Mwanamke mwenye shahada ya Uzamili anayefanya biashara ya Makande jijini Mwanza awe chachu kwa Wasomi nchini

Tangu Nancy aanze kuuza hayo makande ana muda gani na ni makande haya haya tunayoyafahamu wengi wetu ambayo mara nyingi uchanganywa mahindi na maharage? Hata hivyo big up kwake kwa ujasiri wa kutafuta mali.
 
Mimi namfahamu mrembo mmoja mkali kuliko Nancy Lema na yeye ana masters yake anauza juice ya matunda fresh lakini haitoki. Anapiga vibarua vidogo vidogo mambo bado magumu. Sasa anakaribia kuuza biashara haramu.

Nancy pia alikuwa na mtaji flani wa kuagiza vitu toka China vya kuongeza thamani (add value) bidhaa yake. Mambo sio rahisi hivyo.

Tumchukulie Nancy kama motivator mzuri basi lakini asiwe kama yeye ndio ameonesha blue print ya kujikwamua wasomi wote waliokosa kuajiriwa.
 
Nancy Lema.... Ok

Nancy Lema ana Masters degree...

.... afu anapika makande. Asante kwa taarifa.

naona umemzungumzika utadhani wote tunamfahamu

Kwanini hawasemi ni mama ntilie na Luna usiku ya makande??!!!? Kuna nini cha tofauti anachofanya? Anapika makande tuu??!! Hembu msitake kulaumu wasomi kisa mfanya biashara ndogo ndogo mmoja, wako waliofungua magenge ya mbogamboga wako wanaolima mchicha na tembele na wanaendelea na maisha kwa furaha, hiyo dogo anauspecial gani wakushangaza??!!!! B
 
Habarini wakuu,

Si kwamba dada Nancy Lema mkazi wa Mwanza amefanya jambo la ajabu sana, lahasha!! Ila angalau amewafuta tongotongo wasomi wengine nchini wenye level za shahada kuendelea ambao kwao neno kukosa ajira rasmi za kuajiriwa na serikali au kampuni kwao ilikua na maana kwamba usomi wao wote ni BURE na si malikitu

Neno SPECIALIZATION ama kujikita kwenye taaluma moja maalum ambayo ndio dhana inayotawala kwenye mfumo wa elimu yetu ya juu ndiko kulikofanya wasomi wetu wakikosa kuzitumikia zile kada walizo specialize basi hujiona wao ni USELESS

Waliowengi husahau kua ubongo wao unaweza kufanya mamilioni ya mambo nje ya yale waliyospecialize kwenye elimu zao ambazo zina kila harufu ya utumwa wa kikoloni "educate africans for using them in white colar jobs"

Wito wangu kwa watanzania wanaojiita wasomi, umefika muda saa kwa sisi kutupa ujinga tuliolishwa mashuleni kwa miaka kadhaa na kuanza kuzitumia akili zetu halisi kutatua matatizo yetu ya kila siku hasa ya kiuchumi

Niliwahi kumsikia msanii mmoja akisema "hivi hesabu ya vipeo na vipeuo vinamsaidia nini dereva wa boda boda"?

Ni wakati sasa kwa watanzania wenzangu ku deal na hizo wanazoziita INFORMAL EDUCATION ambazo kwa wenzetu walioamua kua serious na kuzitumia kama uingereza, India na Uchina wameshaanza kufaidi matunda yake

Sent using Jamii Forums mobile app
Wiki iliyopita nilisema mtaani kwangu yupo mhitimu wa sheria anauza vipande vya matikitimaji na ndizi mbivu, pia yupo mwingine naye ana grosare ya bia na wale wa Morogoro wanaouza mchele ukimuacha yule muuza mitumba wa Ilala, siku hizi si ajabu kama ilivyo si ajabu asiyesoma kuteuliwa uDC!
 
Elimu mwisho wa siku ikuingizie kipato Bila hivyo ni useless.Huyo mwanamke namkubali kasoma sababu anaingiza kipato kupitia kuuza makande.Mimi mtu hawezi kuniambia eti kasoma wakati hana njia ya kuingiza kipato hiyo elimu ambayo hajui hata afanyaje aingize kipato elimu hiyo ? Huyo anakuwa hajasoma hata kama ana PHD
 
mbona mimi nina P.H.D lakini ni dereva boda boda
Wewe umesoma sana sababu baada ya PhD umegundua njia ya kukuingizia kipato hongera ndivyo msomi anatakiwa kuwa.Siyo jitu Lina PhD halijui lifanyaje kuingiza hela wakati darasa la saba anajua cha kufanya kuingiza hela kama kuuza grnge,mama ntilie nk .Wewe umesoma Doctor naikubali PhD yako.
 
Nakupongeza sana dada Nancy Lema. Naomba namba yako ya simu ili nikuchangie na kukusaidia mbinu ya biashara. Uko eneo gani nije nikuchangie?.
 
Acha kubeba taarifa kutoka mitandaoni ingieni mitaani ndo mtaacha kumpost hyo ukienda karume wamejaa kibao wanauza mitumba wengine kilimo cha mkono Sasa mnavyo mzungumzia hyo utadhani ndo kafanya kitu cha ajabu

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona siku izi zile story za akina billy gate,mark zuge.. kuacha chuo azivutii tena,awaajaacha kudandia hustle za watu kwa kigezo cha kuhamasisha,yani amekuja nancy ana masters na anauza makande.hajaelezea chochote kuhusu mhusika na biashara yake.awa jamaa wanapoteza vijana.
 
Back
Top Bottom