Mwanamke wa aina hii ukiwa naye basi maisha yako yatakuwa magumu sana

Kilenzi _Jr

JF-Expert Member
Sep 10, 2021
301
1,110
Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo hazifurahishi. Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.

Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mwanamke anayekuganda nguoni
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.

2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.

Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani…nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?

3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

4. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msamaha kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

5. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka

6. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.
 
😀😀😀😀😀Nimependa point ya ASIYEJIELEWA
 
7:MWANAMKE KISWASWADU
Hii ni aina ya mwanamke anaependa ngono kuliko kulaa nakushauri kaa nae mbali atakukata mshipa wa mkojoo ukimjua nielekeze alipo kwa matibabu zaid ahsante
 
Au we unaona nipo wapi? 🤣
2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele.

Acha na maneno mengine, hayo tu yanatosha...
 
😂😂😂😂🙌

Na wabarikiwe wanaojua kupenda kupindukia
 
Back
Top Bottom