Mwanamke ni lazima apigwe na mume, “lau kidogo”…………..!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Wengi wetu tumekulia kwenye mazingira ambapo mijisifu na majidai yetu tukiwa vijana na balehe ikiwa imeshika kasi, sifa mojawapo ya kuonesha ushababi wetu ilikuwa ni jinsi tulivyoweza kumshikisha adabu mtoto wa kike. Tumekulia kwenye mazingira ambayo mwanamke hapaswi kujibu wakati mwanaume anaongea. Na pia tumekulia kwenye mazingira ambapo kusikia mwanamke kapigwa au kubakwa kwa staili ya "niangusage" au "chagulaga" ni jambo la kawaida na pengine sifa kwa aliyemfanyia hivyo mwanamke huyo.

Kwa bahati mbaya kuna wale ambao wamelelewa na kukulia kwenye maeneo ambapo tangu kale mwanamke ni kama bidhaa, akishalipiwa ng'ombe kadhaa anakuwa amenunuliwa. Huko mwanamke hatakiwi kumjibu mume, hatakiwi kujitetea kwa lolote. Kwa bahati mbaya na mwanamke naye amelelewa na kukulia kwenye mazingira yenye kumwambia kwamba, hatakiwi kumjibu mume na pengine kupigwa ni dalili ya upendo.

Uwezekano ni mkubwa sana kwamba, kuna watu wa idadi ya kutosha hapa nchini ambao wanaamini kwamba mke ni lazima apigwe kila anapokosea. Watu hawa huwapiga kweli wake zao na pia wako tayari kuwapiga hata wasio wake zao, mradi ni wanawake. Vilevile ingawa siyo kwa idadi kubwa, wapo wanawake wanaoamini kwamba kupigwa na mume ni muhimu au lazima na siyo jambo la kuudhi sana.

Hawa walizoea kuwaona mama zao wakipigwa na baba zao na kusema, "hewala mume wangu," hivyo wakaamini kwamba, kupigwa ni sehemu muhimu katika kukamilisha ndoa bora na imara. Wengine walizoea kuwaona mama zao wakilalamika kila siku kwamba, ni afadhali kupigwa kuliko ghubu. Walipokuwa wakubwa wakaamini kwamba, kupigwa ni adhabu bora na nyepesi zaidi kutoka kwa mume.

Lakini ukweli utaendelea kubaki kwamba kama kuna wanaoamini kuwa mapenzi au uhusiano wao utanona kwa mwanamke kukubali kupigwa kila akikosa, mimi nadhani wanahitaji kutembea safari ndefu sana kabla hawajaufikia ustaarabu.

Na labda wengine wako humu humu JF.
 
Kuna kundi la wengine hawajawahi kusikia hata hiyo chagulaga

Siku mwanamme akinipiga ndo siku ya mwisho kwake kugusa ngozi yangu...ever

Siku hizi, tunawapiga kisha tunawapigia magoti kuwabembeleza na kulia kwa majuto tukisema......... "I was out of control"..... I am so sorry HONEY, Shetani alinipitia Wallahi.................

Na nyie mnatusamehe na maisha yanaendelea kama kawaida..........................LOL
 
unyanyue tu jikono lako unipige? loh!!!!!!! walaaaaahiiiii kama sijakuchana wewe chochote kitakachokuwepo karibu yangu kitakuhusu!!!!!!!!!

ila sometimes wanawake nao wanayataka haya mambo, mkiwa boyfrind na girlfriend jitu linakupiga unavumilia ati atabadilika? thubutuuuuuuuu akikuoa atakudunda mpaka ukimbie na chu*i...!!!!!! mwanaume abusive namna hii anaonekana toka mwanzo, lakini sijui ndo kutaka kuolewa au nini wanakubaliana tu na mazagazaga ya ajabu........................
:A S 13:
 
halafu mtambuzi ujue mwanamke hapigwi ngumi.....
hapigwi kwa khanga; ina maneno.......................Mwanamke anapigwa na KITENGE CHA WAX, na wanaume wa siku hizi wanampiga mwanamke na RAV 4



shaurilo................................
:wink2:
 
Mwanaume anyanyuaye mkono kumpiga mkewe ni mjinga.

Kama una miguvu yako nyanyua mkono upigane na mwanaume mwenzio. Ukipukuchuliwa meno uje bado hujaiva kuwa bondia.

Mke hupigwa kwa maneno kisha tenge la wax bana.
 
halafu mtambuzi ujue mwanamke hapigwi ngumi.....
hapigwi kwa khanga; ina maneno.......................Mwanamke anapigwa na KITENGE CHA WAX, na wanaume wa siku hizi wanampiga mwanamke na RAV 4



shaurilo................................
:wink2:
Ndo maana Liyumba aliwapiga sana na madude mekundu. Chezeya kupigwa na gari wewe......:violin:
 
Kweli sio ustaarabu kumwadhibu mke kwa jinsi hiyo hata kama mke mwenyewe ni CHIRIKU/MAPEPE,yaani wewe unataka kumwelewesha lakini wewe una maneno mawili yeye ana kumi na tano na hawezi kunyamaza mpaka atoe machozi.Psychological punishment ni njia nzuri ya kudeal na wanawake wa aina hii.
 
Kweli sio ustaarabu kumwadhibu mke kwa jinsi hiyo hata kama mke mwenyewe ni CHIRIKU/MAPEPE,yaani wewe unataka kumwelewesha lakini wewe una maneno mawili yeye ana kumi na tano na hawezi kunyamaza mpaka atoe machozi.Psychological punishment ni njia nzuri ya kudeal na wanawake wa aina hii.

Mimi nadhani wewe umezungumzia reality zaidi ya wachangiaji wengi waliotangulia. Asilimia kubwa ya wengi wetu bana tunaishi kwenye mfumo ule ule wa zamani, haya mambo ya Beijing kwetu bado kushika hatamu- sisi huku kwetu (ambako tunaambiwa ni 80%) kibano kipo palepale!!!
 
Ndo maana Liyumba aliwapiga sana na madude mekundu. Chezeya kupigwa na gari wewe......:violin:
:sleepy:
Asprin acha bwana, liyumba alikuwa anahonga, wakishapeana kamchezo.........mambo ya barter{spelling?} trade, ila hapa ni kwa mtu na mpenzi wake au wanandoa, ambao hawafanyi biashara ya kubadilishana bidhaa au huduma.........:redface:
 
Mimi nilioa nikiwa kijana sana at 26 na wife alikuwa 21, tulikutana chuoni, baada tuu ya kumaliza ni ndoa!. Changamoto za ujana zilipelekea wife kupokea kisago!, that was then!.

Kuna wanawake wanafanya visa ambavyo unajua wazi anatamani kula kichapo!.

Pia kuna kuna wanawake wa maeneo fulani, asipopigwa, anajiona hapendwi!. Hivyo atakufanyia visa ili kukupima wivu, akigundua humuonei wivu, ananyong'onyea, kwake mapenzi ni pamoja na kisago.

Ila pia kuna type ya wanawanawake wana matatizo ya kisaokolijia yanayoitwa "masochisim", wahusika wanaitwa "macho men" "macho women" hawa ni wale mnaokubaliana, mnakwenda mnapokwenda, mnaingia room, unafunga mlango, halafu anakukatalia, mpaka amlazimishe ndipo nguo zinavuliwa ili tuu kuzuia sizichanike, baada ya hapo miguu hufungwa!, mpaka utembeze kisago kama unabaka ndipo unafunguliwa njia!. Kumbe hizo fujo kwa mwenzako ndio anapata gratification!. Ndio maana kuna watu hutaka wapigwe, wafungwe pingu, wateswe, wabake ndipo wafike na ndio maana kuna wengine hung'ata hata kukutoa damu!.

Kwa Wasukuma wa asili, ile ngoma ya chagulaga, ni ubakaji, kuna wanawake wengi wanabakwa na waume zao au wapenzi wao.

Hawa wanawake wa kisasa "easy come easy go", ndio wanaokosa uvumilivu na kupelekea ndoa za siku hizi kuvunjika kirahisi, kosa dogo tuu, mama ana fungasha!. Familia nyingi za kiafrikla za kizamani, mama zetu wamechezea sana vichapo na ndio zimesimama!.

Hata mimi siku hizi tumekuwa watu wazima, sithubutu hata kunyanyulia mkono!.

Paskali
 
Kwa vijijini, haya mambo ya mwanamke kupigwa bado yapo, ila kwa mjini wengi kwa sasa wamestaarabika. Ila tuko pamoja mkuu na asante kutukumbusha kuwa hatupaswi kuwadunda wake zetu!
 
Kuna kundi la wengine hawajawahi kusikia hata hiyo chagulaga

Siku mwanamme akinipiga ndo siku ya mwisho kwake kugusa ngozi yangu...ever

Heeeeeh!!!! Basi inabidi uwe na utii mkubwa sana.

Ni kweli kupiga siyo issue wala muafaka wa matatizo, zipo njia nyingi mbadala za kusuluhisha ikiwemo kuachana ikibidi.
 
Ukweli ni kwamba ukitaka kujua mwanamke ana upendo wa dhati kwako siku moja jifanye unataka mpiga, au jaribu kumpiga hata kofi halafu angalia 'REACTION' yake kwako..

Ukimuona na yeye anakuja juu anataka kupigana na wewe huyo hakufai..!!!
 
Hawa wanawake wa kisasa "easy come easy go", ndio wanaokosa uvumilivu na kupelekea ndoa za siku hizi kuvunjika kirahisi, kosa dogo tuu, mama ana fungasha!. Familia nyingi za kiafrikla za kizamani, mama zetu wamechezea sana vichapo na ndio zimesimama!.

Hizi ni dharau na kujaza wanawake ujinga. Kuwa akubali kichapo kwa sana kwa kuwa anataka kusimamisha ndoa
 
Back
Top Bottom