Mwanamke ni Kusikilizwa!SHOST | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke ni Kusikilizwa!SHOST

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Nov 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,694
  Trophy Points: 280
  Mwanamke ni Kusikilizwa!  [​IMG] Mashitaka mengi tunayopata wanaume kutoka kwa wake zetu ni kwamba;
  “Huwa hatuwasilikizi na pia hatuwajali”

  Kumsikiliza mwanamke anapoongea ni pamoja na kuachana na kile ulikuwa unafanya, concentrate kwenye kile anaongea, kusikiliza hisia zake zinaongelea kitu gani na si kile mdomo unaongea tu.

  Wanaume tunahitaji kufahamu kwamba wanawake mara nyingi huongelea matatizo yao kwa maana ya kuwa karibu na sisi na kupata ahueni kutokana na matatizo yanayaowapata, si lazima mwanaume kuanza kutoa solution ya matatizo anakwambia.

  Kama tulivyosema huko nyuma kwamba mwanamke akipata matatizo hutafuta mtu maalumu wa kuongea naye, kumshirikisha hisia zake na kile kitendo cha kuongea humpa ahueni (relief) hivyo basi mwanaume kazi kubwa ni kumsikiliza na zaidi sana kuhakikisha anafahamu kwamba unamsikiliza.

  MFANO
  Mariamu anarudi nyumbani akiwa hoi na kazi pamoja na kusumbuliwa na bosi wake.

  Anaporudi home anajisikia ni vizuri kuongea na mumewe.
  Fikiria Mariam ana wanaume wawili mmoja wa kweli (James) na wa pili ni kwa ajili ya kutufanye tuelewe mfano (Kelvin).
  Unadhani ni mume yupi kati ya James na Kelvin atakuwa amempa ahueni kwa matatizo yake na pia atakuwa alikuwa anamsikiliza?

  Mariam: Kazi yangu ni ngumu sana hadi nakosa muda wa kupumzika!
  James: Kwa nini usiache hiyo kazi na tafuta kazi nyingine ambayo utakuwa na muda.
  Kelvin: Ooh! Pole sana inaonekana leo ulikuwa na siku ngumu sana mke wangu!

  Mariamu: Yaani siamini nimeshindwa kumpigia simu Shangazi leo!
  James: Usihofu atakuelewa, si anajua upo busy.
  Kelvin: Ooh Pole sana mke wangu, unajua kupenda wewe ndo maana nakupenda!

  Mariamu: Unajua shangazi ana mapito magumu sana so ananihitaji kuongea naye:
  James: Una wasiwasi mno na wewe, kwa nini unajisumbua wakati upo busy na kazi yako.
  Kelvin: Pole sana najua leo umechoka, sogea basi nikukumbatie nimekumis sana leo.
  (Mariam na Kelvin wanakumbatiana na Mariam ana relax)

  NB: Mariam anakasirika na anamwambia James siku zote hunisikilizi na hunijali.
  Pia anamwambia Kelvin:
  "Kila siku napenda sana kuongea na wewe, unanifanya kuwa mtu wa furaha, asante sana kwa kunisikiliza, najisikia raha."

  Ukweli ni kwamba James alikuwa anasikiliza, lakini kwa lugha ya mwanamke alikuwa hasikilizi kwa kuwa alikuwa anajitahidi kutoa solution kwa yale alikuwa mkewe Mariam anamwambia.
  Kwa upande mwingine, Kelvin alikuwa anasikiliza kwa sababu alikuwa anaongea lugha ambayo mwanamke anaielewa na anaitaka na alikuwa anampa kile mwanamke anahitaji.

  Je, wewe ni James au Kelvin?
   
 2. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mi Ni eRRy84! na wewe?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mi naweza nikawa yeyote kati ya hawa watu wawili , James na Kelvin, kufuatana na Mazingira ya wakati huo...Hali zote inabidi tuwe nazo ili kujilinda...Wanawake ni wasanii sana soetimes!
   
Loading...