Mwanamke raia wa China azirai baada ya kuvunja bangili ya dola 44,000

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,319
3,912
p0575vwl.jpg

Mtalii huyo kutoka mkoa wa Jiangxi, alikuwa akijaribu kuvaa bangili hiyo kwenye duka moja lililo mkoa wa Yunnam karibu na mpaka na Myanmar.
Mwanamke mmoja raia wa China alizirai akiwa kwenye duka la kuuza vito vya thamani baada ya kuvunja kimakosa bangili ghali ya thamani ya dola 44,000

Mtalii huyo kutoka mkoa wa Jiangxi, alikuwa akijaribu kuvaa bangili hiyo kwenye duka moja lililo mkoa wa Yunnam karibu na mpaka na Myanmar.

Alipoambiwa thamani na bangili hiyo aliifua kwa haraka lakini ikaanguka kimakosa,

Hakuna makubaliano yameafikiwa kuhusu vile bangili hiyo itafidiwa.,

Wafanyakazi wa duka walijaribu kumtuliza baada ya kisa lakini mara alianza kutokwa na jasho na kisha akazirai.

_96722425_7734dd64-c163-4c42-ad1a-3028267159f2.jpg
Haki miliki ya pichaCHINA STATE MEDIA
Image captionMtalii huyo kutoka mkoa wa Jiangxi, alikuwa akijaribu kuvaa bangili hiyo kwenye duka moja lililo mkoa wa Yunnam karibu na mpaka na Myanmar.
Alipata nafuu wakati wateja wangine ambao walikuja kumsaidia walipomfinya pua lake.

Wafanyakazi wa duka walimwambia alipe dola 25,000 ili kutatua suala hilo lakini akasema alikuwa na dola 1,500 tu.

Polisi walishindwa kushawishi pande zote kuafikia makubaliano na suala hilo huenda likaelekea mahakamani.

Chama kimoja cha kuuza vito vya thamani kilisema kuwa bangili hiyo ni ya thamani ya dola 26,000.

Chanzo: BBC

======

Hiyo bangili kwa pesa ya kitanzania ni kama sh. Million 99
Lakini mtu mwingine ukiiangalia kwa haraka haraka unaweza kuona kwa bei yake haizidi sh. 15000
 
Kuna jamaa mmoja hivi vya kuenda sehemu na kujifanya anajua kila kitu
Vilisha mtokeaga puani.

Yeye alishazoega saluni za mikoani kunyolea nywele ni sh.1000 ikizidi sana sh. 2000 siku moja akaenda dar akaikuta saluni moja nzuri sana akajua bei ni zile zile za buku au buku mbili.

Akashanga huduma anazo pewa pale saluni ni nyingi isivyo kawaida yeye kwa akili yake akajua vile vyote wanafanya ni ukarimu tu wa kuwavutia wateja ni sawa ukienda mgahawani ukiagiza wali nyama lazima watakuwekea maharage mboga za majani nk. Ila kwa bei ile ile ili na kesho uje. kumbe wenzake wakimuuliza tukuwekee na kitu flani akisema ndio kule wanaandika.

Na mwisho wa siku akaja kupewa bili ya sh. 40000 na mfukoni alibakiwa na 15000 tu alijaribu kujitetea kwamba jamani mm huu mji ni mgeni nk.

Hiyo pesa walichukua ila walimtukana sana.
 
nimeipenda hii
 
d86ffd11633dfd8bdb72f03093abf797.jpg
3240578eb75dbb308ca40ba050dc2b71.jpg
c1435a43f545c765791c4b487a41a952.jpg

Hiyo bangili kwa pesa ya kitanzania ni kama sh. Million 99
Lakini mtu mwingine ukiiangalia kwa haraka haraka unaweza kuona kwa bei yake haizidi sh. 15000

Only in CHINA....hehehe...mh...kwa gharama hiyo ni lazima ingekuwa na warranty...hata kama ni kito iweje iwe ni rahisi kuharibika hivo...hahahhaha.....ndio maana imebaki kuwa trending news.... Business is Business...kama hiyo ndio price tag yake HAMNA NAMNA....
 
Kweli kwa hiyo bei ni dhuruma.
 
Sasa bangili la pesa nyingi namna hiyo linakuwaje na ubora hafifu namna hiyo? Thamani ya pesa mbona hailingani na ubora wa bangili?
 
Hiyo hata kama una hela sio ya kununua na matoto yetu matundu ya kiswahili utakuwa unazima kila siku kisa bangili.
 
Back
Top Bottom