Mwanamke ni Asset moja nzuri sana ukijua unataka nini kwake

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
6,702
8,480
Habarini mabibi na mabwana

Natumaini sana mu wazima wa afya tele, kila mmoja akiendelea vizuri na mapumziko ya weekend(tumshukuru Mungu) kwa afya na uzima, walioko katika harakati za kutetea afya zao Mungu awasaidie.

Niende moja kwa moja kwenye mada,

Kwa muda mrefu sanaa naona kabisa kuna kitu sijafanya kwenye maisha kuhusiana na swala zima la maendeleo(harakati za kupambana na umaskini kwa kiwango fulani) najiona nimepungua mahali na nahitaji kabisa kufanya kituu.

Kila nikikurupuka huku na huko yaani naona kabisa katika kufanikisha jambo lolote natakiwa tuwe wawili, bila hivyo naona nitafanya juu juu tu, sijui kama hii hali imeshawahi kumtokea mtu

Iko hivi, unaona kabisaaa kuna kitu natakiwa kufanyaa ila unaona/hisi kabisaa kitu hiki ili kikamilike nahitaji uwepo wa mtu fulani kama ni mwanamke au mwanaume, na unaona kabsa kuwa hapa nahitaji jinsia fulani la sivyo utafanya juu juu.

Mwanamke ndugu zangu ni Asset moja nzuri sana chini ya jua hili kama mwanaume ukiweza kujua unataka nini hasa kwa huyo mwanamke hapa naongelea (walio-oa/wanaotarajia), ngoja nikupe mifano, wengi tunapenda kuoa wanawake wenye kazi bassii, ila hatuangalii mbele zaidi

Angalia mifano hii,

1. Wenye taaluma ya Kilimo

Wanaume ukiwa na mke au mchumba wa taaluma hii asee usimwache una vingi vya kumtumia ili kuinua kipata cha familia, huyu unaweza kumtumia kuanzisha "biashara ya ushauri wa kilimo" sasa cha kushangaza utataka uanzishe biashara hii Morogoro mjini au Dsm, au Arusha mjini, ndugu yangu hutapata matokeo chanya

Mchukue nenda nae kwenye vijiji vinavyolima sana, Tanzania hii watu wanalima nenda kaanzishe huko uone utavyofanikiwa, na wewe utalima kirahisi sana, utamtumia mwanamke wako kupata fadhili mbali mbali za wazungu juu ya biashara hiyo, utaanza kuuza na pembejeo za kilimo etc.

Tena wenye taaluma hii kila Halmashauri hua inapewa fungu kwa ajili ya wanawake kutoa mikopo, hebu fikiria upo huko kijijini umeanzisha mradi huo afuu ukaenda halmashauri umehamasisha na wanawake 10 mkajiunga kikundi Mkurugenzi gani wa kuwanyima pesa??

2. Wafamasia

Wengine hawa ukiwa nao ni pesaa tu umeiweka ndani ya nyumba bila kujua, chukua mavyeti hayo yapeleke misungwi, usevya, mpanda kafungue duka la madawa uone pesa zitavyomiminika, unafungua na kituo cha ushauri buureee, wandugu tunakomalia sana mjini kutaka hayo tuyafanyie huko wakati nafasi zimejaa

3. Wamaabara

Hakuna biashara inayolipa vijijini kama maabara, watu wanapima magonjwa kila siku, afu bei unaweza weka mara 2 ya mjini na ukapata watu, una mwanamke ana cheti cha maabara umemweka ndani a asubiria mshahra wa Magufuli na umeridhika, kuanzisha maabara kwa kijijini haizidi hata 6m

4.walio na taaluma za Mifugo

Asee ukitaka wazungu na wafadhili wakupe pesa dili na mifugo hasa Punda, Ng'ombe utapata peaa bwerere, yaani tena ukiwa ni mwanamke watakufadhili kwa kila kitu, ni wewe kuanzisha kijikampuni chako cha kutoa ushauri juu ya utunzaji wanyama, nasema haya kwa uhakika, watumie picha jinsi unavyofundisha

Nenda kwenye mashule omba vipindi vya ziada ufundishe wanafunzi juu ya urafiki na wanyama kulingana na mifugo ya eneo husika watumie picha ukiwa class na ka proposal kako, utasahu shida

5. Mwanamke Mchakarikaji/asieweza kukaa
Mwisho, Sido huwa kuna pesa za buuree kila mwaka, ni wewe tu kwenda na proposal yako unafanya nini, mwanaume usihangaike, yaani mkeo unamweka mbele tu, Pesa zinakuja zenyewe,

Hela za Sido zinaliwa na wachache tu, watu wanajikopesha na kurudisha wanatajirika mnabaki mnashangaa.

Haya yooote kwa mjini yameshajaa na huwezi ukaanzisha ukafanikiwa, jitoe fahamu nenda mbali na mjii,

Akili hizi zinanijia baada ya kutoka mjini na kuingia vijijini na kuona hali halisi ya maisha ya kijijini.

Wandugu mimi sio mwandishi mzuri wa kupangilia hoja, mtanisamehe ila nadhani nimeeleweka.
 
images.jpg
 
Daahh, Hayo nijifunza kwa Baba yangu, mama alikua mwalimu wa Shule ya Msingi, baba alikua welder na maisha yao yamepiga hatua kubwa sana kuliko kawaida ya kueleza
Tatizo ni pale unapompata mwenye kazi ila usijuwe anafanya nini.
Naamini mafanikio ya familia yaani mwanamme ili kufanikiwa anaitaji haya kutoka kwa mke..

1.Utulivu wa akili.

2.Mawazo ya kujenga na

Ikiwa mwanamke atakosa hayo kisha awe na kipato bado itakuwa ngumu kwa familia kuwa na mafanikio ya jumla.
 
Back
Top Bottom