Mwanamke wa kitanzania na Ujasiriamali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke wa kitanzania na Ujasiriamali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kongosho, Jan 27, 2012.

 1. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Nimeamua kuileta hii mada makusudi kwenye jukwaa la MMU sababu japo inahusu ujasiriamali, pia inahusu pia mahusiano ya jinsia hizi mbili yanavyofanikisha au kukwamisha ufanisi kwa mwanamke wa kitanzania.

  Baadhi ya mambo/visababishi vinavyofanya mjasiriamali kwa kike asifanikiwe (challenges) ni pamoja na:-
  1) ufinyu wa network za kibiashara, si rahisi kwa mwanamke kujichanganya na watu waliofanikiwa kibiashara ambao wengi ni wanamme bila jamii kunyanyua kope
  mfano, mkute kongosho na RM kempisky lazima unyanyue kope, kapata kipya?

  2. Kukosa surport ya makusudi toka kwa wanamme, anapoomba mwongozo au ushauri au msaada wowote mwanamme anataka ajilipe kwanza ndo amsaidie

  3. Mwanamke amelelewa kushika nafasi za usaidizi dhidi ya wanamme wakati mjasiriamali anatakiwa awe kiongozi wa biashara yake na aoneshe njia au uelekeo.

  4. Akina mama wanamajukumu mengi ya kifamilia kama kuzaa na kulea familia inawaachia muda mchache wa kujituma katika ujasiriamali

  5. Uchaguzi wa biashara, kwa kuwa asilimia kubwa ya akina mama wana ufinyu wa mitaji, uzoefu, elimu wanajikuta wamejiingiza kwenye biashara ndogo ndogo zisizo na nafasi kubwa ya kukua mfano genge, saloon za kike?

  6. Baadhi ya sheria na tamaduni zinawanyima nafasi, mfano kutorithi mali. Inawanyima upatikanaji wa dhamana za mikopo

  7. Nafasi ya mwenza kama ameolewa.
  Baadhi ya wanamme hawapendi wake zao wawazidi kipato, wengine hawawaamini wake zao kama wanaweza chochote, wengine wakiona wake zao wamefanikiwa wanakata huduma za famiilia.

  Kwa kusema hayo hapo juu, mwanamke anayejiandaa kuingia kwenye ujarisiamali awe ameyatafakari kabla ya kuanza biashara asije akapata hasara au biashara kufa kabisa.

  Kwa wanamme na jamii nzima kwa ujumla, je mtasaidiaje hiki kizazi cha kike kisonge mbele?

  Ongezeeni sababu zingine ili tuzichambue kwa faida zaidi.

  :( sijui itahamishiwa kwa wajasiriamali, sitaki.
   
 2. V

  Van l Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 74
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  upo juu sana
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wanawake wasaidiwe wakati kila siku tunaambiwa wanawake wanaweza!!?? ni % chache sana ya wanawake ambao wanasupport familia wakiwa na kipato, so kwa upande wangu sioni tofauti ya mwanamke kuwa mama wa nyumbani au kuwa mfanyakazi/ mjasiliamari.
  Pesa ya mwanamke ni ya mwanamke, lakini pesa ya mwanaume ni ya wote. nina experience ya kutosha kuhusu jambo hili, wanawake wa Kibongo wengi wao ni tatizo.
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ubinafsi ndio tatizo.
  Watu wanaoamini wao wana haki ya kupewa/pokea tu ndio zao. Hata likitokea tatizo atasubiri mpaka mume aje atoe pesa yeye wakati hata yeye anayo.
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ujue mkeo kama ana pesa yake, angalau atakupunguzia stress za kumsaidia kwa matumizi yake binafsi na kusaidia kwao.

  Pia ubinafsi wa mwanamke ni kitu chenye mizizi ya ndani ya tamaduni zetu maana imejengeka kuwa wao hawana kipato kwa hiyo hawawezi saidia familia.

  Hii imepelekea hata kuwalemaza wanawake wenye kipato kubweteka na kuwaachia wanamme kutimiza majukumu yote ya kifamilia.

  Ili hali hii kuondoka, wanawake wanahitaji kupewa mwamko kuwa wanaweza miliki mali na biashara kubwa na wao kuweza changia au kuwa mhimili wa kutoa mahitaji kwa familia.

  Lengo langu katika mada hii ilikuwa kujaribu ku-raise awareness kwa wanawake vikwazo vinavyowazunguka hasa katika sekta ya biashara kwa sababu tu wao ni wanawake.
  Nilitamani tupate shuhuda/experience kwa ambao wamesimama kibiashara na challengies walizopata.

   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe Lizzy

  huu ubinafsi wa mwanamke ni kitu cha muda mrefu ambacho mwanamke kajifunza kwenye maisha yake.

  Ni hadi ambapo jamii itaongelea hasa akina baba ndipo mabadiliko yanaweza tokea.

   
 7. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyu ndo kongosho bana he/she
   
 8. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,268
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280

  na mimi mmojawao, cha mume chetu.
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Umesahau kitu muhimu sana Kongosho, discipline! Sie wamama tuna tabia ya kuwa disorganized, na kutotimiza ahadi. Unapata mteja wa product A, kesho akija haipati na haujishughulishi kupata alternative. Mteja ukimuahidi delivery kesho saa 4 hata akikukumbusha huwezi kufanya lolote ku-maintain. Hatuna tabia ya kuheshimu kazi zetu, mfano kama ni duka leo litafunguliwa saa 5, kesho saa 7! Hgeli akiondoka siku 7 limefungwa. Hatujiulizi kama ningekuwa nimeajiriwa, ningeachaje kwenda kazini? Nina utaratibu wa kuhakikisha ofisi inaendelea if I'm down for 2 weeks?
  Discipline kwa wateja pia, kuna mtu akiona mteja hafananii na biashara yake hata akiuliza bei hajibiwi! Ngoja ntarudi tena,lol
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Alafu nilisahau kusema "Ahsante Konnie kwa mada nzuri". . .Source unaijua.

  BTT. . . .
  Mabadiliko yanatakiwa yaanze kwenye malezi, kipindi cha upenzi na kuendelea. Embu hata jiulize wadada wangapi hua wakitoka na wapenzi wao hua wanalipia hata soda tu, achilia mbali vitu vikubwa vikubwa. Yani sijui ni uchoyo au ubinafsi. . . unakuta mtu anamwambia mwenzie "baby twende lunch leo" alafu wakishakula anamsubiria mwalikwa atoe wallet. Sasa mtu akishindwa vitu vidogo vidogo kama hivyo hata kwenye mambo ya kifamilia usimtegemee kabisa!!
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,457
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Hata girlfriend wa mume ni wako pia?
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Lol! Nimesahau point ya mahusiano: wanafamilia kwa ujumla hawaheshimu ujasiriapesa wa mwanamke. Kama ndo mjasiriamali, wifi akiumwa u ar expected kuacha kila kitu ukahudumie, siongelei mama mkwe kwanza! Anytime utaitwa from ur work kama sio order ya mume. Nimeshuhudia mwanamke anaambiwa na mumewe ' kazi yako inanisaidia nini mimi?' Mweeeh!
   
 13. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #13
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,268
  Likes Received: 1,419
  Trophy Points: 280
  as long as simjui kila mtu kwa nafasi na ushawishi wake, changu changu cha mume changu.
   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ndo hayo mambo ya 'surbodinate roles' katika familia.
  Kazi zoote ya kusaidia siku zisonge mbele katika familia ni jukumu la mke.

  Ni kweli hili linawanyima nafasi ya ku-invest muda wao katika biashara.

   
 15. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  afu cha kwako??
  Lakini je, una ndoto kubwa kubwa??

  Maana wakati mwingine ukiwa majukumu makubwa yanakufanya uwe na ndoto kubwa pia.
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  asante kwa kushukuru na hiyo aka.

  Ni kweli, usipowajibika kwa kitu kidogo hata kikubwa inakuwa ngumu sana.

  Unakuta watu wana mahusiano ya mwaka mzima, binti hajawi tumia hata sh elfu tano wakiwa na huyo bf wake.
  Usitegemee mabadiliko baada ya kuoana.

   
 17. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha, raha kuwa shemale.
  Unakula a na b

   
 18. M

  Muinjilisti Senior Member

  #18
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera Kongosho kwa mada nzuri, kwa kifupi imenishika.

  Hili suala la kujiajiri na ujasiriamali kwa ujumla halikwepeki kabisa. Tunajipa moyo kuwa tumeajiriwa, na ukiangalia kipato unachopata mwisho wa mwezi hakiendani na ile bugudha ya kuamka saa 11asubuhi, mafoleni ya Dar na kurudi saa 2 au 3 usiku, hapo ndiyo umemuacha mtoto mchanga, haiendani na risk zinazotokea kwa kuwa mbali na watoto na wakati mwingine unalazimika kumpeleka boarding mtoto wa darasa la kwanza, yaani kwa kifupi kuna hasara nyingi tu. Na mwisho wa siku kuna kustaafu, na kazi/field/proffessionals nyingine ukifika umri fulani inabidi uachie ngazi. Ukishastaafu ndiyo kama Mungu kasaidia unarudi na vijisenti vyako eti uanzishe biashara wakati hata biashara ndogo hujawahi kufanya. Na hapo umri umeenda na thinking ability imeshapungua. Ndiyo maana wengi wanaostaafu hawachukui round wanajichokea, pressure, kisukari wanarudi kwenye makao ya milele.

  Baada ya utangulizi huo, wanawake hatuna budi kufikiria kujiajiri, mimi naamini kuna baadhi ya proffessionals unaweza kabisa kujiajiri na ukapata kipato kikubwa kuliko unachopata kwenye ajira. Na pia ukajipangia muda wa kufanya au kushiriki kwenye mambo yako mengine ya kijamii na kulea familia vizuri tu. Kuna changamoto kama zilivyoainishwa na Kongosho, na sisi wa kizazi hiki tumeathirika na tamaduni zetu ambazo kila siku zinatukumbusha ni viumbe duni, dhaifu, wasaidizi tu nk lakini kama tuna watoto wa kike nyumbani inabidi kuwatia moyo, kila siku unawaimbia kuwa wanaweza, wanaweza kuwa mamilionea, wanaweza kuwa mawaziri, ni maisha gani wataishi inategemea na wao walivyopanga. Hii itasaidia sana maana unachokisia ndiyo unachoamini na kukifanyia kazi. Bila kusahau kuwaonyesha role models ambao ni wanawake waliofanikiwa.

  Mimi hadi sasa nimeshafanya kazi miaka 8, nilishapanga mwaka huu mwishoni, piga ua, garagaza lazima nifungue ofisi yangu na kuitumia taaluma yangu. Na siyo wanawake wote wenye kipato wanaacha majukumu yote ya nyumbani kwa waume zao! Maana kuna wakati na yeye anaishiwa, na si mpaka aishiwe tu, kama mna mipango mikubwa kama kujenga nyumba, kufungua biashara fulani kubwa, inabidi financial resources zitoke kote kote. Ingawa pesa ya chakula na mahitaji mengine ya ndani inabidi itoke kwake, nitasaidia akikwama au nikiona kuna mapungufu fulani. Maana hapa usipoangalia ukamsaidia hata hilo wengine ndiyo wanakuachia majukumu yote.

  Nitarudi....
   
 19. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mi ndomana nakupendaga kwasababu ya mambo unayoongeaga
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mara nyingi wanaume huwa wanasaidiana sana kwenye bishara. kasheshe ni kwa kina mama kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.
   
Loading...