Mwanamke Pakistan aua watu 15 katika jaribio la kumuua mmewe kwa sumu

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,260
9,704
Mwanamke ajulikanaye kama Asiya Bibi anashitakiwa kwa kosa la mauaji ya watu 15, huko Pakstan.

Mwanamama huyo, ambaye alilenga kumuua mmewe baada ya kulazimishwa kuolewa na mwanaume asiyempenda huku akikataliwa kuolewa na mpenzi wake aliyempenda.

Alijaribu kutoroka kutoka kwa mmewe ikashindikana ndipo akapata wazo la kumuua kwa njia ya kumwekea sumu kwenye maziwa, ila bahati ni kwamba hayo maziwa mumewe hakuyanywa bali wakayatumia kutengenezea mtindi ambao ndugu na wazazi wa mmewe waliutumia siku ya Ijumaa.

Baada ya kutumia mtindi huo, waliugua ghafla na kukimbizwa hospitali, ambapo 11 walifariki siku hiyo hiyo, wawili walifariki jumamosi.

Mpaka sasa wamekwisha kufa watu 15 kati ya 28 waliokunywa mtindi huo akiwemo mtoto wa miaka saba.

Polisi inamshikilia Asiya pamoja na shangazi yake na mpenzi wake kama washirika katika tukio hilo.

----------
A woman who allegedly tried to kill her husband by giving him poisoned milk ended up killing him and 14 members of his family, police in Pakistan have said.

Officers in Punjab province said Asiya Bibi's husband initially failed to drink the milk and it was then turned into a lassi - a South Asian yogurt drink - and served to the man's family.

Investigators allege Bibi set out to poison her husband after she was forced by her family into an arranged marriage in September.

Bibi has been charged with murder along with two others, senior police official Owais Ahmad told reporters.

The Geo News website said 15 have so far died, including Bibi's husband and a seven-year-old girl, while a further 12 are being treated in hospital after the incident in rural Alipur Tehsil.

Mr Ahmad added: "Police have arrested Asiya Bibi, a man and his aunt for being accomplices and charged them with murder."

He said the man was allegedly Bibi's lover and his aunt helped orchestrate the murder plot.

Bibi has appeared in court and denied all the allegations against her when presented to the media, Geo News reported.

Forced and under-age marriages are common in Pakistan, particularly in rural and poor regions, where women are regarded as having fewer rights.

Source: Wife's 'milk murder plot' accidentally kills 15 in Pakistan
 
hayo maziwa yalikuwa kiasi gani? huyo jamaaa alikuwa anakunywa ndoo nini? maana from mtu mmmoja to watu 28 sio mchezo
 
hayo maziwa yalikuwa kiasi gani? huyo jamaaa alikuwa anakunywa ndoo nini? maana from mtu mmmoja to watu 28 sio mchezo
Ilikuwa sumu imewekwa kwenye glass mmoja ya mtindi kwa ajili ya mumewe, ila hakunywa hayo maziwa badala yake yakamwangwa kwenye maziwa fresh ili kutengeneza maziwa mtindi mingine.
Si unajua ukichukua mtindi ukamwaga kwenye maziwa fresh baada ya muda nayo yanageuka mtindi.
 
ok kumbe mtindi unatengenezwa hivo eeh
 
Mwanamke ajulikanaye kama Asiya Bibi anashitakiwa kwa kosa la mauaji ya watu 15, huko Pakstan.
Mwanamama huyo, ambaye alilenga kumuua mmewe baada ya kulazimishwa kuolewa na mwanaume asiyempenda huku akikataliwa kuolewa na mpenzi wake aliyempenda.
Alijaribu kutoroka kutoka kwa mmewe ikashindikana ndipo akapata wazo la kumuua kwa njia ya kumwekea sumu kwenye maziwa, ila bahati ni kwamba hayo maziwa mumewe hakuyanywa bali wakayatumia kutengenezea mtindi ambao ndugu na wazazi wa mmewe waliutumia siku ya Ijumaa.
Baada ya kutumia mtindi huo, waliugua ghafla na kukimbizwa hospitali, ambapo 11 walifariki siku hiyo hiyo, wawili walifariki jumamosi.
Mpaka sasa wamekwisha kufa watu 15 kati ya 28 waliokunywa mtindi huo akiwemo mtoto wa miaka saba.
Polisi inamshikilia Asiya pamoja na shangazi yake na mpenzi wake kama washirika katika tukio hilo.
Huyo kichwa chake ni halali yao
 
halafu dogo una akili kweli hivi sumu na maziwa inakuaje?
Siyo kweli kwamba maziwa ni dawa ya kila sumu, ingekuwa hivyo mtu akikimbiwa hsp kala sumu angekuwa anapewa maziwa badala ya kugongwa drip za maana.
Maziea yanasaidia kwenye sumu jamii flani tu.
 
Huyu ni muongo. Mimi nipo Pakstan ila sijasikia hii kitu ila namfahamu Asia Bibi aliyehukumiwa kunyongwa kwa kumkashifu Mtume na ambaye hadi leo hajanyongwa Asia Bibi has spent more than 3,000 days in prison for blasphemy ila kama anasema hii Pakistan bride accidentally poisons 13 family members in failed bid to kill husband

2250c477711786c340d80d9221f1be60.jpg

e2fe24ad10865a7523e6e17a9bcefc5c.jpg

Haya bishana na RT, kuwa Pakistan hakukufanyi ujue kila kitu unaweza kuwa huko unauza kashata.
Hata kuwa Tanzania hakukufanyi uwe na habari za kila kitu.
Nimekuwekea screenshot ya pili jina anaitwa Asiya Bibi sasa sijui unabisha nini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom