Mwanamke ukijifanya kuzira, imekula kwako……………………………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke ukijifanya kuzira, imekula kwako……………………………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jan 31, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wanandoa wengi wanapogombana wananuna sana, hata kwa wiki nzima. Kila mmoja anataka kumwonesha mwenzie kwamba, amemkera. Sasa ni nani amemkera mwenzake basi? Ukweli ni kwamba kununa huku ni dalili kubwa kwamba wanandoa hawa kila mmoja anaamini yuko sahihi zaidi ya mwingine, kwa hiyo anataka kuonesha msimamo lakini inawezekana babisa kwamba, wanandoa wote, au mmoja kati yao, hataki kuambiwa jambo ambalo linamkera. Anataka kila wakati kusikia lile analolitaka yeye.

  Kwa hiyo kunyamaza au kuzira kuzungumza, ni aina a mgomo baridi kwake kuonesha kwamba, amekosewa au ameonewa, hata kama siyo kweli. Kati ya watu hao wawili, ni wazi kuna ambaye atajaribu kufungua milango ya mawsiliano na yule anayehisi kuonewa, ambaye ni huyu asiyetaka kuambiwa ukweli kuhusu udhaifu wake, atafunga Milango hiyo. Wanawake ndio ambao wanakabiliwa sana na tabia hii ya kuzira kuzungumza na huitumia njia hii kuonesha kwamba, hawajaridhishwa na kile kinachofanywa na waume zao. Lakini kwa bahati mbaya wanashindwa kujua kwamba kuzira kuzungumza kuna maana ya kuchukua mawe na kuyapanga kwenye njia ambayo mtu anataka kupitisha gari. Ni kufunga njia ya kuelekea kwenye kuelewana na mume.

  Ni jambo ambalo haliwezi kupingwa na ambalo ni lazima litokee ili ndoa ikue na kukomaa. Hili siyo lingine bali kukwaruzana kwa kawaida kati ya wapenzi. Bila kukwaruzana hakuna kukua kwa ndoa, hakuna kufahamiana kati ya wapenzi na hakuna kupanuka kimawasiliano kila mmoja kusema hisia zake kwa uhuru. Kama kugombana kwa aina fulani kumetokea, haina maana kwamba, wanandoa wanune, hapana. Kugombana kunapotokea hata kama hakujatafutiwa ufumbuzi, jambo la maana ni kwa wanandoa kuzungumza kama kawaida mambo mengine. Ajabu ni kwamba katika kuzungumza huku mambo mengine, wanajikuta wanazungumza na kile kilichowagombanisha pengine kukipatia ufumbuzi.


  Wanawake wanapaswa kujua kwamba, kimaumbile, wanaume ni wagumu sana kuanzisha mazungumzo baada ya wake zao kuzira. Ni wagumu kwa sababu, kimaumbile ni wababe na wanapenda kuona wakipewa hadhi ambayo wakati mwingine wala hawastahili. Kwa hali hiyo, mwanamke ndiye anayepaswa kuepuka kutumia njia hii ya kuzira kuzungumza, kama suluhu. Badala ya kuzira mwanamke anapaswa kumwonesha mwanaume kwamba, yeye hana kinyongo, amwoneshe kwamba, vurugu iliyotokea siyo kitu. Hata kama moyoni anajua kabisa kwamba, anamsanifu, kwa ubwege wa mwanaume kupenda sifa, naye ataanza kufungua mawasiliano.

  Kumbuka karibu kila mwanaume amefundishwa kuwa mwanamke akimnyenyekea na kumbembeleza kwa kuonesha kwamba, yeye (mwanaume) ndiye anayepaswa kupewa heshima peke yake, hujisikia vizuri na kubabaika. Kwa nini wanaume wengi ndio wanaoacha ndoa zao na kukimbilia nyumba ndogo? Pamoja na sababu nyingine, lakini pia ni kuonesha kwamba, wao ni wafalme!

  Kauli kama, 'si alijifanya kuzira, nimemchunia hadi mwenyewe kaanza kujipendekeza, anacheza na mimi!' Ni kauli za kawaida sana kwa wanaume pale mke anapoamua kufungua milango ya mawasiliano baada ya kuzira kwa siku kadhaa bila mume kuonesha kujali.Mara nyingi mke anapozira mwisho wa siku mume huja kuwa mshindi, kwa sababu kwao kunyenyekea ni msamiati mgumu na kunakuwa na maana ya kutawaliwa na mwanamke.
   
 2. Tegelezeni

  Tegelezeni JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 31, 2009
  Messages: 268
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kumbeee, nishajua sasa, akijifanya kuzira, najitia kichwa ngumu, nmemdekeza sana huyu mke wangu. Ahsante mkuu, sikujua kama hii mbinu inalipa
   
 3. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ngoja nikioa ntajaribu kuwa makini ktk kulichunguza hilo, bt mkuu uko sawa kabisha juu ya nani atakae umia kwa kununa mwanamke ni yeye mwenyewe ndo muhanga mkubwa.
   
 4. n

  ngwana ongwa doi Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kanuni ya Mungu mwanaume ampende mkewe na mwanamke amtii mumewe,tofoauti na hapo ni songombingo lisiloisha na mama Ngina.
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,577
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi bwana nakuja ,
   
 6. T

  Tata JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,739
  Likes Received: 658
  Trophy Points: 280
  Hiki kipindi cha kuzira huwa kina utulivu sana.
   
Loading...