Mwanamke unaweza kuacha kazi ili ulee familia?

Uvelia

JF-Expert Member
Sep 23, 2018
640
1,191
Mwezi mmoja uliopita nilipata nafasi ya kumtembelea dada yangu mmoja anayeishi mkoani nilipokua kikazi mkoani hapo. Tulikuwa hatujaonana kitambo sana hivyo alinisisitiza sana nifikie kwake kwani hatojisikia vizuri mie kuwa hotelini ilihali yeye yupo pale. Ilinibidi tu niende kishingo upande. Sasa nilichokikuta kwake ndicho kilichonishangaza.

Ameolewa na wana watoto watatu wazuri haswa. Dada yangu huyu alikuwa na kazi yake nzuri tuu na ni workaholic kama mimi, na kazi yake ni very demanding, safari haziishi. Hivyo hawa watoto walianza shule mapema sana ili angalau wazazi wapate muda wa kupiga kazi. Nakumbuka vilikuwa havina adabu, hata salamu ni hadi ubembeleze au watishiwe.

This time nimevikuta vimebadilika, wana adabu na utaratibu mzuri kweli wa maisha tangu wanaamka hadi kwenda kulala. Mtoto wa miaka mitano anaendesha sala ya familia hadi mtu mzima ananitoa nishai. In short niliwatamani na mfumo wao wa maisha kwa ujumla.

Nikamuuliza sister kulikoni haya mabadiliko? Ndipo akanieleza kuwa ilibidi afanye maamuzi magumu ya kuacha kazi ili asimamie vyema malezi ya watoto wake maana no one can do it better than her. Sasa nikamuuliza what if lolote likatokea na shem akatangulia(japo hatuombei)? Akanieleza its all sorted out and they have everything under controll.

Balaa lingine ni kwenye kupika,mwanamke anapika yule hadi unajilamba. Na ni lazima aandae chakula cha familia kila siku. Mwenzangu na mie kupika napika ila ni kile chakula utakula tu ili usife njaa.

To be honest aliniwazisha sana, nikawaza kama naweza kufanya hayo maamuzi sikujiona nikiweza. Maana its like am married to my work, sina muda kabisa hata huyu shemeji yenu ananivumilia tu.

Wanawake wenzangu je haya maamuzi mwaweza kuyafanya? Na wanaume mnasemaje, mwaweza kukubaliana na hili?
 
Hao ndo wanawake wa kale, amekosea tu kuja kwenye kizazi hiki cha nyoka! kwa asili kazi ya kulea watoto na familia ni ya wanawake, sasa hawa wa dot com kila kitu beki tatu, hadi baba wa nyumba anafuliwa nguo za ndani na beki tatu..

Angali hata wanyama, kazi ya majike na madume, naturally kulea ni majike! Nampongeza huyo dada kwa ujasiri huo. Kwani hiyo kazi ina faida gn km baadaye watoto hawana mwelekeo, wavuta bangi, mashoga etc etc...
 
Binafsi nimependa maamuzi yake amefanya maamuzi magum na sahihi maana wa dada wa siku hizi tunatamani kuoa lkn most of them they can't cook, no wash

Raha ya mke akupikie yani yeye ndio mtu wa kuku hudumia mume na mumewe naamin anafaidi sana
 
Mpigie makofi matatu dada yako kwa kufanya maamuzi magumu.Hiyo ndiyo inatakiwa kwa maisha ya sasa hasa ukizingatia waajiri wengi wanazidiwa na graduates wanaomaliza vyuo kila uchao duniani.

Hilo ni funzo kwako kwamba fikiria kujiajiri au kuajiri.Huo ndio ushauri wangu.Mwanamke kuacha kuajiriwa inawezekana na hakuna shida jipange
 
Lol
Hao ndo wanawake wa kale, amekosea tu kuja kwenye kizazi hiki cha nyoka! kwa asili kazi ya kulea watoto na familia ni ya wanawake, sasa hawa wa dot com kila kitu beki tatu, hadi baba wa nyumba anafuliwa nguo za ndani na beki tatu.. Angali hata wanyama, kazi ya majike na madume, naturally kulea ni majike! Nampongeza huyo dada kwa ujasiri huo. Kwani hiyo kazi ina faida gn km baadaye watoto hawana mwelekeo, wavuta bangi, mashoga etc etc...
 
Its a family business so nimeajiri pia. Ila bado nina kazi kubwa.
Mpigie makofi matatu dada yako kwa kufanya maamuzi magumu.Hiyo ndiyo inatakiwa kwa maisha ya sasa hasa ukizingatia waajiri wengi wanazidiwa na graduates wanaomaliza vyuo kila uchao duniani.Hilo ni funzo kwako kwamba fikiria kujiajiri au kuajiri.Huo ndio ushauri wangu.Mwanamke kuacha kuajiriwa inawezekana na hakuna shida jipange
 
Back
Top Bottom