Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake:je ni mmojawapo?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanamke mwenye hekima hujenga nyumba yake:je ni mmojawapo??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Sep 27, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  KAMA SI ANZA SASA USIKUBALI KUHARIBU NYUMBA YAKO

  Sikutegemea kabisa!

  Nimechoka sana kuendelea nkujitahidi kuhakikisha ndoa yetu inakuwa nzuri na inanifanya kuridhika, miaka nenda rudi tumekuwa tunabishana the same thing.
  Sasa tumefika mahali hata hatuwezi kuongelea tatizo lolote katika ndoa yetu, ni kama vile kila mmoja amaona haitawezekana ingawa ndani ya moyo wa kila mmoja kuna vita ya chini chini inaendelea (cold war) ndiyo maana kitu kidogo tu huweza kusababisha moto kuwaka.

  Hakuna raha, hakuna msisimko, hakuna upendo, hakuna kuvumiliana na hakuna ukaribu wa mapenzi ni kama watu wawili tofauti tulioamua kuishi kama kaka na dada wanaogombana katika nyumba.
  Nafahamu hakuna ndoa ambayo ni perfect, hata hivyo nilitegemea hii ndoa yetu iwe ya kuridhisha kwa kiasi fulani.

  Mume wangu hanijali tena, anakuwa excited na natokeo ya mechi ya soka (Asernal huko UK) kuliko mahusiano yetu, hukasirika sana hiyo timu yake ikifungwa huko UK wakati yeye yupo Tanzania na hakasiriki kuumiza feelings zangu mimi mke wake ambaye tunalala akitanda kimoja.

  Hata akifanya kitu kizuri ni kama bahati mbaya katika wajibu wake ila si kwa kupenda au kuamua nimfurahishe mke wangu au kuonesha ananipenda na kunijali.
  Naamini hii si maana ya ndoa ilivyo au inavyotakiwa kuwa , najuta kuolewa na huyu mwanaume pia sijafahamu kama nisingeolewa ningejua ndoa ina mambo magumu kama haya.

  Swali linaloniumiza kichwa ni hivi kwa nini hawezi kutamabua mahitaji yangu kama ilivyokuwa mwanzo? Kwa nini hathamini ndoa yetu kama mimi ninavyothamini?

  Je, nilifanya makosa kuoana nay eye?
  Na je, bado kuna matumaini?
  Ni mimi Jema (si jina la kweli ) miaka 7 kwenye ndoa.

  UFAFANUZI ZAIDI:
  Wanawake wengi hujikuta feelings zako zimaumizwa kama Jema, wao hutegemea baada ya kjuolewa wamepata mwanaume ambaye angempa TRUE LOVE matokeo yake anapewa TRUE FRUSTRATIONS.
  Badala ya maisha ya furaha wamejikuta ni ndanin ya TOTAL DISAPOINTMENT, wamejikuta ndoto zimayeyuka na matarajio au mahitaji yao yakiwa ni ndoto za mchana.

  Tukumbuke kwamba kila mwanamke huwa na ndoto kwamba siku moja atapata MR RIGHT, atampata Prince na yeye kuwa princes, na huyu mwanaume atajitahidi kufanikisha ndoto zake na mapenzi yatakuwa motomoto siku zote za maisha yao na ndoa yao.

  Wakati wa uchumba hufika na binti hujikuta kweli amempata mwanaume wa ndoto zake kwani hakuna tatizo wala kitu unachoona hafai kwani kama ni matching basi imefanywa mbinguni.
  Wanafanana kwani streght za mwanaume zina match weakness za mwanamke.
  Ni mwanaume anayemsikiliza na kumpa mahitaji yote na anaahidi kwamba atajitahidi kuhakikisha ndoa yako unakuwa mfano.
  Macho ya mwanamke hujawa na HOPES na ameamini kwamba amempata wa kumpa TRUE LOVE.
  Kila anayewaona mitaani anawapa mkono wa kheri kwa kuwa siku moja watakuwa mke na mume kwa ndoa safi na kuingie honeymoon kwa madaha na mbwembwe.

  Baada ya kumaliza honeymoon, maisha yanaanza, siku zinaenda, miezi inaenda na miaka inaenda, conflict zinaanza kujitokeza kwani kila mmoja alizawali sehemu tofauti, malezi tofauti na zaidi ni mwanamke na mwanaume wapo tofauti.

  Mume anaanza kupuuza kumsikiliza mke wake tofauti na ilivyokuwa kabla ya kuoana. Mume anaanza kutumia muda mwingi kufanya mambo yake au kuwa na rafiki zake.
  Weekend zikifika anaenda na rafiki zake kutazama sports na kuongea mambo ya business na anarudi nyumbani usiku saa sita bila taarifa kwamba atachelewa.

  Mke amesubiri amechoka na ameamua kulala huku hajala maana anaamini kula na mume ndo raha ya ndoa.
  Mke anaanza kupata shock na kuwa disappointed jinsi prince wake anavyoanza kufanya mambo yake tofauti na matarajio.
  Mke anaanza kujihisi upweke unaanza na hofu kutanda kwenye mawazo yake nini kimetokea kwa mume wake.
  Anajikuta yupoo kwenye njia panda. Maswali yanaanza kujaa kichwani (kumbuka mwanamke ana 8 lanes za kupitisha atraffic za emotions kwenye mind yake).

  Je, nifanyeje nisimkasirishe na wakati huohuo nimwambie anavyofanya ni vibaya na ajirekebishe?
  Je, nilioana na mwanaume sahihi?

  MUHIMU SANA KUELEWA HAYA:
  Hapo juu tunaona contrast kati ya matarajio ya mwanamke na reality ya maisha ya ndoa.
  Matarajio mengi ya wanawake wengi kuhusu ndoa ni UNREALISTIC, si matarajio sahihi, ni vitu ambavyo katika maisha ya kweli kwenye ndoa huwezi kuvipata, ni illusions kama vile movie.

  Wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawana matarajio kwamba kwenye ndoa kuna conflict, kuna kuumizwa, kuna hasira, kuna majaribu, kuna shida, dhiki, tabu na kwamba hivyo vyote ni sehemu ya ndoa kwani ndoa ni mwanaume na mwanamke ambao kila mmoja ni NOT PERFECT ana matatizo yake si malaika.

  Kujiandaa na kuwa tayari kwa ndoa ni pamoja na kufahamu kwamba kwenye ndoa kutakuwa na CHALLENGES ambazo kwa kushirikiana mke na mume wataweza kuzishinda na zaidi kuwa na ndoa sawa na NDOTO ZAO.
  Kuamini kwamba umejiandaa vizuri kwa ndoa na kwamba ukikutana na HUGE DISAPPOINTMENT na kudhani kwamba si sahihi hii ina maana bado hukujiandaa kwa ndoa kwani ulikuwa na upande mmoja tu kwamba ndoa ni tambarare kama mawindoni.

  Kuna msema kwamba:
  “Marriage is a Romance in which the Hero dies in the fuirst chapter”
  Hivyo badi kumbuka kwamba upendo wa mwanzo (honeymoon) ni fantasy ni siku halisi ni illusions upendo wa kweli hujengwa baada ya wawili kuvunjwa vunjwa na shida na matatizo na kushinda pamoja na kukiri wenyewe kwamba kweli mimi na mwenzangu tumetoka mbali.

  Ukikutana na disappointment kwa mara ya kwanza katika ndoa yako usiinue macho kuangalia wanaume wengine kwenye ndoa zingine na ukajiona wewe ulikosea kumpata huyo mume wako bali shukuru Mungu kwa hayo unapitia na jambo la msingi kwa hazina kubwa ua upendo uliyonayo huku ukimuomba Mungu anza kuchimbua hazina ya ushujaa wa mume wako na kuijenga ndoa upya ili iwe na upendo wa kweli.

  UJUMBE MUHIMU:
  Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
  kwa mikono yake mwenyewe.
  Mithali 14:1
   
 2. P

  Preacher JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  IDLE MIND IS THE DEVIL'S WORKSHOP - kama wana ndoa hawako makini kufanya kazi - mwanamke akiwa busy na umbea mitaani, ofisini, kusikiliza udaku na mambo ya ngono (mazungumzo mabaya huharibu tabia njema) - mwanaume naye akiwa busy kudiscuss ngono, macho juu juu kuangalia wanawake wengine - NI UHAKIKA NDOA INAKUWA NA DOSARI - kwani badala ya akili kutulia kwa mmoja uliyemchangua - jinsi ya kujenga familia bora, kutafuta fedha za maendeleo yenu wawili - shetani anapewa nafasi ya kujipenyeza na kuvuruga kusudi lote la ndoa.

  Kama mwanamke kweli yuko makini - 1) atamwombea mwenza wake 2) atamwonyesha upendo 3) hatakuwa na moyo wa kulipiza kisasi - dawa ya moto ni maji na sio moto kwa moto - otherwise moto unakuwa mkubwa zaidi 4) atajaribu kumsaidia mume wake kwa njia za kiroho zaidi kuliko kutumia ushauri wa mashoga.

  Wachumba wanapokuwa na mahusiano ya kimwili hadi kufanya ngono kabla ya ndoa, wanapokuwa watu wa kwenda kwenye club za pombe kila mara kabla ya ndoa; -kutokana na mfumo dume uliopo - mwanamke ajue kuwa wakati yeye analea watoto; mwanaume ataendelea kwenda kwenye starehe alizozoea - inawezekana kukawa na wanaume wachache ambapo wanakuwa stable.

  Watu wawili - wenye background tofauti - inabidi wote wavumiliane, waheshimiane, kila mtu amwone mwenza wake ni bora kuliko yeye, na kujaribu kutengeneza kitu kipya pamoja - waachane na backgrounds zao zilizo tofauti. Kwa neema ya Mungu kama wote wameamua kuwa makini - basi ndoa inaweza kuwa ya raha na furaha.
  Hayo ni mawazo yangu machache
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Sep 28, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mama Mia umesahau ku-acknowledge the source bana.

  Me I hate lawama zinavyopelekwa kwa mwanamke pekee eti mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe !! Phweee

  Mimi nadhani msemo huu unaapply kwa wale wanawake wanaojisahau wanapoolewa but kwa mwanamke ambaye amekuwa akijitahidi kudumisha ndoa yake but mumewe ndo anayemwangusha, ndoa ikivunjika bado ataitwa mpumbavu alovunja nyumba kwa mikono yake mwenyewe??!
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Sore mkuu mambo mengi
  4more info
  www.mbilinyi.blogspot.com
  mungu ambariki kijana huyu natumaini ndoa yake iko na amani all the tym
   
 5. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  mada hii nimeipenda sana, natamani kila mtu aliyepo kwenye ndoa angeweza kuisoma na kuielewa!!
  ndoa kwa sasa zimekuwa ndoana!!
  tunahitaji kubadilika
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  P didy thanks aisee imetulia sana hii sina cha kuoneza kuna baadhi ya vitu nimejifunza humo
   
 7. LD

  LD JF-Expert Member

  #7
  Feb 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Asante mpendwa kwa somo zuri,
  Nitalizingatia, binafsi nimelipenda.
   
 8. tracy

  tracy JF-Expert Member

  #8
  Feb 4, 2011
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hii inatakiwa iende kwa wote,kama mama atakua na hekima na baba atakua mpumbavu them uvumilivu unaeza kummshinda..kumbuka ni rahisi kumuongoza ngamia kwenye kisima ila huezi kumlazimisha anywe maji..kuna wanawake waliyojaribu hadi kufikia kuumwa na magonjwa mengi tu but wanaume hawakubadilika.Hekima na uelewa kwa wanandoa ni muhimu sana,
  kuwa imperfect ni kwa kila mtu ila ukishajua weakness yako,fanya uwezalo kufanyia kazi,sio unajidai kilema wa hicho kitu sasa,hamna kitu kizuri kama kumrekebisha mtu na kweli ukona anajribu,sio lazima awe perfect but alijaribu..
  Mungu anasema TUMTUMAINI YEYE KWA MIOYO YETU NA WALA TUSIZITUMAINI AKILI ZETU WENYEWE TUMKIRI YEYE KWENYE NJIA ZETU ZOTE NAYE ATANYOOSHA MAPITO YETU..so unaeza kubadlika kwa chochote kile.
  Kwa mfano,unapenda sana kuangalia mpira and iko kwenye damu yako,weka priorities zako vizuri,mke wako yuko lonely and unaona kabisa,jaribu kumwabia kama mnaeza kuangalia wote,akisema hapana insist,akikubali..katikati ya game na unaona yuko bored,tell her to lie on your chest or something huku mnawatch,..ni kitu kudogo but ina faida kubwa.
  As a woman,work on the spark vizuri..so kwa mimi hekima,busara,amani,upendo,uelewa na ufaham ni kwa wote wawili ili waweze kweenda na mabadliko,wote wanabadilika so sio kazi ya mwanamke peke yake kupokea mabadlikoya mume but mume nae ajue mwanamke atabadilika na ni jukumu lake kuishikilia familia yake,awe pillar na sio a string that upepo utampeleka kokote.
  binafsi naona ni ngumu sana kumrekebisha mtu ambae hataki,haoni,hasiki,haelewi!yeye yuko perfect saa zote,anaona mna ugomvi wa ndani ila atasema haoni chochote(back to the topic),a happy marriage is built by two people trying their best to work things out kwa upendo,kila mmoja akijua nafasi yake na kufanya majukumu yake huku Mungu akishika njia zao zote.:pray:
   
Loading...