Mwanamke ni sawa na jua umuhimu wake ni pale linapokosekana anahitaji upendo na heshima tu!

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
FB_IMG_1509105245741.jpg


Mwanamke ni kama Jua unaweza usione umuhimu wake, yaani kila siku unaenda mjini jua lipo tu, unaliangalia lakini huangalii umuhimu wake kwako.

Wakati mwingine likiwa kali unaanza kulalamika kuwa linachoma na lina kera. Lakini ukitafakari kidogo tu utajua kuwa bila jua maisha yasingekuwepo.

Hembu chukulia mfano mchana kungekuwa giza tu kama usiku nini kingetokea? Chakula tunachokula ni kwasababu ya Jua, mvua ikinyesha sana mafuriko yakitokea tunatamani jua, kwenye baridi tunatamani pia jua, hatuliwazii kwasababu lipo tu na linatimiza majukumu yake kimya kimya bila kelele.

Hiyo ni sawa na mwanamke, ukishaoa kuna mambo ambayo mwanamke huyafanya na baada ya muda unaanza kuyaona ya kawaida kawaida, chakula kinakuwa mezani kila siku hujui kinapikwaje na vyombo vinaoshwaje, anabeba mimba na watoto wanazaliwa hujui maumivu aliyoyapata lakini unatabasmu na kucheka ukijisifia watoto wangu na hata mkigombana unasema niachie wanangu wewe nenda tu tafikili unajua maumivu aloyapata kipindi anawaleta duniani ao watoto.

Watoto wanaumwa mpaka wanapona hujui hata wameponaje, wanalia usiku hujui hata nani alikuwa anawabembeleza, ukirudi unakuta nguo safi chumba kisafi hutoi hata shukurani kwakuwa ushasahau kua kuna mtu anasafisha siwe safi muda wote.

Na anafanya vitu vyote hivyo kama Jua bila kelele lakini wewe ukitoa elfu mbili ya sukari utamnyaanyasia mpaka ndugu zake kuwa unawalisha wewe!

Hembu siku aondoke akuachie hao watoto unaojisifia kila siku kuwa ni wakwako na kumuambia hajaja na kitu, uanze kuwapikia na kuwaandaa kwenda shule, ufue nguo zao na zako.

Unaweza kuajiri mfanyakazi lakini hawezi kufanya hata nusu ya kile anachokufanyia mkeo, kwani yeye atafanya kama kazi lakini mkeo anafanya kwa mapenzi, hahitaji umlipe chochote zaidi ya kutimiza majukumu yako na kumheshimu kama mke katika maisha yenu.

Vuta picha umeamka mkeo hayupo, watoto wanataka kuogeshwa kunywa chai na kwenda shule, hapo unatakiwa kuwahi kazini na mchana watoto wale! Mheshimu sana mkeo kuna mambo mengi ambayo anayafanya ukiambiwa uyafanye wewe utachanganyikiwa na mkeo huyafanya kwa upendo.

Mwanamke anachohitaji kwa mume ni upendo na heshima tu. Mhudumie, mpe upendo, muheshimu na muonyeshe kuwa kwako ana umuhimu mkubwa, mfanye mkeo atabasamu kila mara na familia nzima itatabasamu.
 
tatizo tukiwaheshima mnahisi mmetyshika.


nawahimiza wanaume wenzangu tuendeleza utemi, akizingua anatembea kinashuka chombo kipya.
 
Mara nyingi wanaume wengi wamekuwa wanatamani wawe hivyo ila hukatishwa tamaa na wanawake wapumbavu hivyo kujikuta akilini alishajiwekea kuwa hatorudia tena kosa.

Ata anapokuja kukutana na mwanamke mwenye mapenzi ya kweli anakuwa amejitune kutokana na historia aliyopitia na hapo panakuwa na kuviziana kwingi.
 
Kiukwel mwanaume unaweza ukjituma kumpenda mwanamke kwa dhati kabisa ila akishajua unamnyenyekea sana aisee anatumia nafasi uliyompa kukukosea heshima...mpk tunalazimila kuendeleza utemi yaan hawa viumbe mm nashindwa kujua wanapenda MTU uweje maana ukiwapenda sana na kuwaheshimu huwa wanakuona bwege tu na kukuletea dharau tu duuuh....
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom