Mwanamke mwenye uhitaji wa ndoa huwa sio king'ang'anizi

Makau Js

Member
May 25, 2017
93
233
Ukisoma Biblia takatifu ,utakuta neno ndoa limezungumzwa mara 38 katika vifungu 38 ,na ukisoma kitabu cha Methali[ 31:10-31] Mke mwema kweli, apatikana wapi?

''Huyo ana thamani kuliko johari! Mumewe humwamini kwa moyo, kwake atapata faida daima. Kamwe hamtendei mumewe mabaya, bali humtendea mema maisha yake yote.'''

Kizazi hiki wanawake wanahitaji harusi ,na wanaume wanahitaji ndoa,ndio maana katika katika harakati za kufunga harusi wanaume wengi hukonda na wanawake wengi hunenepa sababu ,mmoja anahitaji harusi na mwingine anahitaji ndoa.

Baada ya harusi na safari ya ndoa inapoanza ,mwanamke hukonda na mwanaume hunenepa sababu ,Harusi ni sherehe ya siku moja wakati ndoa ni agano la milele,wanawake wanakamia sana harusi kuliko kukamia ndoa zao.

Mwanamke mwenye uhitaji wa ndoa huwa sio king'ang'anizi wa harusi hata siku moja ,yeye hutizama agano takatifu la ndoa ambayo inaweza kufungwa bila ya harusi wala gharama kubwa .Wanawake wa aina hii kwa kizazi hiki hawapo na wanapatikana kwa kufunga na kusali pekee.

Mwanamke anayehitaji ndoa baada ya kufika katika kilele cha mafanikio ya maendeleo ya ndoa na furaha ya ndoa yake ,hupendekeza kwa mume wake wabariki ndoa ndipo mume wake hupokea shauri la mke wake sababu ya hekima na busara ya mke wake na kuibariki ndoa.

Wanawake ,msilazimishe kufunga harusi wakati uwezo wa
wanaume wenu mdogo,harusi ni sherehe ya siku moja na ndoa ni agano la milele,tuwekekeza fikra za kutengeneza ndoa nzuri na bora na sio kuwa na hamasa ya kutengeneza harusi bora na tamu.

Dear brothers maisha ya sasa yanahitaji mwanamke mwenye akili na sio mwanamke mzuri ,sababu unaweza pata mke mzuri asiye na akili na ukapata mwanamke mwenye akili asiye mrembo-uzuri wa mwanamke huwa haudumu milele ila akili ya mwanamke hudumu milele.To be married by the person you love the most is the greatest blessing God can give.

b32099cf591a5805e94ced66cdf0a3fc.jpg
 
Hakuna neno kubariki ndoa ambayo haipo, kuna neno kufunga ndoa. Nje ya hapo ni kuishi katika uasherati na kuchakazana bila sababu za msingi
 
Sio wote,mbona Mimi siko ivo,..ni hulka ya kibinadamu siku zote haridhiki,..mi mwenyew nimepitia maumivu makali ivo vyote kumwonesha MTU unampenda nikaja kugundua kua watu wawili hawawez kupendana kwa pamoja,mmoja apende mwingine aache,so sikuizi sipend nasubir watu wanipende tu,..sifany makosa mawili mm
 
Acha porojo na upoyoyo

Unafikilia, Babu na bibi zetu wote walikuwa na hizo ndoa za vitabu vya wazungu na Waarabu!?

Ndoa ni mke na mke waishi pamoja, ikitokea wakaza watoto poa.

Vinginevyo ni kuleta vikwazo vya watu kuishi kwa amani.

Mfano, dini nyingi za kilokole zimeharibu mabinti na vijana kwa vigezo uchwara Kama hizo za kufunga ndoa mara sherehe za kabla ya harusi za kipoyoyo na mwisho wake wamejikuta kwenye ndoa za kutojitakia .

Kwa sababu, ya kufanya utaratibu wa kuoa kuwa kama kujiunga na jeshi la marekani.
 
Sio wote,mbona Mimi siko ivo,..ni hulka ya kibinadamu siku zote haridhiki,..mi mwenyew nimepitia maumivu makali ivo vyote kumwonesha MTU unampenda nikaja kugundua kua watu wawili hawawez kupendana kwa pamoja,mmoja apende mwingine aache,so sikuizi sipend nasubir watu wanipende tu,..sifany makosa mawili mm
Ni jukumu lako kupenda, mwanamke ni kukuheshimu tu!!
 
Kila siku wanawake wanawake tu wakati wanaoongoza kushindwa ndoa wanaume,,nenda angalau mtaani kwako kaangalie wanawake wanaolea watoto peke yao baada ya mijanaume kukimbia kwa kisingizio cha maisha magumu..

Achaga uongo wew., !! Kione kwanza.
 
Back
Top Bottom