Mwanamke wa Iran aliyefanya mapenzi nje ya ndoa kuuliwa leo kwa mawe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke wa Iran aliyefanya mapenzi nje ya ndoa kuuliwa leo kwa mawe

Discussion in 'International Forum' started by Saint Ivuga, Nov 4, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,869
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Sakineh Mohammadi-Ashtiani

  Wednesday, November 03, 2010

  Mahakama ya nchini Iran imeruhusu adhabu ya kifo inayomkabili mama wa watoto wa wawili wa nchini Iran ambaye alikamatwa akifanya mapenzi na mwanaume aliyemuua mume wake.Pamoja na shinikizo kubwa toka nchi za Magharibi na taasisi za kutetea haki za binadamu, Sakineh Mohammadi-Ashtiani huenda akauliwa leo kwa kupigwa mawe kwa mujibu wa vyanzo vya habari.

  Mwanaharakati anayemtetea Sakineh alisema kuwa wamepokea taarifa toka kwa mtu anayefanya kazi ndani ya mahakama kuwa Sakineh atauliwa siku ya jumatano.


  "Tumepokea taarifa siku tatu zilizopita kuwa Sakineh atauliwa siku ya jumatano", alisema Mina Ahadi, mwanaharakati anayemtetea Sakineh wakati akiongea na shirika la habari la AFP kuhusiana na barua aliyotumiwa na mtu ambaye hakutajwa jina lake.


  Mahakama ya mji wa Tabriz ambako Sakineh ametupwa jela imeruhusu adhabu ya kifo inayomkabili Sakineh itekelezwe. Kwa kawaida adhabu za kifo nchini Iran hutekelezwa siku ya jumatano.


  Tangu mwezi julai mwaka huu Iran ilikuwa ikisema kuwa adhabu ya kifo kwa kupigwa mawe inayomkabili Sakineh haitafanyika mpaka baada ya kuidhinishwa na mahakama kuu.


  Sakine mwenye umri wa miaka 43 ambaye ni mama wa watoto wawili, alihukumiwa adhabu ya kifo na mahakama mbili tofauti mjini Tabriz mwaka 2006.


  Adhabu yake ya kwanza ilikuwa ni adhabu ya kifo kwa kunyongwa ambayo baadae ilibadilishwa kuwa kifungo cha miaka 10 jela. Adhabu hiyo ilitokana na Sakineh kutuhumiwa kushiriki kwenye mauaji ya mumewe.


  Adhabu ya pili ya kifo ilikuwa ni kuuliwa kwa kupigwa mawe kwa kosa la kufanya mapenzi nje ya ndoa na mwanaume aliyekamatwa kwa mauaji ya mumewe.


  Chanzo: Nifahamishe
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  mwanaume aliyefanya naye ngono atauliwa lini? au alijifanya ngono mwenyewe?
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  He jamani hzi adhabu mbona zinatisha sana.. Bado zipo hizi sheria? Na kwa mwanaume inakuaje?

  Kweli wanaruhusu watoto wakose baba na mama kwa adhabu zilizokaa kiubinafsi kama hii. This is so bad!
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Uko sawa bro Ubungoubungo, kwa nini adhabu hii haimuhusishi mwanamume, au machoni pa hawa waIran ni mwanamke tu ndio mzinifu?

  Pamoja na yote haya hivi kweli kwa kosa la uzinifu tu ndio mtu astahili adhabu ya kifo tena kwa kupigwa mawe? hii ni kuonesha jinsi jamii hii ilivyo na kiwango kidogo cha ustaarabu! sawa wanaweza sema eti wanafuata sharia, lakini kwa ufahamu wangu si imeandikwa na sharia hiyohiyo kuwa "

  ....Ama kwa hakika iepukeni zinaa, kwani zinaa ni uchafu mkubwa mno kwenu, na mwanamke mzinifu na mwanaume mzinifu wachapwe viboko mia moja kila mmoja huku ikishuhudiwa na walioamini" Sasa hii ya wazanifu kuuwawa kwa mawe imeandikwa wapi?
   
 5. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sheria nyingine znatakiwa kuachwa kabisa-kama ingekua sheria kama hio ina-apply huku kwetu-wengi wangekuwa washauliwa mpaka sasa
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kungebaki jangwa bila watu!hawa wa iran hawawezi kubadilishiwa vitabu? Hiki kitabu nichazamani sana!
   
 7. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Hodi hodi wana JF,

  Pengine mwanaume yeye alikuwa si mwana ndoa kwahiyo adhabu yake viboko 100
   
 8. bona

  bona JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  ku practise mediaval life style kwa kujifanya hamtaki kubadilisha maneno ndiko kunakosababisha baaadhi ya imani kukosa appeal kwa watu ktk dunia ya sasa iliyostaarabika ndio force inaanza kutumika! kila kitu kina mda wake, watu wazamini walikua ndio kwanza wametoka kwenye u primitive kwa iyo instituition ya law and justice ndio kwanza ilikua inaanza kucopy ujinga huo kuuleta sasa wewe ndio unaonekana mjinga zaidi ndio maana hata wakiulizwa wanakwambia ndio imeandikwa meaning reasoning haitakiwi! kwa dunia ya sasa tumesha advance ndio maana sasa ivi kuna cocept mpya inayosema ''SIO TU HAKI ITENDEKE BALI PIA WATU WAONE HAKI IMETENDEKA''
   
 9. B

  Bull JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii sheria ni nzuri sana na ndio maana wenzetu hawana janga la maradhi ya ukimwi, sisi waafrika wengi wameathirika na bado wanategemea misaada iwaokoe ili wajitibu.


  By the way huyu mama hakufanya kosa la zinaa pekee, pia alishiriki kumuuwa mmewe, kwa kama kauwa nae anafaa kuuliwa.
   
 10. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,475
  Likes Received: 19,869
  Trophy Points: 280
  SHARIA hizo wakuu
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi alijifanya mwenyewe?kama walikuwa wawili then wote wapigwe mawe
   
 12. F

  Far star Senior Member

  #12
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hizi hukumu mimi naona zihamishiwe kwa mafisadi wanaohujumu uchumi wa watanzania, lakini kwa hao wanao chakachuana huko iran wasamehewe kwa kuchapwa viboko
   
 13. F

  Far star Senior Member

  #13
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  alaf ukimuangalia machoni huyu mama wa kirangi unaweza kusema hakufanya hiyo mambo, amekauka mmmmmmmmmmmm!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 14. F

  Far star Senior Member

  #14
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivi jamani hilotendo ni lazima sana kufanya ? Unaona sasa linamgharimu mtu uhai wake,siangejua angeacha tu
   
 15. F

  Far star Senior Member

  #15
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapana ,irani sio kama hapa bongo,watuwanaiba kura wanaachwa,waiba pesa za watanzaia wanaachwa, wanaamua kuongoza nchi wanavyotaka wanaangaliwa tu, hizo ni sheria zao na zina wasaidia kuendesha nchi yao jamani,mbona sisi hatuingiliwi tunapoachia uchafu unapofanyika ktk nchi hii.
   
 16. F

  Far star Senior Member

  #16
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwahiyo huko irani hakuna machangu, au hawasumbuliwi endapo hawajaolewa?
   
 17. F

  Far star Senior Member

  #17
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana huyu mwanamke alifanya mwenyewe bila mwanaume,nasikia alifanya mwenyewe siunajua sikuhizi kuna technohama?
   
 18. sister sista

  sister sista Member

  #18
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 6, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sikubaliani na wewe.inatakiwa ifutwe hii.
   
 19. F

  Far star Senior Member

  #19
  Nov 5, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 139
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu mwanamke anajuta kuwa mwanamke maana inamsababishia kuvunja sheria na kufa
   
 20. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kweli kila nchi ina sheria zake! Tuombe Mungu tusibadili sheria na kuwa kama Iran! Itakuwa noma!
   
Loading...