Mwanamke wa kwanza mtanzania mwenye kumiliki Hoteli 5 za Kitalii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke wa kwanza mtanzania mwenye kumiliki Hoteli 5 za Kitalii

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by X-PASTER, Jul 5, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Alikuwa mwajiriwa wa ATC, sasa anamiliki hoteli 5 za kitalii

  [​IMG]
  WANAWAKE kwa muda mrefu wamekuwa wakiaswa kujituma na kujiamini ili waweze kufanikiwa katika kutimiza ndoto zao.
  Kujiamini huko kunaweza kuwa na manufaa mengi katika kuinua maisha ya wanajamii hasa kama mhusika atakuwa akijiamini na kuanzisha mradi wake wa kujiajiri na kujikuta akiajiri watu wengine wengi. Zainab Ansell, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Utalii ya Zara ni miongoni mwa wanawake waliojitoa mhanga, kwa kuacha ajira na kuamua kujiajiri.


  Kwa kuwa alikuwa na malengo, Zainab amefanikiwa si kujiajiri kwa mafanikio tu, bali pia ameweza kutoa ajira kwa maelfu ya Watanzania, hususan vijana.

  Kwa Zainab, mzaliwa wa Hedaru, Same mkoani Kilimanjaro awali alikuwa ameajiriwa na Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), mnamo mwaka 1984 akiwa kitengo cha kukata tiketi za ndege za shirika hilo ambalo kwa sasa liko taabani kiuchumi.

  Miaka miwili baada ya kuajiriwa, mama huyo aliyezaliwa mwaka 1959 aliamua kuingia rasmi katika ujasiriamali.

  Lakini leo hii, ikiwa ni miaka 25 tangu achukue uamuzi wa kujiajiri, Zainab hana cha kujutia, zaidi ya kujipongeza kwa mafanikio yaliyovuka milima na mabonde, kiasi cha kuwa mwanamke wa kupigiwa mfano.

  Na haikushangaza kuona mwaka huu akitangazwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Mwanamke Bora Mjasiriamali katika tuzo za Mwanamke Bora zilizoandaliwa na Kampuni ya Frontline ya jijini Dar es Salaam.

  Mafanikio yake yametokana na kupanuka kwa biashara zake kwa kiasi kikubwa, sasa akiwa anamiliki kampuni kubwa ya utalii, ikiwa na hoteli tano za kitalii, kwa ujumla akiwa na zaidi ya wafanyakazi 9,000!

  Katika mazungumzo na HABARILEO Jumapili, Zainab anasema kuwa tangu alipoamua kujiajiri, alilenga kujituma ili aweze kutimiza ndoto ya kuwa mwajiri na mmiliki wa vivutio vya utalii nchini.

  Akizungumzia alivyoanza biashara, anasema kuwa mwaka 1986 akiwa katika ofisi za Air Tanzania aliingiwa na shauku ya kuwa anasimamia safari za watalii wake mwenyewe huku akiwakatia tiketi na kuwapeleka Mlima Kilimanjaro na kwingineko kwa shughuli za kitalii.

  Anakumbuka wakati huo alikuwa na umri wa miaka 27 tu (sasa ana umri wa miaka 52), alifunguka macho na kuamua kufungua ofisi yake katika eneo la Hoteli ya Moshi ambapo alikuwa na wafanyakazi watatu mwaka huo.

  Anasema kwamba, alianza katika mazingira magumu, akivizia watalii katika kituo cha mabasi na kuwashawishi kwenda kupanda Mlima Kilimanjaro chini ya kampuni yake, huku akisisitiza kuwa, siri kubwa ya kuwamudu wateja hao ilikuwa ni kauli nzuri na kuwa mchangamfu.

  “Ni kwamba kila kukicha nilikuwa najipangia mikakati mipya juu ya nini nifanye ili niweze kuinuka na kusaidia jamii inayonizunguka na ndipo nikajikuta naona umuhimu wa kuwa na hata hoteli za kuwasaidia watalii wanaotumia huduma za kampuni yangu,” anasema Zainab. Ndoto yake ya kuanzisha hoteli ilitimia mwaka 1996, yaani miaka kumi tangu alipoanzisha kampuni.

  “Kwa muda mrefu nilikuwa nikiwapeleka watalii wa kampuni yangu katika hoteli mbalimbali kwa ajili ya malazi, kufikia mwaka 1996 nilianzisha hoteli yangu,” anakumbuka mama huyo anayefichua kwamba, hoteli yake ilianza ikiwa na chumba kimoja tu, ingawa kwa sasa ni moja ya hoteli kubwa mjini Moshi.

  Inaitwa Spring Land Hotel, sasa ikiwa na zaidi ya vyumba 100 vya kulala, sehemu za kulia chakula, baa moja, bwawa la kuogelea, sehemu ya kuangalia runinga. Pia hoteli hiyo kwa sasa ina bustani zaidi ya nne za kupumzikia, sehemu ya kuchua mwili (massage), sehemu ya mazoezi na sehemu ya kupata joto hasa wakati wa baridi (sauna).

  Anasema baada ya kuanzisha hoteli hiyo, ilimwezesha kutoa huduma za kiutalii vyema zaidi kama vile utalii wa kwenda msituni kutembea, utalii wa Moshi mjini kwa baiskeli, kwenda Masai Boma, Marangu na shughuli nyingine muhimu.

  Katika kufanikisha ndoto hiyo ya kuwahudumia watalii ameweza kufungua huduma za hoteli zake sehemu nyingine nyingi kama vile Serengeti Wild Camp iliyopo ndani Mbuga ya Serengeti, Ngorongoro Wild Camp iliyopo ndani ya Mbuga ya Ngorongoro na High View Hotel iliyopo katika eneo la Karatu.

  Akizungumzia wito wake kwa Serikali kuhusu kuwasaidia wanawake katika kuendeleza utalii anasema kuwa inatakiwa Serikali kuwapa kipaumbele wanawake waliowekeza katika sekta ya utalii kwa kuwapatia maeneo ya kujenga hoteli.

  Anasema kuwa kwa kumwezesha mwanamke kuwekeza katika sekta ya hoteli kutasaidia kuendeleza jamii inayozunguka katika maeneo ya hoteli ambapo anatolea mfano wa kampuni yake ilivyoanzisha Taasisi ya kusaidia jamiii iitwayo Zara. Anasema kuwa kupitia taasisi hiyo ameweza kuwasaidia watoto wengi kwa kuwapatia elimu, na huduma nyingine muhimu za afya na za kiroho.

  Pia ni mwanzilishi wa Chama cha Wabeba Mizigo wa Wapanda Mlima Kilimanjaro ambapo kupitia chama hicho vijana zaidi ya 3,000 wanapata elimu, mikopo pamoja na misaada mbalimbali ya kijamii. Chama hicho alichokianzisha kwa sasa kinatambulika kimataifa kwa kuwa kupitia wabeba mizigo hao, watalii wengi wameweza kupitishia michango yao na kuifikia jamii.

  Anasema kuwa asilimia moja ya fedha anazolipwa mbeba mizigo ya watalii inawekwa katika chama hicho na mwisho wa siku hutumika kuwasaidia wanajamii pamoja na wao wabeba mizigo wenyewe.

  “Huruma tuliyonayo wanawake inatufanya kuwa na hali ya huruma ya kutaka kuona jamii ituzungukayo ikiendelea zaidi hivyo tukiwezeshwa kumiliki rasilimali kutatufanya kuisaidia jamii yetu kwa hali na mali hasa kwa kuwapatia mahitaji muhimu” anasema Zara.

  Anasema kuwa licha ya kupatiwa tuzo ya kuwa mwanamke mjasiriamali bora wa mwaka, lakini pia ameweza kupatiwa tuzo ya kutambuliwa mchango wake katika sekta ya utalii iliyotolewa nchini Hispania na taasisi ya Bonestor iliyowahusisha akinamama wengine wawili mmoja akitokea nchini Senegal na mwingine Msumbiji.

  Pia amewahi kupata tuzo kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) yenye kutambua mchango wake katika masuala ya kijamii. Zainab, mama wa watoto wawili, mmoja akiwa ni meneja wa hoteli yake iliyopo Karatu nje kidogo ya Mbuga ya Ngorongoro anaitwa Leyla na mwingine Anna yuko masomoni Sweden. Anapendelea kuangalia vipindi vya utalii na mazingira katika runinga, huku akiwa anapendelea zaidi kula vyakula vya asili anapenda michezo hasa riadha.

  Akizungumzia tuzo ya Zainab ambaye kampuni yake ina mtandao mkubwa wa ofisi ndani na nje ya Afrika, Mkurugenzi wa Kampuni ya Frontline iliyomzawadia mama huyo, Irene Kiwia anasema Zara ni mfano wa kuigwa na kuwa Mkurugenzi wake, Zainab amewafumbua macho akinamama wengi katika kuthubutu. Anasema kuwa, Zainab anaweza kutumiwa kama mfano katika kuwapatia moyo wasichana wadogo hasa wa sekondari na vyuo kwa kuwaonesha ni kwa jinsi gani wanaweza kufanikiwa hasa wakijiamini na kuwa na malengo.

  “Binafsi naona kuwa huyu mama ni mfano na ndio maana ameweza kutunukiwa tuzo hii kwa kuwa ameweza kutoka chini kabisa hadi kufika juu kiasi cha hata kuajiri wafanyakazi wengi, karibu 10,000! Jiulize, mtu alikuwa ameajiriwa, leo hii anafanya mambo makubwa hivi, kwanini umuhimu wake usitambuliwe? Kwetu sisi, huyu ni mfano mzuri na wa kuigwa,” anasema Kiwia.

  Huyu ndiye Zainab Ansell, mama mcheshi na mchapakazi ambaye alithubutu kuanzisha kitu chake, akakisimamia, na leo hii anawaacha wengi midomo wazi kutokana na hatua kubwa aliyofikia kimaisha, kibiashara na pia katika kuisaidia jamii na Serikali katika kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Ama kweli, Zainab ni mfano wa kuigwa na miongoni mwa nyota wa kweli katika Tanzania ya leo.
   
 2. Mabagala

  Mabagala JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 1,465
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Aisee hongera zake zimfikie popote alipo
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,102
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Zenunaaaa. Kudos.
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi 9,000? I doubt. Kwa vyovyote vile, anastahili pongezi nyingi.
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Hongera dada!
   
 6. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera Mama, kumbe wewe ndio unatumia Zara Logo?
   
 7. Amina Thomas

  Amina Thomas JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 272
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mh! nimependa sana hii. hongera sana dada.kwanza pamoja na umri lakini amejitunza na kuonekana mrembo. hongera kwa hilo pia!
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  Hongera dada! japo atc ime dead
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Hongera Mama Mjasiriamari Hotel Tano sio mchezo wastahili pongezi.
   
 11. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #11
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Hongeara sana ..
  Mungu azidi kukuzidishia....
   
 12. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  safi sana ....
   
 13. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ebwn nilistuka kusikia High View ya karatu ni yake, nilishafika hapo, hongera sana mama Leyla!!!
   
 14. u

  ureni JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Huyu mama ameolewa na mswidish kitu ninachomsifu ameweza kumbana huyo mzungu mpaka wakainvest Tanzania kiukweli amefanya kitu kizuri.Changamoto kwa wamama wengine mnaopata wazungu wenyeuwezo mkumbuke kuinvest nchini mwenu.
   
 15. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2011
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Sio kati ya ndege zetu, tano zimebadilika kuwa hizo hotel tano za kitalii?!
   
 16. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Salute!
   
 17. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,430
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  Behind every successful woman there is a successful man, huyu mama aliolewa na mzungu na fweza mbaya ndio aliyemtoa ingawa nae ni hard worker. Hongera mama hoteli zako ni nzuri mno
   
 18. CHE GUEVARA-II

  CHE GUEVARA-II JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 531
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Habari kama hizi ndizo waTz wanahitaji kufahamishwa. Siyo kupandishwa cheo. Mtu anajisifu au anasifiwa eti kapandishwa cheo! Unajisifu kuajiriwa? Wewe utaajiri lini? Au ukiwa na house girl/ houseboy nd'o unajisifu umeajiri?

  Mama Zainab hongera sana!
  Wewe ni mfano wa kuigwa hapa Tz!
   
 19. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hongera sana mamaa zai kwa mafanikio makubwa..
   
 20. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hongera sana hii inaonyesha tukiamua wanawake tunaweza
   
Loading...