Mwanamke wangu niliyezaa naye tumezinguana. Roho inaniuma naombeni ushauri wenu

Member wote wa JF kwangu ni kama sehemu ya familia. Humu unaweza kupata ushauri mzuri sana ambao unaweza kubadirisha maisha yako ina a positive way.

Ndugu zangu kwa huo utangulizi naombeni ushauri wenu kuhusu haya mahusiano yangu.

Siku ya Xmass nilileta uzi humu kuhusu wife kunikamata red handed nikijiandaa kutoka kwenda kula Xmass na mama wa mwanangu japo wengine mlimuita mchepuko.

Siku ile nilienjoy vizuri tu na mama wa mwanangu na niliweza kurudi mapema nyumbani ili kumtuliza wife. Wife nilimkuta ana huzuni kubwa hata kula hakuweza.

Niliingia nikiwa nimevaa sura ya upole na kumkalisha wife chini na kuzungumza naye.

Nilimuomba wife ajaribu kunielewa. Utetezi wangu mkuu ulikuwa ni kwamba "yule mwanamke nimezaa naye, hivyo mtoto wake hana tofauti yoyote na hawa watoto wetu wa humu ndani, hivyo hata yeye na mtoto wake wanastahili better treatment as you and our children".

Wife kwa sababu ananipenda hakutaka kuongea sana ila aliendelea kununa japo baadae alikaa sawa na amani ndani ya nyuma ilirejea.

Ushauri ninaouomba kwenu ni kuhusu huyu mpenzi wangu niliyetoka naye siku ya Xmass. Jumapili ya 29 Dec nilimtaarifu huyu mama wa mwanangu ningekuja kwao kumchukua tuende zetu sehemu lakini alinikatalia kwa kisingizio eti kachoka anataka kumpumzika.

Nilimwambia hatutaenda mbali, nataka tutoke kidogo tu then tutarudi. In fact yeye alihisi nataka kwenda kula tunda hivyo alikuwa anadai yeye amechoka na mimi nilimsistizia lengo langu wala sio kula tunda.

Baadae alikubali akasema nimfuate. Basi muda umefika namcheki kwenye simu nakuta simu haipatikani, nikaendelea kumcheki now and then bado tu simu haikupatikana. Baadae baada ya kupita kama saa moja hivi akapatikana.

Swali la kwanza nilimuuliza kwa nini simu umezima, akasingizia eti network ndio shida ila hakuzima simu.

Nilihisi anaongea uongo hivyo nikampandishia, nikamkoromea akanikatia simu na kuizima kabisa. Baada ya kama nusu saa hivi simu ikaanza kupatikana tena. Nilichomwambia tusijuane.

Kusema ukweli huyu mwanamke nampenda na hapa nafsi inanisumbua sana. Najishauri sijui nimrudie, sijui nimpotezee mazima tu. Naombeni ushauri wenu.

Kama huna cha kushauri naomba upite kimyakimya tu badala ya kutoa kejeli.
Natanguliza shukrani zangu za dhati.
PUMBAVU, PUMBAVU WEWE! narudia WEWE NI MPUMBAVU!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Subiri na yeye akianza kutafuta aliemtoa bikra au aliemkuna vizuri mwanzoni kisha ulete uzi wa mke wako anachepuka
 
Pale unapo mchukulia poa make wako, unaanza kuhangaika na mzazi mwenzio ambaye naye nafikiri ana ndoto za kuja kuwa na mume........ Labda utakuja na ungunduzi mwingine mkuu
 
Nyie masingle parents muwe mnaoa au kuolewa na wazazi wenzenu tu wa awali, hili kuwaepushia na balaha hao watoto wa wenzenu mnaofunga nao ndoa mpyaa.

Sasa angalia kama wewe hapa yaani huyo mke wako anaonekana amebeba balaha zito humo ndani analoliita mume, sipati picha jinsi atakavyojiskia endapo kama atabahatika kusoma hichi ulichokiandika hapa.

Hakika ukioa au kuolewa na single parent wewe ni mwizi wa mali ya watu na siku yoyote inarudi ilipotoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumbe shida sio single mothers tu.
Kuna wanaume ni tatizo pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani mkuu. ...Sikumuoa kwa sababu tayari nina mke ila nataka nimuoe hivyo hivyo hata kwa taratibu nje ya dini. ...By the way nikimtafuta si ataniona najipendekeza? Mimi mwenyewe ndio nilimwambia tusijuane halafu tena mimi ndio nianze kumtafuta huoni kama atachukua point zote tatu?
Acha ujinga wee jamaa unatakiwa uwe na msimamo kama unahisi una muhitaji nenda kama hakufai acha una lia na kinacho kuliza unalijua kwann usijitibu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mfia nchi, Ndo maana kuna jamaa hapo juu amekwambia hujitambui.

Unaendeshwa na tamaa za ngono! Tunza na kulea familia yako na huyo mtoto wa nje mlee pia lakin suala la ngono kwa huyo mama wa nje unafanya ujinga tu ambao utakucost badae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom