Mwanamke wangu simuelewi amekuwa staki nataka kuhusu suala la kuwa na mtoto

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Miezi miwili iliyopita kipindi tunasherekea birthday yake akitimiza miaka kwa kuwa umri umeenda aliniambia mwaka huu Lukasi anahitaji mtoto na kuhusu swala la maisha baada ya kujifungua nimwachie mwenyewe atapambana kiasi flani na mimi nipambane kiasi flani tutakachopata to save kwa ajiri ya mtoto hivyo akanipatia muda nijiandae na majukumu tulikubaliana japo mimi kimoyoni nilikuwa nimekubali shingo upande ila sikuwa tiyari.

Sasa leo asubuhi alinipigia simu tukazungumza mambo mengi baada ya muda akagusia swala la mtoto akitaka kufahamu nimejipangaje nyumbani kwao kipindi akiwa na mimba yangu atawaelezea nini, je nipo tiyali kwenda kujitambulisha na ikitokea nimejitambulisha nimejianda kutoa mahali lakini je mtoto akizaliwa nitaweza kumtunza na kusimamia majukumu kwa kifupi mambo ni mengi lakini mwisho wa siku nimegundua hayupo tayari

Kwa wale wanaowajua wanawake hebu nisaidieni binti anapoonesha dalili kama hizi kubadilisha mawazo kwenye jambo kama hilii ili nianze kuchukua hatua sahihi
 
Huyo sio kwamba hataki mtoto wala si kwamba hakupendi. Wanawake wanataka security ikiwemo social security na financial security. Hakuna mwanamke anataka aolewe na hoehae maishani wala hii haitafsiri kuwa wanapendea pesa.
Yani umuoe leo, kesho awapigie simu ndugu zake kuwa hana hela ya kwenda kliniki wakati wewe upo?

Anataka kuwa na wewe ndio maana kakuuliza maswali ya msingi. Yupo katika wakati wa kuamua kama unafaa au haustahili kuwa baba kwa sasa, either akuongezee muda au atafute aliye tiyari.
What if akapata complications akiwa mjamzito au mtoto akiumwa sana. Vipi kuhusu shule, malezi ya watoto, mahitaji muhimu ya familia, uwekezaji, n.k.

Mapenzi sio huruma. Wewe unataka huruma hapa mtoto wa mtu ajilipue unless kama una promised future. Mkipendana mtachemsha upendo mle chamchana?
 
Inawezekana wewe ni chenga kifikra au mtazamo. Au future yako na mfuko wako hausomi
 
Mkuu binti yuko sahihi, swala la Kuzaa akiwa kwao ni swala la aibu kwake, pia akizaa usipowajibika ndio mbaya mbovu zaidi.

Mtoto anahitaji uwajibike wakati wa ulezi na ndio maana anakuhoji hayo yote!
 
Wanaosema mwanamke yupo sahihi wanakudanganya Kwa kifupi tuu mwanamke mpka anakuuliza maswali hayo tiyali majibu anayo kichwani mwake kwa sababu anakujua in and out
Na maisha yako anayaelewa vizuli ...

Mwanamke mwenye busara na anayekupenda kwa dhati na anapenda mfike mbali kwa kuwa anailewa hali yako angekuweka chini na kukushauli hili jambo muende Nalo vipi na jinsi gani mnaweza kuvuka hatua hiii

Hivyo basi ninachokiona mimi huyo mwanamke wako tiyali ana PLAN B muda mrefu hivyo hapo anajaribu kufanya maamuzi kama aendele na wewe au asiendele na wewe kama atakuwa yupo tiyali kukusubili au kusepa aendele na mtu mwingine ambae anamuona yupo vizuli tuu
 
Alikuwa anakupima kuona uelekeo wako na mipango yako juu yake,kashakuona mpigaji tuu huna lolote nani akubali kuzaa na mtu asiye na dira,sio rahisi
 
Mara hii unajisahaulisha kuwa ulikubali kwa SHINGO UPANDE ila hukuwa TAYARI?

Wewe ndo hueleweki, na demu kakupima kaona HUTOSHI... sasa nini KULIALIA!
 
Wewe ni kilaza. Unasema hukuwa tayari sasa unalalamika mwanamke hayuko tayari. Badala ya kufurahi amekurahisishia.
 
Kaka unataka kuzaa bila kufunfa ndoa, ila umeshtukia huo ni kama mtego wa kuharakisha ndoa... Kama unamalengo na ndoa na uchumi unaruhusu, tandika kibendi... Otherwise, kama badobado endelea kuenjoy mzigo huo ila ukiwa unajua muda wowote unapigwa kibuti
 
Huyo alikuwa anakupima tu, usikute kuna mtu anataka kuzaa naye zaidi ya wewe. Alikuwa anakupa stress tu ili ukimbie na yeye aweze kujivinjari na mtuwe, si mimi lakini. Soma alama za nyakati.
 
Back
Top Bottom