Mwanamke peke yake hawezi kumkuza mtoto wa kiume kuwa mwanaume

umeandika uharao, kwani mama Diamond kamleleaje Diamond?

Mama Mwana FA kamleleaje FA?

Mama Dreki msanii mashuhuri Marekani, kamleleaje Dreki?

na wengineo kama hao ambao wamelelewa na mama na sio baba, mbona wako freshi tuu

Nilowataja hapo ni baadhi ya wasanii wachache sijaweka wote.

Pia kuna matajiri wakubwa wasiowajua baba zao, ila wamelelewa na mama zao tuu. Mbona wao wako freshi.

Kama hujui kitu sikuingine usijaribu kuandika uharo.

Umeongea na mihemko. Vijana wengi mtaaji wa hivyo wamelewa na mama. Nina ndug wengi ambao baada ya baba zao kufa mama zao hawkauwa na wanaume tena.
 
I finally understand for a woman isn't easy tryna raise a man ~ 2 pac
 
Wanaume waliolelewa na single parent yaani mama peke yake huwa wanapwaya sana kwenye ndoa..wanashindwa kutenganisha space ya Mama yake na space ya mke wake . Mama anageuka mshauri mkuu huku mke akitupwa pembeni.

Hawajiqmini when comes to family decision making, mama yake anageuka mwamuzi ya mambo mengi ya kiuchumi hasa hasa.

Wanawake wengi huishia kuvunja ndoa hizi maana wanaishi kwa shida bila uthamani wa ndoa.
 
Kama hao ndio mfano mzuri kwako, utakuwa umelelewa na mama ama bibi wewe. Kama hiyo ilitokea kwa sababu ya kufiwa, pole sana.
umeandika uharao, kwani mama Diamond kamleleaje Diamond?

Mama Mwana FA kamleleaje FA?

Mama Dreki msanii mashuhuri Marekani, kamleleaje Dreki?

na wengineo kama hao ambao wamelelewa na mama na sio baba, mbona wako freshi tuu

Nilowataja hapo ni baadhi ya wasanii wachache sijaweka wote.

Pia kuna matajiri wakubwa wasiowajua baba zao, ila wamelelewa na mama zao tuu. Mbona wao wako freshi.

Kama hujui kitu sikuingine usijaribu kuandika uharo.
 
PAKA JIKE HAWEZI KUKUZA SIMBA DUME

Mwanamke pekee hawezi kumkuza mtoto wake wa kiume kwenye kizazi hiki kipya, hii haijalishi mwanamke kaelimik kiasi gani, cheo, pesa, n.k. itakuwa ni ngumu sana, ponea ya mtoto labda awe na wajomba, ndugu wa kiume, n.k wenye muda nae, pia watoto wengine wanabahatika kuwa na watu wa mitaani sahihi ambao hugeuka kuwa kama baba kimtindo, lakini bado nafasi ya baba ni nzito.

Baba ni muhimu sana katika malezi ya mtoto wa kiume, uwepo wake pekee ndani ya nyumba hauna uzito, baba inabidi awe na jukumu la kukuza watoto wa kiume waje wanaume na sio watu wa kiume.

DISCIPLINE:

Mtoto wa kiume humuona mama yake kama rafiki yake tu ambae hata wakikosana anajua kuna madhara kidogo sana, atafinywa finya labda au atakaripiwa tu, binafsi mama yangu hata anichape nilikuwa namatania "hakijaingia", rafiki yangu flani akianza kuchapwa alikuwa anavunja vunja kiboko.

kwa baba ni tofauti kabisa, mtoto akikosea halafu aambiwe amsubiri baba yake wamalizane anajua tayari mziki wake, sio lazima kipigo kama wengi wanavyodhani lakini hata baba akikaa na mtoto wake kumpa darasa huwa kuna kitu kizito sana kinachomfanya mtoto ajihisi kweli kakosea na atajisikia vibaya, kiukweli huwa yanakuwa ni maumivu.

binafsi baba alikuwa ananipa dozi ya viboko mara chache sana na hapo ni kwamba nimekuwa mtukutu sana, lakini yale maneno aliyokuwa akinihusia kwenye makosa niliyofanya yalikuwa mazito sana, kuna muda niliwahi kulala saa tisa usiku nawaza tu darasa chungu alilonipa bila hata kuinua kiboko.... hii hali inamwingizia sana displini mtoto kujua kutii sheria hata za mama yake.

KUKABILIANA NA MAISHA YA WANAUME

Hapa utake usitake maisha ya wanaume utakutana na wanaume wenzako wakorofi ama waonezi, baba atamfundisha mtoto jinsi ya ku deal na hizi hali aidha kujua kupigana, kuwa na marafiki wa kum back up, n.k. mama yake atakuwa anaenda kulalamika mtoto kapigwa ila mzee wake anamuonesha mbinu.


ELIMU YA KUJITEGEMEA

Baba anaweza kuwa mfugaji, mkulima, seremala, fundi ujenzi, fundi mabommba, n.k hapa anaweza kumfundisha mtoto wake haya mambo ili hata akiondoka kuwe na mtu wa kuweka ugali mezani kihalali, mtoto akikosa hizi mbinu kuna uwezekano mkubwa akaanza kukaba watu.

MASULINITY (TABIA ZA KIUME)

Uwepo wa baba pia unamfanya mtoto wa kiume aweze kukopi tabia kibao za kiume, mzee anaweza kuwa mpenzi wa kutazama kwenye tv mieleka na muvi za ngumi, hapa mtoto nae anajijenga taia za ujasiri, kupenda mazoezi , n.k. hata pale mtoto anapoona mzee ana upinde ama rungu chumbani kwake hii inamfanya ajue mapema kwamba baba ndie mlinzi wa familia,

mtoto akikaa sana na mama yake si ajabu anaweza kuanza kupenda taarab, kujipiga make up, n.k,

INAENDELEA.............

Andiko safi kabisa hata likiishia hapa
 
Mleta mada hongera sana! Uliyoandika ni kweli kabisa! Ila humu ndani kuna baadhi ya vijana ufahamu wao ni mdogo hawawezi kuelewa.
 
Andiko la ukweli na lina uhalisia wa maisha tunayo ishi. Wanawake single mama wengi sana wanaharibu swatoto wa kiume. Dogo anakua fala fala tu maisha yake yote.. u know my mommy this .... my mommy that.. faken kabisa hao.
 
Wazazi wote ni sawa...
Ni kweli wazazi ni sawa kwa ustahili wa heshima na upendo…
ila naungana sana na mleta mada: pengo la baba haliwezi zibwa na mama kikamilifu (especialy kwa malezi ya mtoto wa kiume)
Utafuzwa vipi na mama kuwa baba/mwanaume bora wakati mama hajawahi hata kuwa mvulana!
 
Duu mkuu wakati Niko o level pale songea boy's Kuna mtoto wa mwalimu wetu alikuja ANALIA amepigwa huko alikokuwa anacheza babake kamwambia mama mpe chakula ale halafu akapigane wamepiga sababu ya njaa
 
Andiko la ukweli na lina uhalisia wa maisha tunayo ishi. Wanawake single mama wengi sana wanaharibu swatoto wa kiume. Dogo anakua fala fala tu maisha yake yote.. u know my mommy this .... my mommy that.. faken kabisa hao. cheki toto la uwoya tayari liko wasted
 
Ni kweli wazazi ni sawa kwa ustahili wa heshima na upendo…
ila naungana sana na mleta mada: pengo la baba haliwezi zibwa na mama kikamilifu (especialy kwa malezi ya mtoto wa kiume)
Utafuzwa vipi na mama kuwa baba/mwanaume bora wakati mama hajawahi hata kuwa mvulana!

Matatizo mengi kwenye jamii ya sasa yanasababishwa na Fatherlessness na kuwa na mzazi wa kiume kwenye familia haimaanishi una baba…
yamkini ni akawa “Sperm doner” tu. Baba ni zaidi ya kuwa na jinsia ya kiume kwani nilivyomwelewa jamaa mwenye uzi wake..
 
Andiko la ukweli na lina uhalisia wa maisha tunayo ishi. Wanawake single mama wengi sana wanaharibu swatoto wa kiume. Dogo anakua fala fala tu maisha yake yote.. u know my mommy this .... my mommy that.. faken kabisa hao.
Usiseme wanawake wanawaharibu hao watoto was kiume jiulize hao baba was kuwalea hao watoto wako wapi???na usitoe jibu la kuwa wamekufa nop find another genuine answer as a man yourself
 
sijawahi kukubali mtt angu akae na mama ake angalau kwa week 2 bila mm
 
Ni kweli na ndiyo maana unaona masingo maza kibao wanatusakizia watoto wao waliozaa na vibaka kwa ajili ya tamaa zao za kijinga ili tuwe father figure kwao.
 
Back
Top Bottom