Mwanamke mzuri wa kuoa ni mwalimu.

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,723
9,189
Ukitaka kuoa oa mwanamke ambaye ni mwalimu.
Huwa ni watu wenye hekima, wanaweza malezi kwasababu huwa wanakutana na watoto wengi wa tabia tofauti so wa kwake hawatomshinda.
Ni watu ambao hawawi overworked mara nyingi hivyo anapata muda wa kuwa na familia yake.
Na inasemekana wanaume wengi wenye hela huoa walimu.
Hiyo ni kweli wadau?
Wenye taaluma zingine mbona kazi tunayo.
 
mwanamke mzuri wa kuoa ni
mwanasheria na awe mnyakyusa
awe mzaramo na mwimba taarabu
awe mwanasiasa then muhaya
IZO NDO FLAG ZA KUOA!!!!
 
Ni kweli Husninyo. Halafu pia inapendeza kweli kama mkeo utamwita kwa jina lake au cheo chake. Ukimwita mkeo mwalimu..... atajisikia vizuri kwa kuwa inaonesha heshima yako kwake na hakika nawaambeini ukimwita mwanamke kwa cheo au sifa yake ugomvi ndani ya nyumba utakuwa mdogo sana. Sana. Wanaume tujishushe kwa wateule wetu (Wanawake).

Zaidi ni kweli kuwa walimu huwa wanajua malezi, saikolojia na hufanikiwa ku-handle wanaume zao kwa skills za saikolojia. Halafu mwanaume hupenda kuweka minimum supervision kwa watoto wake. Sasa mke mwalimu anaweza kudeal na watoto vizuri na watoto wa walimu "kwa kawaida" huwahi kujifunza mambo mengi katika utoto wao.
 
mwanamke mzuri wa kuoa ni
mwanasheria na awe mnyakyusa
awe mzaramo na mwimba taarabu
awe mwanasiasa then muhaya
IZO NDO FLAG ZA KUOA!!!!

Mkuu Rose, heshima kwako.
Mi naona kama umeweka utani na hii thread mi naiona ni serious.
 
Nesi! anatibu watoto na kuwapa chakula bora
Daktari hapo ndo haswaa anafaa kabisa
Mwanasheria hafai anaweza kukulima mvua jela
Mtangazaji kama wale wa clouds hafai ataanika mambo ya nyumbani redioni/luningani:A S-alert1:
 
kaka nakubaliana nawewe 100% cos nimeshuhudia na nina uhakika kwamba ni kweli, kwanza walimu wana busara na wana malezi bora katika familia na mpaka shuleni, pili wana upeo wa maendeleo cos wana face chalenge toka kwa wanao wafundisha. sija fanikiwa kupata mchumba mwalimu ila if it hapens then mwalimu ndio the best choice kwa mariage type
 
Kikubwa ni kuoa mwanamke mwenye maadili ya DINI, (yoyote unayoijua). Maana ndani ya dini mambo yote mema yanafundishwa. Wajibu wake kama mama ndani ya nyumba, kama mke kwa mumewe na kama mama kwa watoto wake na watoto wa wanajumuia wenzake. Haijalishi kama Ana kazi, au hana kazi. Haijalishi utaalamu gani anao. Awe mwalimu, mwanasheria, Polisi, Dereva, mwanamuziki, nk
 
Kwa hiyo wote wasiokua walimu wasiolewe? Au hapa mnamaanisha nn? Kama kila mtu aamue kufuata huu ushauri?
 
Ha ha ha ha...
hi thread imenifurahisha maana mie nnaye teacher
wangu almost tabia mlizozieleza ndivyo zilivyo
tatizo lao kwa vile anakaa muda mrefu na wanafunzi
humfanya mmewe kama student vile utaelekezwa hata pasipoelekezwa
utafundishwa hata yasiyofundishika na kuna wakati utafananishwa na wanafunzi wake

ila kwa malezi ya watoto ni namba wani
si unakumbuka ulipokuwa msingi walivyokuwa wanabana
kupigwa round kitu cha kawaida, ndivyo wanavyowabana watoto
wakali hao...
 
Kwa hiyo wote wasiokua walimu wasiolewe? Au hapa mnamaanisha nn? Kama kila mtu aamue kufuata huu ushauri?

Haikusemwa wote wasiokuwa walimu wasiolewe. Haikusemwa wote waliokuwa walimu waolewe.
 
Kwa hiyo wote wasiokua walimu wasiolewe? Au hapa mnamaanisha nn? Kama kila mtu aamue kufuata huu ushauri?

Mkuu tuko pamoja.
ukioa mke sababu tu ni mwalimu nadhani sio sahihi, wapo walimu utulivu ziro.
Mke mzuri ni yule mnaependana kwa dhati na mwenye tabia njema inayokubalika, thats all.
 
Ni kweli Husninyo. Halafu pia inapendeza kweli kama mkeo utamwita kwa jina lake au cheo chake. .

Id yangu ni utata nini? Mimi ni mwanamke. Sawa nitamwita mme wangu kwa cheo chake. Cjui atakuwa mwalimu..!!
 
Mkuu tuko pamoja.
ukioa mke sababu tu ni mwalimu nadhani sio sahihi, wapo walimu utulivu ziro.
Mke mzuri ni yule mnaependana kwa dhati na mwenye tabia njema inayokubalika, thats all.
Imetoka kwenye makabila sasa tumeingia mke wa kuoa kutokana na kazi aifanyao! Kazi kwelikweli!
 
mwanamke mzuri wa kuoa ni
mwanasheria na awe mnyakyusa
awe mzaramo na mwimba taarabu
awe mwanasiasa then muhaya
IZO NDO FLAG ZA KUOA!!!!

da rose upo seriouse? Au umekwazika! Utaolewa na taaluma yako hiyo hiyo.
 
Kwa hiyo unamaanisha nn? Labda sijakuelewa!

Kinachozungumzwa ni tabia za jumla za makundi ya watu katika jamii. Mfano kuna makundi kama walimu, wanasheria, askari, mama lishe, madaktari, wanasiasa n.k. Watu wa kundi moja huwa na tabia zinazowatofautisha na wengine katika makundi tofauti. Hata hivyo si ajabu baadhi ya watu wa kundi moja kuwa na tabia fulani za walio katika kundi jingine. Sasa kilichopo hapa ni mapendekezo kutokana na kundi la walimu. Watu wanaowafahamu walimu (kwa ujumla wao) wanatoa changamoto ambazo kwa sasa ni kupendekeza sifa chanya na hata hasi za wanawake katika kundi hili.
 
Kwa hiyo sisi mamessenger tusiolewe jamani nyie watu mna balaa nyie. Mwanamke mzuri wa kuoa ni yule mwenye tabia na maadili mema, mwenye heshima, adabu, uvumilivu bila kusahau upendo. Hiyo ni taaluma tu hakuna uhusiano na kuolewa
 
Kinachozungumzwa ni tabia za jumla za makundi ya watu katika jamii. Mfano kuna makundi kama walimu, wanasheria, askari, mama lishe, madaktari, wanasiasa n.k. Watu wa kundi moja huwa na tabia zinazowatofautisha na wengine katika makundi tofauti. Hata hivyo si ajabu baadhi ya watu wa kundi moja kuwa na tabia fulani za walio katika kundi jingine. Sasa kilichopo hapa ni mapendekezo kutokana na kundi la walimu. Watu wanaowafahamu walimu (kwa ujumla wao) wanatoa changamoto ambazo kwa sasa ni kupendekeza sifa chanya na hata hasi za wanawake katika kundi hili.

umejibu vizuri.
 
Back
Top Bottom