawatashinda, maana sie tuna Mungu, to be frank this is the last slap, yaani haitakuwepo kujivua gamba wala kujivika ni kufa kabisa
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Acheni kuzunguka timizeni ahadi zenu:
1. Barabara iwe bora, foleni iishe
2. Huduma za afya hali ni mbaya na inazidi kuwa mbaya - watu wanalala chini Muhimbili bila huduma
....
....
....
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Mmoja wa wanamsafara wa Sekretarieti mpya ya CCM iliyo ziarani mikoani,amefunguka. Mwanamsafara huyo ambaye anatokea upande wa Zanzibar kuingia kwenye Sekretarieti,amesema kuwa sera ya kuzunguka imeshindwa mapema. ' Hakuna mafanikio. Hali ni ngumu. Ndio kwanza tumeacha ugomvi nyuma yetu. Wanachama wanahoji iweje shughuli za chama zimilikiwe na viongozi wa Serikali?' alisema . ' Nadhani mikutano ya hadhara si aina yetu ya mapambano ya kisiasa. Hatutafanikiwa. Aibu tupu' aliongea kwa kwikwi mjumbe huyo. Afadhali yetu sisi tuliobaki dar

Mzee Tupatupa,

Kwani wewe bado ni kiongozi CCM? Mimi nilifikiri umeishajitoa kama ulivyodai wakati ukiwa Kizota kwamba uko mbioni kuitisha press conference kutoa dukuduku lako kuhusiana na 'mizeng'we' ndani ya CCM.

-Huoni kama ni morally wrong kulipwa pesa za walipa kodi na michango ya wanachama wakati hufanyi kazi za chama. It's thieving.

-Hujui ni kosa lisiloelezeka pale mtu anapokuwa traitor

-hujui uongo ni dalili ya binadamu kuwa na psychological defect

PLEASE COME CLEAN AND WE ARE NOT THAT FOOLS AS YOU MAY THINK
 
W J Malecela, unayasikia wayasemayo wana ccm? Hao siyo wanafiki ni wakweli. Lakini kijana wewe umejaliwa umbo kubwa zuri na bonge la bichwa, lakini akili hakuna. Uwe fair kwa mambo ya kitaifa wewe. Nchi hii yetu sote, usitegemee ccm kutawala milele, haipo hiyo. NI BIG NO!
 
Lazima tukomae nao hawa majangili. Ni kweli CCM wamechokwa na kupoteza uhalali na utashi wa kisiasa kuliongoza hili Taifa, lakini kutoka madarakani kwa hiari/kura ni ngumu sana.

Uteketezaji wa fedha za umma (kodi zetu) unaendelea kwa kasi ya jet. Hizi ni hujuma zilizopangwa na ziko wazi, zinazotekelzwa na CCM ili kuwaumiza wananchi.......ktk mfululizo wa utamaduni wa kifisadi na ubadhirifu wa awamu hii ya nne.
 
acheni kuzunguka timizeni ahadi zenu:
1. Barabara iwe bora, foleni iishe
2. Huduma za afya hali ni mbaya na inazidi kuwa mbaya - watu wanalala chini muhimbili bila huduma
....
....
....

3. Watanzania tunaish kwa kula mlo mmoja kwa siku hali ni mbaya sana
 
sio kinana wala chadema watakaoleta mapinduzi ya uchumi tanzania.........ni siss watanzania kwa umoja wetu tukishikamana na kukataa umaskini kwa kuweka viongozi thabiti wenye upeo na uwezo

Singependa utafsiri kwamba nimekutukana ila uelewe tu kwamba ulichoandika hapa ni pumba zinazoonyesha jinsi usivyoelewa mambo. lakini pata nafasi hii kujifuza kwamba, hakuna maendeleo unayoweza kuyaleta kwenye nchi bila vyama vya siasa kwa mfano mfano wako CHADEMA ama chama chochote, ODM, DEMOCRAT, Labor nk. kwa vile ndiyo vyenye forum ya watu na mipango ya kupanga sera ambazo wewe na mimi tutazisafiria ili tujiletee aendeleo, kwa mfumo ulivyo duniani haijapata kutokea nchi ikaenda kama uavyofiki wewe, labda nchi ya kusadikika. unachosema wewe ni sawa na kusema mwanamke apate mimba bila kukutana kimwili na mwanamme, biologically impossible!!!
 
Hali ni mbaya kwa CCM, hali hiyo wanaojua ni ccm wenyewe.

Watu zamani walikuwa wanatenganisha makosa ya serikali na CCM. Lakini sasa wengi watajua kuwa CCM na serikali lao mmoja hivyo CCM ijiandae kupokea matunda ya serikali yao kushindwa. Wananchi watawaadhibu kwa pamoja>
 
Mtoto wako akifeli shule kwa sababu ya elimu mbovu
Ndugu/mtoto amefariki kwa sababu ya huduma duni za afya au mgomo baridi wa wataalamu wa afya
Usalama wa raia na mali zao

Ndiyo utajua wajibu wa serikali ni nini!
 
ccm wameumizwa na kitendo cha madereva toyo wa arusha mjini kukataa elfu 10000 na badala yake ikawabeba kutoka monduli na mto wa mbu.bado haikusaidia kwani mkutano ulidoda .
 
Si mlisema Kinana mwanamapinduzi,mwanauchumi na kiboko wa chadema.? Sasa tena imekuaje.?

Chadema ataiwezea wapi? Anawaonea NDOVU huko maporini ataiweza nguvu ya umma? Operesheni iliyoshindwa kabla ya kuanza.
 
W J Malecela, unayasikia wayasemayo wana ccm? Hao siyo wanafiki ni wakweli. Lakini kijana wewe umejaliwa umbo kubwa zuri na bonge la bichwa, lakini akili hakuna. Uwe fair kwa mambo ya kitaifa wewe. Nchi hii yetu sote, usitegemee ccm kutawala milele, haipo hiyo. NI BIG NO!

It has come to my attention that he has just passed 54! Naomba kujua ujana unaanzia na unaishi wapi? Mtu yuko kwenye voluntary retirement age halafu anajiita kijana na haishi kutema pumba kila uchao!
 
Singependa utafsiri kwamba nimekutukana ila uelewe tu kwamba ulichoandika hapa ni pumba zinazoonyesha jinsi usivyoelewa mambo. lakini pata nafasi hii kujifuza kwamba, hakuna maendeleo unayoweza kuyaleta kwenye nchi bila vyama vya siasa kwa mfano mfano wako CHADEMA ama chama chochote, ODM, DEMOCRAT, Labor nk. kwa vile ndiyo vyenye forum ya watu na mipango ya kupanga sera ambazo wewe na mimi tutazisafiria ili tujiletee aendeleo, kwa mfumo ulivyo duniani haijapata kutokea nchi ikaenda kama uavyofiki wewe, labda nchi ya kusadikika. unachosema wewe ni sawa na kusema mwanamke apate mimba bila kukutana kimwili na mwanamme, biologically impossible!!!
ungeelewa wazo langu usinge kurupuka......watanzania hatuna mshikamano tunaenda na peer presha badala ya kuchagua kiongozi mwenye sera na uwezo wa kutuongoza tunaendeshwa na itikadi .....mimi chadema..mimi ccm sio dawa
dawa ni kuchagua kiongozi bora kutoka na sera alizo nazo
 
Kwa kashfa aliyonayo Kinana sasa hivi (Ya Tembo wetu) kumzungusha nchini ni kuzidi kukiua chama. Hii ni neema kwa wapenda mabadiliko Tanzania. CCM wanakosa kusoma halama za nyakati
 
Back
Top Bottom