Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,709
Nadhani utakua umewahi kusikia hiyo kauli.
Inadaiwa kuwa kuna wanawake ambao mwanaume ukimuoa tu mambo yako yanaparaganyika.Yaani kama ulikua na mafanikio kidogo au sana unaanza kuandamwa na mikosi mpaka unafilisika kabisa.
Jambo la kushangaza sijawahi kusikia mwanaume mwenye nuksi,hapo ndipo napata wasiwasi wa dhana hii kuwa ya ukweli.
Kwanza sijui kama dhana hii ina ukweli na kama ina ukweli ni kwanini ni wanawake tu? Je, tutawezaje kumjua mwanaume aliyeshindwa kuwajibika na mwanaume alioa mwanamke wa aina hii kisha tukamhusisha na dhana hii?
Nahisi hii ni excuse ya wanaume wazembe ili wahalalise uzembe huo.
Kama ni kweli kuna wanawake wana nuksi naombeni uthibitisho halafu mniambie ni kwanini hakuna wanaume wenye nuksi (au wapo? Kwa mujibu wa dhana?)
Vinginevyo mtu atakaeniletea maneno haya nitamuona kama aliyeshindwa kuwajibika tu!